picha

Mambo yanayobatilisha funga au yanayoharibu swaumu.

Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika.

Yanayobatilisha Funga

Mtu aliyefunga analazimika kujizuilia na vitendo mbalimbali ambavyo hubatilisha funga yake. Mfungaji akifanya moja wapo katika yafuatayo swaum yake itabatilika.

 

(i)Kula na Kunywa
Ukila au ukinywa chochote kile kwa kudhamiria hata ikiwa ni dawa utakuwa umefungulia. Vile vile ukivuta sigara au chochote kile au ukivuta dawa ya mafua kwa pua utakuwa umefungua. Pia kupitisha chochote puani au masikioni kwa kudhamiria, hata ikiwa dawa utakuwa umefu n gu a.

 


Ikumbukwe kuwa kujifunguza makusudi katika mwezi wa Ramadhani kwa kula na kunywa bila ya udhuru wowote wa kisharia ni kosa kubwa sana mbele ya Allah(s.w) kwa kiasi ambacho hata kama mtu atafunga umri wake wote hataweza kuilipia hiyo siku moja aliyojifunguza makusudi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

 


Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Yule anayefungua siku moja ya Ramadhani bila kuwa mgonjwa au kuwa na udhuru mwingine wa kisheria, hata akifunga maisha yake yote hataweza kuilipia funga hiyo. (Ahmad, Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah, Darimi).

 


Hadith hii inatuasa tusifanyie mas-khara amri za Allah (s.w). Hivyo mtu akijifunguza makusudi ajue wazi kuwa amefanya kosa kubwa ambalo halitasameheka kwa kuilipia tu siku hiyo bali ni lazima pia arejee kwa Mola wake kwa toba ya kweli.

 


(ii)Kujitapisha Makusudi
Mtu akijitapisha makusudi funga yake itavunjika kutokana na Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Anayeshindwa kuzuia matapishi halipi. Lakini anayejitapisha makusudi, na alipe. (Tirmidh, Abu Daud, Ib Majah).
Kutokana na Hadith hii kutapika kwa ugonjwa hakufunguzi.

 


(iii)Kupatwa na Hedhi au Nifasi
Mwanamke akipatwa na hedhi au nifasi hata kama imempata nyakati za mwisho kabla ya jua kuchwa, atakuwa amefungua na atalazimika kuilipia siku hiyo baada ya Ramadhani.

 


(iv)Kujitoa Manii Makusudi Ukijitoa manii kwa mkono au kwa kubusiana na kukumbatiana mume na mke, au kwa njia nyingine yoyote ile utakuwa umefungua.Kutokwa na manii kwa kuota au kwa njia nyingine isiyokuwa ya makusudi, hakufunguzi.

 


(v) Kunuia Kula na hali umefunga
Ukinuia kula hata kama hukula swaumu yako itakuwa imebatilika kwa kuwa utakuwa umevunja nguzo moja ya funga - nia.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 3236

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     ๐Ÿ‘‰3 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰4 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰5 web hosting     ๐Ÿ‘‰6 ai web app    

Post zinazofanana:

Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali

Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir

Soma Zaidi...
Jinsi ambavyo msafiri anatakiwa aswali akiwa safarini

Postvhiibinakwenda kukufundisha kuhusu swala ya msafiri na jinsi ya kuiswali.

Soma Zaidi...
Maana ya swala

Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno ยSwalaatย lina maana ya ยombi au ยdua.

Soma Zaidi...
Ni ipi hukumu ya kutoa talaka hali ya kuwa umelazimishwa au ukiwa umerukwa na akili

Endapo mtu atamuacha mke pasi na ridhaa yake yaani amelazimishwa ama amemuwacha wakati amerukwa na akili. Je ni ipo hukumu yake.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya swala

Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike?

Soma Zaidi...
Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani

(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu.

Soma Zaidi...