Somo hili linakwenda kukuletea njia za asili walizotumia zamani katika kupima ujauzito
NJIA ZA KIASILI WALIZOTUMIA ZAMANI KUPIMA UJAUZITO:
1.Kukojoa kwenye nafaka (mbegu za ngano na shayiri)Tafiti zilizofnywa na wavumbuzi wa mabo ya kale (archeologist) wamegunduwa kuwa yapata miaka 1350 KK kabla ya kuzaliwa Yesu kuwa wanawake wa Misri (Egypt) walikuwa wanapotaka kujuwa kama wamebeba ujauzito walikuwa wakichukuwa viroba vya ngano na shayiri (barley) kisha wanakojolea kiroba chote. Kama ngano itaota basi mwanamke ana ujauziti tena wa mtoto wa kike. Na kama shayiri itaota atakuwa na ujauzito wa mtoto wa kiume. Na kama nafaka hizi hazitaota basi mwanamke hana ujauzito.
Ni kuwa katika mwanamke mjamzito kwenye mojo wake kuna homoni ambazo zinachochea ukuwaji wa mbegu. Baada ya kukojolea pishori lile mbegu hazifukiwi, hivyo ztaota mulemule kwenye kiroba kile bila ya kufukiwa kwenye udogo. Miaka ya 1960 wanasayanzi wa leo walifanya tafiti wakagunduwa kuwa njia hii ni sahihi ya asilimoa 70%.
2.Kitunguu.Njia hii ilifanywa na wagiriki mikaa ya zamani sana. Matabibu wa kigiriki walikuwa wanapotaka kujuwa kama mwanmke ana ujauzito walikuwa wakiinguiza kwenye uke wa mwanamke kitunguu na kukiacha humo kwa usiku mzima. Na kama ikifika asubuhi mwanamke akawa anatowa harufu ya kitunguu kwenye mdomo wake basi ana ujauzito. Wagiriki waliamini kuwa mwanamke akiwa na ujauzito uke wake unauwezo mkubwa wa kufyonza vitu. Tafiti hii haikuweza kuthibitishwa na sayansi hili leo.
3.Kwa kutumia funguo ama kitasa.Njia hii ilifanya kwa namna hii, endapo mwanamke anajihisi ni mjamzito alikuwa anachukuwa fnguo ama kitasa kisha anaweka kwenye bakuli kisha anakojowa kiasi cha mkojo kuzamisha funguo ama kitasa kisha anaacha hivyo kwa muda wa masaa matatu. Kama akitowa hakuna mabadiliko ya michubuko ama rangi ana chochote basi mwanamke ni mjamzito. Njia hii [ia haikuweza kuthibitishwa hivi leo.
4.Kwa kuangalia rangi ya macho.Moja katika matabibu wa zamani sana wa kifaransa aliyetambulika kama Jacques Guillemeau yeye aliamini kuwa macho ndio kioo cha mwili, hivyo unaweza kujuwa maradhi na hali ya mwili wa kutumia macho. Aliamini kuwa mwanamke mjamzito macho yake yameingia ndani kidogo, mboni ya macho yake imesinyaa kidogo na mishipa ya neva ilajitokeza pembezoni mwa macho. Wanasayansi wa leo pia wameshindwa kuthibitisha usahihi wa njia hii, ijapokuwa ni kweli mabadiliko yanaweza kutokea kwenye macho ila si kwa kipindi cha mwanzo.
5.Njia uliyojulikana kama Piss ProphetsNjia hii ilitumiaka miaka ya 1600, matabibu hawa walikuwa wakipima ujauzito kwa kutumia kuangalia mkojo. Hawa waliamini kuwa mkojo wa mjamzito unakuwa ni msafi naani hauna uchafu, una rangi ya limao bivu lililopauka lakini unakuwa na ukungu kwa mbali juu yake. Pia matabibu hawa hawakuishia hapa walikuwa wakiangalia uwepo wa maradhi engine kwa kuangalia mkojo. Wanasayansi wa leo pia wameshindwa kuthibitisha usahihi wa njia hii.
6.Kwa kutumia riboni:Njia hii ilikuwa na mzunguruko kidogo, nikuwa mwanamke anapojihisi ni mjamzito anakwenda kwa tabibu. Tabibu atamwambia akojoe kwenye beseni, kisha tabibu atachukuwa riboni na kuitia kwenye beseni lenye mkojo. Baada ya muda ataitoa na kuikausha, kisha ataichoma mbele karibu na mwanamke. Kama harufu ya riboni itamfanya mwanamke ahisi kichefuchefu basi atakuwa ana ujauzito. Wanasayansi waleo pia hawakuweza kuthibitisha njia hii.
7.Kwa kutimia Sungura ama wanyama wadogo wadogo kama panya.Njia hii iligunduliwa miaka ya 1900 na matabibu waliojulikana kwa majina ya Bernhard Zondek na Selmar Aschheim. Hawa miaka ya 1940 waliamini kuwa mkojo wa mjamzito ukiingizwa kwenye mwili wa vijinyama vidogo basi ovari zao huwa kubwa. Baadaye jaribio hili lilijikita sana kwa kutumia sungura. Wanasayansi wa leo walionyesha kuwa njia hii ilikuwa na ukweli kiasi japo sio njia nzuri maana ilihitajika kumuuwa sungura ili kuchunguza kama ovari zimekuwa kubwa.
8.Kwa kutumia chura.Njia hii ilianza kutumika Afrika ya Kusini. Wao walikuwa wakutumia chura wa kike. Waliamini kuwa endapo chura wa kieke akichomwa sindano yenye mkojo wa mwanamke mjamzito, basi chura huyo atataga mayai ndani ya masaa 12.
Njia nyingine:9.Kuangalia mwendo, yaani jinsi anavyotembea mjamzito ni tofauti na mwanamke asiye mjamzito.10.Kwa kuaangalia ongezeko la mapigo ya moyo. Kama mapigo ya moyo yameongezeka basi mwanamke ana ujauzito.
Njia zilizotajwa hapo juu zilikuwa zukitumika katika nyakati zake na zilionekana kusaidia kwa wakati ule. Ni kweli njia hizo zina madhaifu makubwa lakini si kila wakati zilikuwa zikikosea. Wakati mwingine zilikuwa zikipatia, ni kwa sababu mwanamke alikuwa ni mjamzito kweli. Hata hivyo ilibidi pia kuangalia dalili nyingine za ujauziti ndipo tabubu alikuwa akitoa jibu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka.
Soma Zaidi...Je na wewe unasumbuliwa na fangasi wenye uume. Post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito, ni mojawapo ya njia ambazo utumiwa na wahudumu wa afya ili kuweza kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito.
Soma Zaidi...Miongoni mwa dalili zamwanzo za ujauzito ni maumivu ya tumbo ama kupatwa na damu kidogo. Mabadiliko ya ute ute sehemu za siri ni katika baadhi ya dalili. Endelea na makala hii utajifunza zaidi.
Soma Zaidi...Nimesoma makala yenu, sasa nina swaliJe kitunguu saumu kina madhara kwa Mgonjwa wa figo?
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia Faida za Uzazi wa mpango kwa watoto, mama, wanandoa, na jamii au JUMUIYA.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Kama na wewe una tatizo la kupitiliza siku zako za hedhi hli ya kuwa huna ujauzito, soma post hii ina majibu yako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuhusu njia za uzazi wa mpango, uzazi wa mpango ni njia za kupanga uzazi Ili kupata idadi ya watoto unaohitaji
Soma Zaidi...