32.
32. Kuwa Mwenye Kutosheka
Kutosheka ni kuridhika na neema uliyonayo. Kutosheka ni utajiri kuliko utajiri wote uliopo ulimwenguni.
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema, utajiri si kuwa na mali nyingi lakini utajiri ni kutosheka”. (Bukhari na Muslim)
Muislamu anatakiwa awe ni mwenye kutosheka na kile alichoruzukiwa na Mola wake. Kila mtu amekadiriwa riziki yake na Allah (s.w). Hakuna mwenye uwezo wa kumpunguzia au kumzidishia mtu riziki. Hili linabainishwa katika Qur-an katika usia wa Mzee Luqman kwa mwanawe:
Ewe mwanangu! Kwa hakika jambo lolote lijapokuwa na uzito wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni au katika ardhi, Mwenyezi Mungu atalileta (amlipe mstahiki); bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo yaliyofichikana, (na) Mjuzi wa mambo yaliyo dhahiri. (31:16)
Pia Allah (s.w) anatuhakikishia:
“Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Allah...” (11:6)
Juu ya moyo wa kutosheka Mtume (s.a.w) anatuwaidhi katika Hadithi ifuatayo:
Imesimuliwa katika mamlaka ya Abdullah Bin Amr bin al-’As (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: “Yule aliyeingia Uislamu na akajaaliwa kupata riziki inayotosheleza mahitaji yake muhimu na Mwenyezi Mungu akamfanya kuwa mwenye kutosheka na kila alichotunukiwa, hakika amefuzu kikweli”. (Muslim)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي حَمْزَةَ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ خَادِمِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه ?...
Soma Zaidi...Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...