Navigation Menu



Mtazamo wa Uislamu juu ya usawa kati ya mwanaume na mwanamke

Mtazamo wa Uislamu juu ya usawa kati ya mwanaume na mwanamke

Mtizamo wa Uislamu juu ya Usawa kati ya Mwanamke na Mwanamume



Usawa kati ya mwanamume na mwanamke katika Uislamu umetokana na suala Ia lengo Ia maisha ya mwanaadamu hapa duniani na namna ya kulifikia. Tumeona kuwa madai ya usawa kati ya mwanamume na mwanamke katika nchi za Ulaya, Marekani na katika nchi za Kikomunisti, yametokana na hali halisi ya mazingira yao. Kaitka nchi za Ulaya na marekani madai ya usawa kati ya wanawake na wanaume ni zao Ia hali ngumu ya maisha wakati wa maendeleo ya viwanda.


Na katika nchi za Kikomunisti, hasa Urusi, madai ya usawa msingi wake ni kutoa "Bakshishi" kwa wanawake baada ya kushiriki kwao kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha mapinduzi ya Urusi ya Oktoba, 1917 (The Great Otober Russian Revolution). Katika Uislamu sheria ya usawa kati ya mwanamume na mwanamke sio zao Ia hali yoyote ya mazingira bali imezingatia suala zima Ia lengo Ia kuumbwa mwnaadamu na nafasi yake hapa duniani.


Ni katika utaratibu wa Allah (s.w) ili kuyawezesha maisha ya viumbe yaendelee na kufikia lengo lililokusudiwa ameumba vitu viwili viwili ambavyo kimoja hakijitoshelezi mpaka mwenziwe awepo kama vile usiku na mchana, utamu na uchungu, uhai na umauti, chanya na hasi, kike na kiume, n.k. Ni pale tu jozi hizi za vitu viwili zitakapo shikamana ndipo kitakapotokea kitu kamili. Allah (s.w) anatufahamisha hili kaitka Qur'an:


Na hakika katika kila kitu tumekiumba dume najike iii mpate kufahamu (51:49). Kwa hiyo mwanamke kuwa kama alivyo si ishara ya udhaifu wala mwanamume kuumbwa kama alivyo si ishara ya ukamilifu. mume na namke hawababudi kuishi maisha ya kusaidiana ili kufanya kitu kimoja kizima ili maisha yawezekane na yafikie lengo lake. Kiasili na wanamke wako sawa katika maeneo yafuatayo:



1. Asili yao ni moja
Tunafahamishwa katika Qur'an kuwa usawa kati ya mwanamume na mwanamke umekuwepo tangu mwanzo wa kuumbwa Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi moja na akamuumba mkewe katika nafsi ileile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao. Na Mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana (mnategemeana). Na (muwatazame) jamaa. Hakika Mwenyezi Mungu ni mlizijuu yenu (anayeyaona kila mnayoyafanya). (4:1).



Katika aya hii tunafahamishwa kwa uwazi kuwa mwanadamu asili yake ni moja na tunasisitizwa kufanyiana wema baina yetu, jambo ambalo iwapo hatutalifanya, Mwenyezi Mungu (s.w) atatauadhibu vikali. Tofauti za kimaumbile, tofauti za kjjinsia, tofauti za mazingira na wakati na tofauti nyingine kama hizi, sizo zinazomfanya mwanadamu mmoja awe bora kuliko mwingine, au kumfanya mwanamume awe bora kuliko mwanamke, bali aliye bora zaidi ya wengine ni yule amchaye Mwenyezi Mungu zaidi ya engine.


Tunajifunza hili katika aya ifuatayo: Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja, Adam) na (yule yule) mwanamke (mmoja Hawa). Na tumekufanyeni matafa na makabila (mbali mbali) ili mjuane. Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu ni yule amchaye Mwenyezi Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mwenye khabari (zote). (49:13).



2. Lengo Ia kuumbwa kwao ni moja
Jambo lingine linalosisitiza usawa kati ya mwanamke na mwanamume ni usawa wa lengo Ia kuumbwa mwanadamu. Lengo Ia maisha ya mwanaadamu hapa ulimwenguni Iinadhihirishwa katika Qur'an: "Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu ". (51:56)



Kumuabudu Allah (s.w) ni kuishi maisha yote kwa kufuata hukumu Zake (s.w) katika kuendesha maisha ya kila siku kaitka nyanja zote za maisha. Katika aya mbali mbali za Qur'an tunafahamishwa kuwa wanaume na wanawake watalipwa sawa sawa kulingana na amali zao ya kujali jinsi yao. Hebu turejee aya zifuatazo:


Mola wao akawakubalia (maombi yao kwa kusema): "Hakika mimi sitapotezajuhudi ya mfanyajuhudi miongoni mwenu akiwa mwanamume au mwanamke, kwani nyinyi ni nyinyi kwa nyinyi " (3:195).


Na watakaofanya vitendo vizuri, wakiwa wanaume au wanawake, hali wao ni wenye kuamini, basi hao wataingia peponi wala hawatadhulumiwa hata tundu ya kokwa ya tende. (4:124).



Mwenyezi Mungu amewaahidi wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake (Amewaahidi) mabustani yapitayo mito mbele yake wakae humo daima na makazi mazuri kwenye mabustani hayo yenye kudumu. Na radhi za Mwenyezi Mungu ndizo kubwa zaidi. Huko ndiko kufuzu (kufaulu) kukubwa (9:72).



3. wote wamekusudiwa kuwa Makhalila wa Allah (s.w) katika jamii Jambo lingine linalodhihirisha usawa kati ya wanaume na wanawake katika Uislamu ni hadhi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni. Mwanaadamu ameletwa hapa ulimwenguni ili awe Khalifa wa Allah (s.w) katika ardhi hii kama tunavyojifunza katika Qur'an:


Wakati Mola wako alpowaambia Malaika: 'Mimi nitaleta katika ardhi Khalfa (wangu,)." Wakasema: Utaweka humo watakaofanya uharibfu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutukuza kwa sfa na kukutaja kwa utukufu wako? Akasema (Mwenyezi Mungu): "hakika mimi najua msiyoyajua ". (2:30).



Katika aya hii tunajifunza kuwa mwanaadamu amekusudiwa kuwa Khalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni. Kuwa Khalifa wa Allah (s.w) ni kuwa kiongozi kwa niaba ya Allah (s.w) hapa ulimwenguni. Yaani kuutawala ulimwengu kwa kufuata mwongozo na sheria za Allah (s.w). Pia tunajifunza kuwa cheo cha Ukhalifa ni cheo chenye hadhi kubwa sana


kiasi kwamba malaika walimuonea wivu mwanaadamu na kupendekeza kuwa wao ndio stahiki kupata cheo hicho.
Katika aya hii hatuoni ubaguzi wowote kati ya mwanamume na mwanamke bali tunafahamishwa kuwa watakao chukua cheo hiki ni wanaume na wanawake watakao muamini na kumtii Allah (s.w) ipasavyo:


Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri, kuwa atawafanya makhalfa (watawala) katika ardhi kama alivyowafanya Makhalfa wale waliokuweko kabla yao, na kwa yakini Atawasimamishia dini yao, Aliyowapendelea, na Atawabadilishia amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote (24:55).



Hivyo ukhalifa ni kwa wote wanawake na wanaume. Kila mmoja anao wajibu wa kusimamisha ufalme wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni kwa kila mmoja kutekeleza jukumu lake alilopangiwa katika jamii kulingana na umbile, uwezo, vipawa, bahati na fursa alizotunukiwa.



4. Hakuna dhambi ya asili
Suala Ia dhambi ya asili anayonasibishiwa nayo mwanamke kama tulivyoona katika maandiko ya Wakristo, halipo kabisa katika Uislamu. Katika maandiko hayo, Hawa ndiye pekee aliyeonekana mkosaji katika kuvunja amri ya Mwenyezi Mungu ya kula tunda kutoka kwenye ule mti ulioharamishiwa. Katika Qur'an tunajifunza kuwa wote walikuwa wakosaji mbele ya Allah (s.w) na wote walitubia na kusamehewa.



Na tukasema: Ewe adam! Kaa wewe na mkeo katika bustani hii na kuleni humo maridhawa popote mpendapo lakini msikurubie mti huu tu, ms/e kuwa miongoni mwa waliodhulumu. (lakini) shetani (yule Iblis adui yao) aliwatelezesha wote wawili wakakhalfu amri ile, wakala katika mti huo walio katazwa na akawatoa katika ile (halO waliyokuwa nayo..." (2:35-36).


(Kisha Allah (s.w) akasema): Na wewe Adam kaa peponi pamoja na mkeo na kuleni mnapopenda lakini msikurubie mti huu ms/e kuwa miongoni mwa waliodhulumu (nafsi zao). Basi shetani aliwatia wasi wasi ili kuwadhihirishia aibu zao walizofichiwa na akasema: "Mola wenu hakukukatazeni mti huu ila (kwa sababu hii): ms/e kuwa malaika au kuwa miongoni mwa wakaao milele (wasfe). Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni mmoja wa watoa usharui mwema kwenu. (7:19 -21)



Basi akawateka (wote wawili) kwa hadaa yake. Na walipouonja mti ule, aibu zao ziliwadhihirikia na wakaingia kujibambikiza majani ya peponi. Na Mola wao akawaita (na kuwauliza): Je, sikukukatazeni mti huu na kukwambieni ya kwamba shetani ni adui yenu aliyedhahiri? Wakasema: "Mola wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na kama hutatusamehe na kuturehemu, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye khasara (7:22-23).



Kutokana na aya hizi wote wawili, Adam na Hawa, walikosa na wote walitubia na kusamehewa. Hivyo hapana tena dhambi yaAsili. Hata kama Adam na Hawa wasingali samehewa haingelikuwa dhambi hii iendelee kwa watoto wao na kizazi chote cha binadamu kwani Allah (s.w) si mwenye kuonea waja wake na ni katika utaratibu wake kuwa hambebeshi mtu mzigo USiO muhusu.


"... Wala mbebaji (mizigo yake ya dhambi) hatabeba mizigo ya mwingine. Kisha marejeo yenu (nyote) ni kwa Mola wenu..." (6:164).
Wala isichukuliwe kuwa Adam na Hawa kutolewa Peponi na kuletwa hapa ulimwenguni kuwa ni adhabu kwani ilibainishwa tangu mwanzo kabla ya kuumbwa kwao, kuwa wao ni Makhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni.


Pamoja na kuona msimamo wa Sharia ya Kiislamu juu ya usawa kati ya mwanamume na mwanamke, hatuna budi kutafakari "usawa" huu kwa undani zaidi. Hatuna budi kufahamu kuwa kuna "usawa" wa sheria na usawa wa maumbile. Uislamu unasimamisha usawa wa sheria. Binaadamu wanaweza kuwa sawa kisheria lakini ni jambo lisilowezekana kupata usawa wa maumbile, vipaji, uwezo, bahati, fursa, n.k. kati ya wanadamu. Ukweli ni kwamba hakuna watu wawili, hata kama ni mapacha (identical twins), walio sawa moja kwa moja. Wanaadamu wanatofautiana sana katika wajihi, akili, uwezo, vipaji, majukumu, na kadhalika. Hizi ni tofauti za kimaumbile anazozaliwa nazo mwanaadamu. Tofauti hizi za kimaumbile sizo zinazoleta tofauti za hadhi na haki miongoni mwa watu bali kinachofanya watu watofautiane katika kupata hadhi na haki wanazostahiki ni sheila, mila na desturi za jamii. Ni wajibu wa jamii kuondoa sheria, mila na desturi zinazoondoa usawa miongoni mwa watu katika jamii na kubakisha tu zile sheria, mila na desturi ambazo humpa kila mtu hadhi na haki zake na kumwezesha kutoa kwa ukamilifu mchango wake katika kuistawisha na kuiendeleza jamii.



Uislamu unapinga vikali ule usawa unapigiwa zumari na matwaghuti wa kumtoa mwanamke awe sawa na mwanamume kimaumbile kivipawa na kimajukumu na nakumfanya mke asiwe mwenza wa mume bali kila mmoja ajitegemee kimaisha na kuwa mshindani wa mwenzake katika uchumi, siasa, n.k. hatima ya usawa wa ama hii, kama tulivyoona katika nchi ya Ulaya na Marekani, ni kuua taasisi ya familia, kuivuruga jamii na kumdhalilisha mwanamke kwa kiasi kikubwa.



Uislamu unasisitiza sana usawa kati ya mke na mume na kati ya binaadamu wote kwa ujumla lakini pamoja na kuzingatia tofauti za kimaumbile,kivipawa na kimajukumu zilizopo. Kutokana na tofauti hizi za kimaumbile utamkuta mwanamke ana uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu fulani ambayo ni muhimu kwa maisha ya mwanaadamu katika jamii. Hivyo hivyo, utamkuta mwanamume anafursa na uwezo wa kutekeleza majukumu mengine zaidi kuliko mwanamke.


Kuna baadhi ya majukumu anayoweza mwanamke peke yake na mwanamume hana uwezo nayo. Kwa mfano, kubeba mimba, kuzaa mtoto na kumlea mpaka afikie umri wa miaka miwili, ni jukumu analolibeba mwanamke peke yake. Je, katika kutekeleza jukumu hili, mwanamke huyu atakuwa na uwezo mkubwa tena wa kushiriki kwa ukamilifu katika uchumi, siasa, na katika shughuli nyinginezo muhimu za jamii? lkumbukwe kuwa jukumu hili moja Ia kuzaa na kulea mtoto ni kubwa sana Iinalochukua muda mrefu, miezi 30 kama Allah (s.w) anavyotufahamisha katika aya ifuatayo:


Na tumemuusia mwanaadam afanye wema kwa wazazi wake. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na akamzaa kwa taabu. Na kubeba mimba yake hata kumwachisha ziwa (kwa uchache) ni miezi thelathini (46: 15).



Katika muda huu wote sehemu kubwa ya akili na fikra ya mama huyu imeelekezwa katika jukumu hili kwa kiasi kwamba humfanya asiwe na umakini katika shughuli nyingine yoyote ile. Je, kama tutadharau ukweli huu tukaendelea kudai kuwa wanawake na wanaume wako sawa katika kutekeleza majukumu mengine yote ya msingi ya jamii, kama vile uchumi, uongozi n.k. huoni kuwa mwanamke anakandamizwa kwa kuvishwa majukumu mengi na mazito kuliko mwanamume? Kumdanganya mwanamke kuwa kuacha kazi ya kulea watoto nyumbani na kwenda shambani, ofisini au kiwandani ndio kujikomboa kwake na kuwa sawa na wanaume ni;-



Kwanza, kumlaghai na kumnyonya. Chukua mfano wa mume na mke wanaofanya kazi ofisini. Mke asubuhi, wakati mumewe anaendelea kulala, ataamka mapema kuhakikisha kuwa ataondoka nyumbani akiwa ameiacha nyumba katila hali nzuri. Kisha baada ya mumewe kuamka atamhudumia ili wawe tayari kuondoka. Baada ya kazi wote hurudi nyumbani pamoja lakini wakati baba anapumzika, mke hujishughulisha na kufahamu watoto walivyolishwa, walivyofuliwa, walivyokogeshwa na husikiliza shida zao nyingine mbali mbali. Huhakikisha watoto na watu wote nyumbani wanakula na kulala. ndio naye alale. Je, huu si utumwa wa hiari kwa mwanamke huyu? Je, huoni wanamke wa namna hii hufanya kazi maradufu ya ile ya wanaume - kazi ya ofisini na kazi ya malezi? ,Je, kama mama naye, kwa kudai usawa, ataamua abakie na kazi ya ofisini tu, familia yenye mshikamano na utulivu itapatikana? Je, ni nani anayempa mwanamke haki zake na kutetea usawa, huyu anayemng'ang'aniza aende ofisini au Uislamu unaompunguzia mwanamke majukumu ya kuhemea na. kumbakishia majukumu ya kuzaa na kulea watoto, kutunza mali ya mumewe, kumliwaza na kumfariji arudipo kazini?



Pili, kumpachika mwanamke majukumu mengine zaidi ya lile Ia kuilea familia ni kumpunguzia ufanisi na kuidodesha jamii. Mwanamke mwenye mimba na watoto wa kulea nyumbani, akiwa mwanaadamu wa kawaida, unadhani ataweza kufanya kazi yake ofisini kwa ufanisi? Atafanyaje kazi vizuri na iii hali ni mgonjwa kwa kipindi chote cha ujauzito? Kama ataiweka familia yake vizuri ni wazi kuwa kazi za ofisini zitadorora. Na atakapo jifungua itambidi achukue likizo ya uzazi ya miezi mitatu. Hata baada ya miezi mitatu ya likizo, fikra zake zitakuwa kwa mtoto wake mpaka angalau miaka miwili itimie. Tuseme mathalan, wanawake 1000 walioshika nafasi muhimu katika uchumi na uongozi wa jamii wawe wamechukua likizo ya uzazi miezi mitatu, muda huu wote nani atakaye fanya kazi zao?



Tatu, kudharau kazi ya malezi ya familia. Malezi ya familia ni kazi muhimu sana kwa jamii inayotaka maendeleo ya vitu na maadili. Kuikuza na kuilea familia katika maadili ni kazi muhimu inayotaka ifanyike kwa uangal ifu na kwa upendo na huruma za mzazi. Hakuna mtaalam yoyote anayeweza kuifanya kazi hii vizuri isipokuwa mama watoto mwenyewe.



Ni katika msingi huu Sheria ya Kiislam imemuondolea mwanamke majukumu yote ya nje ya nyumba yake na kumbakishiajukumu Ia uzazi, ulezi na utunzaji wa nyumba na mali ya mumewe. Mtume (s.a.w) amesema: Mwanamke ni Malikia wa nyumba ya. mume wake na atakuwa. masuuli juu ya. wajibu wake huu. (Bukhari,).



Kwa ajili ya umuhimu wake kuwepo nyumbani saa zote, mwanamke amesamehewa Ibada zote zinazofanywa nje ya nyumba. Kwa mfano si lazima kwake kuswali swala ya ljumaa na amesamehewa kwenda msikitini kwa swala za jamaa japo ameruhusiwa kwenda akitaka. Vile vile Si faradhi kwa mwanamke kwenda Jihad japo hawakatazwikwenda hasa pale msaada wao utakapo hitajika. Kwa ujumla Uislamu haumtaki mwanamke kutoka toka nyumbani kwake ila kwa haja maalum. Amri ya wanawake kubakia katika majumba yao inadhihirika katika aya ifuatayo:


Na kaeni majumbani mwenu, wala msionyeshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za ujahili ... (33:33).
Pamoja na amri hii wan awake wameruhusiwa kwa haja maalum kutoka nje ya nyumba zao. Kwa mfano mwanamke asiye na yeyote wa kumtegemea kiuehumi itabidi atoke kutafuta mahitaji ya maisha. Au wakati mwingine mwanamke analazimika kutoka kufanya kazi iii kuongeza kipato ehamumewe kutokana na umaskini, ugonjwa au jambo lingine lolote linalomzuia kukidhi mahitaji ya familia. Kwa hali hii Uislam umetoa ruhusa ya mwanamke kufanya kazi nje ya nyumba yake Mtume (s.a.w) amesema:
Allah amewaruhusu(wanawake) kutoka nje ya majumba yenu kwa haja maalum (Bukhari).



Kumbakisha mwanamke nyumbani kwake si kumnyima uhuru bali ni kumpa uhuru na wasaa wa kutekeleza majukumu yake vizuri zaidi iii aweze kuilea familia kwa utulivu na kwa ufanisi. Kwa upande mwingine mwanamume kupewa jukumu Ia kuiongoza familia na kukidhi mahitaji yake muhimu, siyo sababu ya kujifanya bora zaidi kuliko mkewe, bali amepewa jukumu hilo kulingana na umbile lake, vipawa na nafasi aliyonayo ambayo humruhusu kutekeleza majukumu hayo. Vile vile hapana upendeleo wowote, uliofanyika katika kumpa mwanamke na mwanamume majukumu hayo. Wote wanatakiwa washirikiane kwa upendo na huruma katika kutekeleza majukumu ya familia na jamii kwa ujumla.




                   


Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 481


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Zoezi - 4
Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE. Soma Zaidi...

(xiii)Huwa muaminifu
Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Soma Zaidi...

Zingatio:
Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote. Soma Zaidi...

Nani Muadilifu na zipi sifa za mtu muadilifu kwenye uislamu
Uadilifu ni usimamizi wa ukweli na kutoa haki kwa kila anayestahiki kulingana na ukweli. Soma Zaidi...

Faida za kuwa na Huruma Kwenye Uislamu
23. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Quran na sayansi
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

tawhid
Soma Zaidi...

Hadhi na haki za mwanamke katika uislamu
4. Soma Zaidi...

Uhakiki wa hadithi za mtume
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...