Posti huu inahusu zaidi malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama, ni huduma muhimu ambazo zimetolewa kwa akina Mama ili kuweza kuepuka hatari mbalimbali zinazowakumba akina Mama wakati wa ujauzito, kujifu na malezi ya watoto chini ya miaka mitano.
Malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama.
1.Kuangali Magonjwa yanayoweza kutokea kwa wajawazito na kuwapatia dawa mapema ili wasiweze kuwaambukiza watoto.hili ni lengo mojawapo kuhakikisha kubwa kama kuna dalili yoyote ya ugonjwa ambao unaweza kujitokeza na kuwa tayari kuwapatia dawa ili kutibu na kuepuka kuwaambukiza watoto wakati wa ujauzito, mfano wa magonjwa ni kaswende na HIV kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto na kwa asilimia tisini hili limeweza kufanikiwa katika jamii zilizo nyingi.
2.Kuhakikisha kwamba maendeleo ya mtoto na Mama yako vizuri. Kwa kuhakikisha kuwa Mama anakuwa na damu ya kutosha mwilini kwa kupima wingi wa damu, kumpatia Mama dawa za minyoo na kupima kama kuna Malaria na kumpatia Mama vidonge vya sp kwa kila udhulio na kumpatia Mama neti mara tu anapoanza kliniki kwa kufanya hivyo Mama anaweza kuwa na afya nzuri pamoja na mtoto wake.
3. Kuhakikisha kuwa Mama anajua Maana ya uzazi wa mpango ili aweze kupata watoto anaowahitaji na kuwa na distansi fulani kama ni kuzidiana miaka minne au mitano kuu kadri ya maamuzi ya wazazi wenyewe kwa kufanya hivyo watoto wanaozaliwa wanapata upendo kutoka kwa wazazi wao na pia Mama anapata nafasi ya kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi kwa kupata mda wa kutosha badala ya kubaki katika kulea watoto wanaofuatana bila mpangilio.
4.Lengo lingine ni kuhakikisha kuwa Dalili za hatari wakati wa ujauzito zinapungua kwa kuwapatia akina mama elimu kabla ya kuanza mahudhurio ili mama akiona dalili mojawapo ambayo ni ya hatari aweze kuja hospitali mara moja ili kuepuka madhara kwa mtoto, Dalili hizo ni pamoja na mtoto kushindwa kucheza, kugongwa na kichwa, kizungu Zungu, kutoka damu ukeni, kuhisi maumivu makali ya tumbo, homa kali na mabadiliko mengine ambayo siyo ya kawaida kwa Mwanamke mjamzito.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Makala hii itakwenda kukufundisha baadhi ya dalili za uchungu kwa mama mjamzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mathara yanayosababisha Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukuletea mambo kadhaa yanayohusiana na malezi bora ya mama mjamzito na mtoto mchanga
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukufundisha dalili za kujifunguwa, hatuwa za kujifunguwa na kuzalisha, pia utajifunza mabo muhimu kabla na wakatii wa kujifungua.
Soma Zaidi... Posti hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa ovari kunakosababishwa na maambukizo ya bakteria na kawaida huweza kusababishwa na magonjwa sugu katika Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha kwa sababu kuna familia nyingi zinakosa watoto sio kwa sababu ni tasa ila kuna njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...