Navigation Menu



image

Fadhila za usiku waalylat al qadir

Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000.

Umuhimu wa usiku wa Lailatul Qadr

Umuhimu wa Usiku wa Lailatul Qadr umebainishwa wazi katika Qur-an kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:

 

Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima. Ndiyo hukumu itokayo kwetu; kwa hakika sisi ni w aletao (Mitume ili w awaongoe watu). (44:4-5).
Katika Suratul-Qadr tunasoma

 

“Hakika tumeiteremsha (Qur-an) katika Lailatul-Qadr (Usiku wenye heshima kubwa). Na ni jambo gani litakalo kujulisha ni nini huo usiku wa Lailatul-Qadr? Huo usiku (wa Lailatul-Qadr) ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na Roho (Jibril) katika usiku huo kwa idhini ya Mola w ao kw a kila jambo. Ni amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajir. ” (9 7:1 -5).

 


Tunajifunza katika aya hizi kuwa Allah (s.w) ameutukuza Usiku mmoja katika mwezi wa Ramadhani ili iwe kumbukumbu kwa Waumini wa umati huu wa Mtume Muhammad (s.a.w), ya kuletewa mwongozo pekee wa maisha yao kutoka kwa Mola wao. Mwongozo ambao huwa ni ponyo na rehma kwa Waumini na ambao hauwazidishii makafiri ila khasara:

 

 

 

Na tumeteremsha katika Qur-an (hayo mafundisho yake) ambayo ni ponyo (poza la nyoyo) na rehema kwa wanaoamini. Wala hayawazidishii (mafundisho haya) madhalimu ila khasara ” (1 7:82).

 


Tunafahamishwa katika aya zilizomo katika Surat Qadr kuwa Allah (s.w) ameutukuza usiku huu zaidi ya miezi elfu moja au miaka 83 na miezi 4. Ina maana kuwa muumini akifanya amali njema katika usiku huu, thamani yake katika malipo na katika uwezo wa kumfikisha mja kwenye lengo la maisha yake itakuwa ni kubwa zaidi ya thamani ya amali hiyo iliyofanywa kwa miezi elfu moja. Umuhimu wa lailatul-Qadr pia unabainika katika Hadith ifuatayo:

 


Ames imulia Abu Hurairah (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani akiwa na Imani na akiwa na tegemeo la kupata malipo kutoka kwa Allah (s.w), basi dhambi zake zote zilizopita zitasamehewa. Na mwenye kusimama kwa swala katika usiku wa Qadr akiwa na imani na mategemeo ya kupata malipo kutoka kwa Allah, basi dhambi zake zote zilizotangulia zitasamehewa.” (Bukhari).

 


Ili kupata malipo na baraka ya usiku huu wa Lailatul-Qadr, Mtume (s.a.w) ametuhimiza sana kuupania huo usiku kwa kuzidisha ibada za usiku kwa kuswali, kusoma Qur-an, kumkumbuka Allah (s.w) kwa wingi na kuomba maghfira.

 


Aysha (r.a) ameeleza: Niliuliza: “Ewe Mtume wa Allah! Nifahamishe niseme nini nitakapoudiriki usiku uliobarikiwa ?” Akasema (Mtume s.a.w) sema; “Ee, Allah! Wewe ni Msamehevu Unayependa kusamehe, Basi (Nakuomba) Unisamehe”. (Ahmad, Ibn Majah, Tirmidh).

 


Usiku wa Lailatul-Qadr ni usiku uliofichwa na Allah (s.w). Yaani haijulikani siku maalum ya mwezi wa Ramadhani ambamo usiku huu hutokea. Kwa jitihada zetu tunaona hekima ya kufichwa usiku huu ni ili Waislamu wasiwe wavivu wa kufanya ibada katika mausiku yote ya mwezi wa Ramadhani na badala yake wakautegea usiku huo mmoja tu. Hata hivyo, kutokana na Hadith sahihi tunajifunza kuwa usiku huu hutegemewa zaidi kutokea katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani. Mtume (s.a.w) aliutafuta usiku huo katika kumi la mwisho kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:

 

Abu Sayed al-Khudr(r.a) am eeleza kuw a Mtum e (s.a.w) alikaa itiqaf katika siku kumi za kwanza za Ramadhani. Kisha akakaa tena itiqaf katika kumi la katikati la Ramadhani. Kisha aliinua kichwa chake akasema: “Hakika nilikaa Itiqaf katika siku kumi za mwanzo, niliutafuta usiku huu (wa Qadr). Kisha nilijiwa na kufahamishwa kuwa usiku huu hupatikana katika siku kumi za mw isho. Yule atakayekaa Itiqaf na mimi, basi na akae katika kumi la mwisho, kwa sababu nilionyeshwa kutokea kwake katika siku hizo lakini nilifanywa kusahau (siku gani hasa), japo niliuona mimi mwenyewe nikiwa (kwenye ndoto) nikiwa ninasujudu kwenye maji na matope. Basi utafuteni usiku huu katika siku kumi za mwisho na hasa mausiku ya witr ...” (Bukhari na Muslim).

 


Hadith hii inatufahamisha kuwa mtume (s.a.w) alibainishiwa u siku huo kuwa katika kumi la mwisho la Ramadhani na akakokoteza watu wakae Itiqaf katika kumi hilo.Pia kutokana na Hadith hii mausiku yenye mategemeo zaidi katika hili kumi la mwisho ni zile za witr - usiku wa 21, 23, 25, 27, na 29. Katika Hadith iliyosimuliwa na Zirri bin Hubaish (r.a) na kupokelewa na Muslim, usiku wa 27 umetiliwa mkazo zaidi. Lakini hasa alichosisitiza Mtume (s.a.w) sio kutegemea usiku mmoja tu kama vile usiku wa 27, bali kujizatiti kwa kuzidisha ibada za usiku kwa kuswali, kusoma Qur-an, kumkumbuka Allah kwa wingi, kuomba maghfira na dua mbali mbali kwa mausiku yote ya kumi la mwisho la Ramadhani.Hivi ndivyo alivyofanya Mtume (s.a.w) kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:

 


Aysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akijizatiti sana kufanya ibada katika mausiku ya kumi ya mwisho, kuliko ilivyokuwa kawaida yake katika wakati mwingine. (Muslim).

 


Aysha (r.a) ameeleza kuwa wakati usiku wa kumi la mwisho ulipoingia, Mtume (s.a.w) alikuwa akijifunga kibwebwe akikesha katika Ibada na akiamsha familia yake kwa swala. (Bukhari na Muslim).

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1196


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Saumu (funga)
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Je manii ni twahara au najisi?
Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis Soma Zaidi...

Hukumu na taratibu za ndoa katika uislamu
Soma Zaidi...

Jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi. Soma Zaidi...

Mifumo ya benki na kazi zake
Hapa utajifunza kazi za benki. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)
Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume Soma Zaidi...

Jinsi ya kufanya suluhu kati ya mume na mke.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kufanya suluhu katika ndoa. Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za Mwanamke katika jamii mbalimbali hapo zamani
Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii. Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

haki na wajibu katika jamii
Soma Zaidi...

Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir Soma Zaidi...

Haya ndio yanayobatilisha Hija
Soma Zaidi...