image

Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake

30.

Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake

30. Kuwa MkarimuUkarimu ni miongoni mwa tabia njema anayotakiwa ajipambe nayo Muislamu.Muislamu anatakiwa awe mwepesi wa kuwakirimu wengine kwa kuwasaidia wakati wanapokuwa katika hali ya kuhitajia msaada bila ya kutarajia malipo yoyote kutoka kwao. Sifa ya wakarimu inabainishwa katika aya zifuatazo:Na huwalisha chakula maskini na mayatima na wafungwa, na hali yakuwa wenyewe wanakipenda (chakula hicho). (Husema wenyewe katika nyoyo zao wanapowapa chakula hicho): “Tunakulisheni kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala shukurani”. (76:8-9)
Pia kumfanyia mgeni takrima ni jambo lililowajibishwa kwa Waislamu, kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema, “Yule anayemuamini Allah(s.w) na siku ya mw isho hatamdhuru jirani yake, na yule anayemuamini Allah(s.w) na siku ya mwisho atamkirimu mgeni wake na yule anayemuamini Allah na siku ya mwisho ataongea mazuri au atakaa kimya ”. (Bukhari na Muslim).Abu Shuraikh Ka ’ab (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema, “Yeyote anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho hanabudi kumkirimu mgeni wake, na jukumu lake (la kumhangaikia sana) ni mchana mmoja na usiku.Ukarimu (kwa mgeni) ni siku tatu na zaidi ya hapo ni sadaqa. Si vyema kw a mgeni kuendelea kubakia baada ya siku tatu na kuendelea kumuweka mwenyeji wake katika hali ya uzito.” (Bukhari na Muslim).
Kiigizo chetu cha ukarimu ni Mitume wa Allah. Tunafahamishwa katika Qur-an juu ya ukarimu wa Nabii Ibrahim:


Je! Imekujia hadithi ya wageni wahishimiwao wa (Nabii) Ibrahimu? Walipoingia kw ake w akasema: “Salaam (alaykum)”. Na (yeye Ibrahimu) akasema: (“Alaykumus) Salaam” (Na katika moyo wake anasema): “Ninyi watu nisiokujueni”. Mara akaenda kwa ahali yake na akaleta ndama aliyenona. Akampeleka karibu yao. (Walipokuwa hawajanyosha mikono kula) alisema: “Mbona hamuli!” (51:24-2 7)


Katika hadithi, amesimulia Ibn Abbas (r.a) kuwa: Mtume (s.a.w) alikuwa mkarimu sana kuliko watu wote na alikuwa akizidisha ukarimu katika mwezi wa Ramadhan...” (Bukhari).
Malipo ya kuwakirimu watu ni kupata takrima ya Allah (s.w) huko Peponi kama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:


“Basi Mw enyezi Mungu ataw alinda (waka rim u) na shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha.(76:11)Na atawajaza mabustani (ya Peponi) na maguo ya hariri, kwa sababu ya kusubiri (kwao). Humo wataegemea viti vya enzi, hawataona humo jua (kali) wala baridi (kali).(76:12-13)


Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yake yataning’inia mpaka chini. Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae.(76:14-15)Vigae vya fedha; wamevijaza kwa vipimo. Na humo watanyweshwa kinywaji kilichochanganyika na tangawizi. Huo ni mto ulio humo (Pep oni) unaitwa Salsabili. Na watawazungukia (kuwatumikia),wavulana w asiochakaa, ukiw aona utawafikiri ni lulu zilizotaw anyw a. (76: 16-19)


Na utakapoyaona (yaliyoko) huko utaona neema(zisizo kuwa na mfano) na ufalme mkubwa. Juu yao wana nguo za hariri laini, za kijani kibichi na za hariri nzito. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao ataw anyw esha kinyw aji safi kabisa (76:20-21)


“Hakika haya ni malipo yenu; na amali zenu zimekubaliwa ”. (76:22)
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 238


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mawaidha Kutokwa kwa Shekhe
Karibu kwenye Darsa za mawaidha na Mafundisho ya dini. Soma Zaidi...

Aina za hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake
30. Soma Zaidi...

Faida za Kuwa mwenye Subira na Uvumilivu
29. Soma Zaidi...

Husaidia wenye matatizo katika jam ii
Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada. Soma Zaidi...

Husimamisha swala
Husimamisha swala katika maisha yao yote. Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE. Soma Zaidi...

Zoezi - 2
1. Soma Zaidi...

(xiii)Huwa muaminifu
Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Soma Zaidi...

jamii somo la 26
(vii)Hufanya bias hara na Allah (s. Soma Zaidi...

Uandishi wa hadithi wakati wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Uhakiki wa hadithi za mtume
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...