32.
32. Kuwa Mwenye Kutosheka
Kutosheka ni kuridhika na neema uliyonayo. Kutosheka ni utajiri kuliko utajiri wote uliopo ulimwenguni.
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema, utajiri si kuwa na mali nyingi lakini utajiri ni kutoshekaโ. (Bukhari na Muslim)
Muislamu anatakiwa awe ni mwenye kutosheka na kile alichoruzukiwa na Mola wake. Kila mtu amekadiriwa riziki yake na Allah (s.w). Hakuna mwenye uwezo wa kumpunguzia au kumzidishia mtu riziki. Hili linabainishwa katika Qur-an katika usia wa Mzee Luqman kwa mwanawe:
Ewe mwanangu! Kwa hakika jambo lolote lijapokuwa na uzito wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni au katika ardhi, Mwenyezi Mungu atalileta (amlipe mstahiki); bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo yaliyofichikana, (na) Mjuzi wa mambo yaliyo dhahiri. (31:16)
Pia Allah (s.w) anatuhakikishia:
โNa hakuna mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Allah...โ (11:6)
Juu ya moyo wa kutosheka Mtume (s.a.w) anatuwaidhi katika Hadithi ifuatayo:
Imesimuliwa katika mamlaka ya Abdullah Bin Amr bin al-โAs (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: โYule aliyeingia Uislamu na akajaaliwa kupata riziki inayotosheleza mahitaji yake muhimu na Mwenyezi Mungu akamfanya kuwa mwenye kutosheka na kila alichotunukiwa, hakika amefuzu kikweliโ. (Muslim)
Umeionaje Makala hii.. ?
ุนููู ุฃูุจูู ุญูู ูุฒูุฉู ุฃูููุณู ุจููู ู ูุงูููู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฎูุงุฏูู ู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ุนููู ุงููููุจูููู ุตูู ุงููู ุนููู ?...
Soma Zaidi...Maswali mbalimbali yanayohusu elimu ya dini ya kiislamu na mwongozo wa elimu na elimu mazingira.
Soma Zaidi...Kipengele hichi kina maswali mbalimbali kuhusiana na dini na mitazamo mbalimbali.
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...