Posti hii inahusu zaidi nguzo kuu za umama katika umri wa kujifungua na kulea watoto, ni kipindi ambacho mama anakuwa analea watoto kwa kawaida kadri ya makadirio kipindi hiki uanza kati ya miaka kumi na mitano mpaka arobaini kwa walio wengi na kinaweza k
Nguzo za kuu za umama katika kipindi cha kujifungua na kulea watoto.
1.Mama akiwa katika kipindi cha kujifungua na kulea watoto katika kipindi hiki anapaswa kuwa na nguzo kuu muhimu zinazopaswa kumwongoza ili aweze kupata watoto wenye afya nzuri na makuzi mema pasipokuwa na magonjwa na vizuizi vyovyote wakati wa makuzi ya mtoto mpaka mtoto anafikia umri wa miaka mitano na kuzidi kwa hiyo zifuatazo ni nguzo kuu za umama.
2.Uzazi wa mpango.
Wazazi wote wawili wanapaswa kutumia uzazi wa mpango ambao wanaona unafaa kwao baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya, kwa kutumia uzazi wa mpango wazazi wanaweza kupata idadi ya watoto ambao wanawahitaji na watoto wanaweza kupata malezi muhimu na mapenzi kutoka kwa wazazi wao, kwa kutumia uzazi wa mpango uepusha kubwa na watoto wanaofuatana sana na kusababisha ukuaji wa watoto kubwa wa shida na kusababisha umaskini ambapo mama baada ya kufanya shughuli mbalimbali za kuongeza uchumi anatumia mda mwingi kulea watoto.
3.Kuhudhulia kliniki wakati wote wa ujauzito na baada ya kujifungua pale anampeleka mtoto.
Mama akibeba mimba tu anapaswa kwenda kliniki ili kuweza kuona maendeleo ya mimba na kupata elimu mbalimbali hasa kuhusu Dalili za hatari wakati wa ujauzito pia mama anapaswa kupima maambukizi ili aweze kumkinga mtoto na Maambukizi yoyote yale, kwa hiyo hata mama akijifungua anapaswa kupeleka mtoto wake kliniki ili apate chanjo mbalimbali za kumkinga na magonjwa kama vile kifua kikuu, kupooza na magonjwa mbalimbali, kwa hiyo akina Mama mnapaswa kuhudhuria kliniki kwa sababu kuna faida nyingi kwa Mama na mtoto pia.
4. Kuzuia maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito.
Mama akiwa na mimba anapaswa kupima maambukizi yote kwa awamu mbili ya kwanza ni pale anapobeba mimba tu na wakati akiwa na miezi minane ya ujauzito hii ni kwa sababu ya kuepuka kumwambukiza mtoto akiwa kwenye tumbo la Mama, na wakati wa kujifungua kwa kumpatia mama dawa za kupunguza makali ya virus vya ukimwi na mtoto akizaliwa na Mama mwenye Maambukizi anapaswa kupewa dawa pindi anapozaliwa hata kama yeye hana Maambukizi kwa hiyo huwa kwenye uangalizi kwa kipindi cha miezi sita.
5.Uangalizi wa Mama na mtoto ndani ya masaa ishirini na manne.
Mama anapojifungua salamu huwa kwenye uangalizi ndani ya masaa ishirini na manne ili kuangalia kama kuna mabadiliko yoyote yanayoweza kujitokeza kwa mtoto na Mama pia kwa hiyo kama hakuna mabadiliko yoyote mama anaruhusiwa kutoka hospitalini na kama kuna mabadiliko yoyote Mama na mtoto watapaswa kutibiwa kufuatana na hali zao.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi sababu za kondo la nyuma kuwa mbele ya mlango wa kizazi, kwa kawaida kondo la nyuma huwa nyuma ya mlango wa kizazi ila Kuna wakati kondo la nyuma ujishikisha mbele ya mlango wa kizazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo zinaweza kujitokeza na zikaonesha kwamba mbegu za kiume ni dhaifu au ni chache.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuhusu kwa mimba kutoka kabla ya mda wake,ni kitendo ambacho mimba utoka kabla ya wiki ishilini na na nane.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango, Ni watu ambao Wana matatizo mbalimbali endapo wakitumia wanaoweza kuleta madhara mbalimbali.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukuletea orodha ya vyakla vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume.
Soma Zaidi...Tunaposema uzazi wa mpango, tunamaanisha ile hali ya kuachanisha muda kutoka mtoto hadi mwingine. Inatakiwa angalau mtoto na mtoto wapishane miaka miwili. Uzazi wa mpango ni maamuzi kati ya mama na baba.
Soma Zaidi...Unaweza kujiuliza ikiwa inawezekana kupata dalili za ujauzito mchanga kama siku 7 baada ya kudondoshwa kwa yai (DPO yaani Days Past Ovulation).
Soma Zaidi...inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto.
Soma Zaidi...