38.
38. Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)
Muumini wa kweli anayemtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kila hali hana budi kuwa na msimamo thabiti katika kuusimamisha na kuufuata Uislamu. Si muumini wa kweli yule anayeyumba yumba (mudhabidhabina) kwa kuchanganya haki na batili au utii na uasi katika kuendesha maisha yake ya kila siku. Mwenyezi Mungu (s.w) ametuamrisha wale tutoao shahada ya kweli tuuingie Uislamu wote au tuwe Waislamu katika kila kipengele na kila hatua ya maisha yetu na wala tusiuingie nusu nusu. Anatuamrisha:
Enyi mlioamini! ingieni katika Uislamu wote, wala msifuate nyayo za shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri. (2:208)
Hivyo, kutamka tu shahada au kusema: “Tunakiri kuwa hapana Mola ila Mwenyezi Mungu na Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake” haitoshi kutufanya kuwa Waislamu wale walioahidiwa malipo makubwa huko akhera; bali tutakuwa wa kweli katika shahada zetu iwapo tutaendesha
maisha yetu yote kama alivyotutaka tuishi Mwenyezi Mungu (s.w) na kama alivyotuelekeza Mtume wake (s.a.w). Waislamu watakaokuwa imara katika kuutekeleza Uislamu katika maisha yao ya kila siku, ndio walioahidiwa malipo makubwa ya Peponi katika maisha ya Akhera. Hebu turejee aya chache zifuatazo:
“Wale waliosema: Mola wetu ni Mwenyezi Mungu kisha wakabakia imara (wakawa na msimamo), hao huwateremkia Malaika (wakawaambia), “Msiogope wala msihuzunike, na furahini kwa Pepo mliyokuwa mkiahidiwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata vitu vinavyopendwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka ”. (41:30-31).
Hakika wale waliosema: “Mola wetu ni Mwenyezi Mungu’, kisha wakatengenea (wakawa na msimamo) hawatakuwa na khofu (siku ya kufa kwao wala baadaye) wala hawatahuzunika. Hao ndio watu wa Peponi, watakaa humo (milele); ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyatenda. (46:13-1 4).
Hebu pia tuone jinsi Mtume (s.a.w) alivyotuwaidhi juu ya kuwa na msimamo katika Uislamu wetu:
Sufyaan bin Abdullah (r.a) amesimulia kuwa alisema: Ee! Mtume wa Allah niambie neno juu ya Uislamu ambalo sitakuwa tena na haja ya
kumuuliza mtu mwingine baada ya hapa. Alisema Mtume(s.a.w); ‘Sema: Ninamuamini Mwenyezi Mungu kisha ubakie katika msimamo huo”. (Muslim)
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Fuata barabara njia sahihi ya imani na kuwa na msimamo huo, na ujue kwamba hapana yeyote atakayeokoka kutokana na amali yake (nzuri). Mmoja akauliza: Hata wewe Mtume wa Allah? Akajibu (Mtume) hata mimi, ila mpaka Allah anikunjulie Rehema zake na Fadhila zake. (Muslim)
Enyi mlioamini! Kwanini mnasema msiyoyatenda. Ni chukizo kubwa mbele ya Allah kusema msiyoyatenda.
(61:2-3)
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 572
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Madrasa kiganjani
Zijuwe Faida za Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)
38. Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa mtume (s.a.w)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
NENO LA AWALI
Darasa la elimu inayohusu ujauzito na namna ya kulea mimba Soma Zaidi...
Majina ya vijana wa pangoni
Makala hii inakwenda kukutajia majina ya vijana saba wa pangoni Soma Zaidi...
Zoezi la 5
Maswali mbalimbali kuhusu fiqih Soma Zaidi...
Maswali juu ya hadithi
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya) Soma Zaidi...
KULA HALALI NA ZILICHO KIZURI NI AMRI KATIKA UISLAMU
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "إنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إلَّا طَي... Soma Zaidi...
(xvi)Huepuka ugomvi na mabishano
Waumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano. Soma Zaidi...
Fadhila za kujenga msikiti
Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah. Soma Zaidi...
Epuka kuwa muoga na yajue madhara ya uwoga
36. Soma Zaidi...
sura ya 02
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...