Posti hii inahusu zaidi sifa ambazo mtoto mchanga anapaswa kuwa Nazo,ni sifa ambazo lazima zionekane kwa mtoto mchanga pale anapozaliwa na zikikosa ni lazima kuja kuwa mtoto ana matatizo mbalimbali kwa hiyo zifuatazo ni sifa za mtoto mchanga kama ifuatavy
1. Mwonekano mzima wa mtoto.
Kwanza kabisa mtoto anapaswa kuwa na uzito kuanzia mbili na nukta tano mpaka tatu na nukta tano na kwa kawaida urefu wa mtoto ni kuanzia hamsini sentimita, na rangi ya mtoto anapozaliwa ni rangi ya pinkie, kwa hiyo mtoto akiwa na uzito chini ya mbili na nukta tano anakuwa kwenye uangalizi kwa mda na pia akiwa na uzito kuanzia tatu na nukta tano na kuendelea tunasema kwamba ni mtoto aliyezidi kwa uzito kwa hiyo naye huwa kwenye uangalizi maalumu kwa mda na baadae anaweza kuruhusiwa na kuwa kwenye uangalizi wa wazazi.
2.Watoto waliochini ya uzito au juu ya uzito uwa kwenye uangalizi kwa sababu, zifuatazo.
Mwenye uzito mkubwa anaweza kuwa amezoea vyakula vya kutosha kutoka kwa Mama yake akiwa tumboni akizaliwa tu anapaswa kuhudumiwa mapema na kupewa glucose Ili kulinganisha na chakula alichokuwa anakipata akiwa tumboni kwa hiyo akicheleweshwa anaweza kushuka kwa sukari. Na pia mtoto akizaliwa na uzito mdogo anapaswa kuangaliwa kwa sababu ya kupata uzito unaotakiwa kwa kihakikisha kuwa Mama yake anapewa elimu ya kumtunza mtoto mpaka akafikia kuwa na uzito unaotakiwa.
3. Pia mtoto akizaliwa anapaswa kuwa na kitovu kilicho kwenye tumbo na kinatakiwa kukatwa kwa uangalizi unaofaa Ili kuweza kuzuia maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto, pia na Mama anapaswa kupewa elimu kuhusu namna ya kumtunza kitovu cha mtoto wafundishwe kuwa kitovu cha mtoto kinakauka baada ya siku kumi, pia akina Mama wanapaswa kukumbushwa kuwa waachane na tabia ya kuweka vitu visivyofaa kwenye kitovu kwa kufuata mila na desturi zao hali inayosababisha kuwepo kwa tetunus kwenye kitovu kikitunzwa visivyo.
4. Pia kitu kingine ambacho ni sifa ya mtoto ni kulia tu baada ya kuzaliwa hii ikiwa ni ishara ya uhai kwa mtoto,kwa hiyo mtoto asipolia wauguzi na wasaidizi wote wanapaswa kihakikisha mtoto analia kwa kutoa huduma ya kwanza kwa mtoto na walio wengi wanafanyiwa na wanapona na kuendelea kwenye hali ya kawaida
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Watu wengi wanadhania kuwa kufanya tendo la ndoa katika siku hatari ni lazima kuwa utapata ujauzito. Hili sio sahihi kabisa. Post hii itakwenda kuangalia jambo hili zaidi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi homoni ya androgen, ni homoni ambayo imo kwa wanaume na ikizidi kwa kiwango chake inaweza kuleta shida kwenye mwili wa binadamu kwa hiyo homoni hii inaweza kuleta shida iwapo ikiongezeka kwa kiasi kikubwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kama mtoto alizaliwa na uzito mkubwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye via vya uzazi kwa wajawazito, tunajua kuwa Mama akibeba mimba tu kuna mabadiliko utokea katika sehemu mbalimbali za mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uzazi wa mpango kwa njia ya kumwaga shahawa nje, hii ni njia mojawapo kati ya njia za uzazi wa mpango ambapo mwanaume humwaga nje mbegu ili asimpatie Mama mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba, ni Imani ambazo zimekuwepo kwenye jamii kuhusu wanawake wenye mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Soma Zaidi...Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, ni faida wanazozipata waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi.
Soma Zaidi...