picha

Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake

30.

Ukarimu na Sifa za kuwa Mkarimu na faida zake

30. Kuwa Mkarimu



Ukarimu ni miongoni mwa tabia njema anayotakiwa ajipambe nayo Muislamu.Muislamu anatakiwa awe mwepesi wa kuwakirimu wengine kwa kuwasaidia wakati wanapokuwa katika hali ya kuhitajia msaada bila ya kutarajia malipo yoyote kutoka kwao. Sifa ya wakarimu inabainishwa katika aya zifuatazo:



Na huwalisha chakula maskini na mayatima na wafungwa, na hali yakuwa wenyewe wanakipenda (chakula hicho). (Husema wenyewe katika nyoyo zao wanapowapa chakula hicho): “Tunakulisheni kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala shukurani”. (76:8-9)
Pia kumfanyia mgeni takrima ni jambo lililowajibishwa kwa Waislamu, kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema, “Yule anayemuamini Allah(s.w) na siku ya mw isho hatamdhuru jirani yake, na yule anayemuamini Allah(s.w) na siku ya mwisho atamkirimu mgeni wake na yule anayemuamini Allah na siku ya mwisho ataongea mazuri au atakaa kimya ”. (Bukhari na Muslim).



Abu Shuraikh Ka ’ab (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema, “Yeyote anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho hanabudi kumkirimu mgeni wake, na jukumu lake (la kumhangaikia sana) ni mchana mmoja na usiku.Ukarimu (kwa mgeni) ni siku tatu na zaidi ya hapo ni sadaqa. Si vyema kw a mgeni kuendelea kubakia baada ya siku tatu na kuendelea kumuweka mwenyeji wake katika hali ya uzito.” (Bukhari na Muslim).
Kiigizo chetu cha ukarimu ni Mitume wa Allah. Tunafahamishwa katika Qur-an juu ya ukarimu wa Nabii Ibrahim:


Je! Imekujia hadithi ya wageni wahishimiwao wa (Nabii) Ibrahimu? Walipoingia kw ake w akasema: “Salaam (alaykum)”. Na (yeye Ibrahimu) akasema: (“Alaykumus) Salaam” (Na katika moyo wake anasema): “Ninyi watu nisiokujueni”. Mara akaenda kwa ahali yake na akaleta ndama aliyenona. Akampeleka karibu yao. (Walipokuwa hawajanyosha mikono kula) alisema: “Mbona hamuli!” (51:24-2 7)


Katika hadithi, amesimulia Ibn Abbas (r.a) kuwa: Mtume (s.a.w) alikuwa mkarimu sana kuliko watu wote na alikuwa akizidisha ukarimu katika mwezi wa Ramadhan...” (Bukhari).
Malipo ya kuwakirimu watu ni kupata takrima ya Allah (s.w) huko Peponi kama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:


“Basi Mw enyezi Mungu ataw alinda (waka rim u) na shari ya siku hiyo na kuwakutanisha na neema na furaha.(76:11)



Na atawajaza mabustani (ya Peponi) na maguo ya hariri, kwa sababu ya kusubiri (kwao). Humo wataegemea viti vya enzi, hawataona humo jua (kali) wala baridi (kali).(76:12-13)


Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yake yataning’inia mpaka chini. Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae.(76:14-15)



Vigae vya fedha; wamevijaza kwa vipimo. Na humo watanyweshwa kinywaji kilichochanganyika na tangawizi. Huo ni mto ulio humo (Pep oni) unaitwa Salsabili. Na watawazungukia (kuwatumikia),wavulana w asiochakaa, ukiw aona utawafikiri ni lulu zilizotaw anyw a. (76: 16-19)


Na utakapoyaona (yaliyoko) huko utaona neema(zisizo kuwa na mfano) na ufalme mkubwa. Juu yao wana nguo za hariri laini, za kijani kibichi na za hariri nzito. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao ataw anyw esha kinyw aji safi kabisa (76:20-21)


“Hakika haya ni malipo yenu; na amali zenu zimekubaliwa ”. (76:22)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 1595

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

quran na sayansi

2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.

Soma Zaidi...
Zoezi la 5

Maswali mbalimbali kuhusu fiqih

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
HUYU NDIYE MUUMINI WA KWELI KATIKA UISLAMU

عَنْ أَبِي حَمْزَةَ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ خَادِمِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه ?...

Soma Zaidi...
Nani Muadilifu na zipi sifa za mtu muadilifu kwenye uislamu

Uadilifu ni usimamizi wa ukweli na kutoa haki kwa kila anayestahiki kulingana na ukweli.

Soma Zaidi...