Hapa utajifunza nguzo kuu za swaumu. Kama hazitatimia nguzo hizi basi swaumu itakuwa ni batili.
Nguzo za Funga
Nguzo za funga ni mbili: Kutia Nia na kujizuilia na kila chenye kufunguza tangu mwanzo wa alfajiri mpaka kuingia magharibi.Nia ni dhamira anayokuwa nayo mtu moyoni mwake kuwa atafunga. Nia ya funga ya faradhi inatakiwa iletwe kabla ya Alfajir, kwa mnasaba wa Hadith ifu atayo:
Bibi Hafsah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: ambaye hakunuia kufunga kabla ya alfajir, hana funga. (Tirmidh, Abu Daud, Nis a i).
Ama nia ya funga za sunnah, inaweza kuletwa mchana iwapo mtu hajala chochote tangu alfajir kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Aisha, Mama w a Waumini (r.a) ameeleza: Mtume (s.a.w) alikuja kwangu siku moja akaniuliza: Una chochote (cha kula)? Nilijibu: Hakuna. Kisha akasema: “Basi nitafunga.” Siku nyingine alikuja tena kwetu tukamuambia: Mtume wa Allah, tumeletewa zawadi ya Hais (aina ya chakula cha mchanganyiko wa Tende na Siagi). Kisha akasema: “Nionyeshe, nilifunga tangu asubuhi. Kisha alikula chakula kile.” (Muslim).
Katika Hadith hii tunajifunza mambo mawili. Kwanza tunajifunza kuwa mtu anaweza kunuia funga ya sunnah mchana kabla ya adhuhuri, iwapo atakuwa hajala chochote tangu alfajiri.
Pili, tunajifunza vile vile kutokana na Hadith hii kuwa mtu anaruhusiwa kuvunja funga ya sunnah pasi na sababu ya kisharia.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza aina za biashara ambazo ni haramu.
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kuona jinsi ya kuzitathmini swala zetu.
Soma Zaidi...Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake.
Soma Zaidi...