31.
31. Kuepuka Uchoyo na Ubahili
Uchoyo na ubahili ni kinyume cha ukarimu. Mtu mchoyo ana kasoro katika imani yake. Anaona kuwa chochote alichonacho amekipata kwa jitihada na akili yake tu. Pia anahofu kuwa akitoa kumpa mwingine atapungukiwa au atafilisika. Mtume (s.a.w) anatutanabahisha katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Mtu anasema: โHiki changu! Hiki changu! Lakini ukweli ulivyo ni kwamba, vilivyo vyake katika mali yake ni vitu vitatu: โKile alichokula au nguo aliyoivaa ikachakaa au kile alichokitoa sadaqa (hakika) amekiweka akiba, na kingine chochote zaidi ya hivi, hakika si vyake (si vyenye kumfaa) na ataondoka awaachie watu โ. (Muslim)
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: โChakula cha watu wawili kina watosha watu watatu, na chakula cha watu watatu kinawatosha watu wanneโ.(Bukhari na Muslim)
Jabir bin Abdullah (r.a) ameeleza: Mtume w a Allah amesema: โChakula cha mtu mmoja kinawatosha watu wawili na chakula cha watu wawili
kinawatosha watu wanne na chakula cha watu wanne kinawashibisha watu wananeโ. (Muslim).
Hivyo ukizingatia Hadithi hizi, utaona kuwa hapana sababu ya Muislamu kuwa mchoyo au bahili. Uchoyo na ubahili ni tabia mbaya na malipo yake ni kwenda Motoni kama inavyobainishwa katika Qur-an:
Yule anayetoa (zaka na sadaka) na kumcha Mwenyezi Mungu. Na kusadiki jam bo jem a (akalifuata). Tutamsahilishia njia ya kw enda Peponi. Na afanyae ubakhili, asiwe na haja ya viumbe wenzake, na akakadhibisha mambo mema (asiyafanye). Tutamsahilishia njia ya kwendea Motoni. Na mali yake haitamfaa atakapokuwa anadidimia (Motoni humo). (92:5-11).
Umeionaje Makala hii.. ?
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุฑูููุฑูุฉู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ููุงูู: ููุงูู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู "ุฅููู ุงูููููู ุทููููุจู ููุง ููููุจููู ุฅูููุง ุทูู...
Soma Zaidi...