Post hii inahusu zaidi sababu za mimba kutoka, hili ni tatizo ambalo linawakumba wanawake wengi ambapo mimba utoka kabla ya kumfikisha mda wake, kwa kawaida Ili kawaida mimba nyingi utoka zikiwa na miezi chini ya Saba au wengine wanaweza kusema kwamba mim
Sababu za mimba kutoka.
1. Sababu ya kwanza ni kuwepo kwa maambukizi hasa kwa akina Mama.
Maambukizi kama vile kaswende kisonono na mengine kama hayo usababisha mimba kutoka hasa pale yanaposhambuliwa sehemu ya kondo la nyuma na kusababisha kulegea na hatimaye mimba kutoka.
2. Kuwepo kwa homa inayozidi kipimo au homa kuwa juu sana, kwa kawaida kiwango cha homa kwa mwanamke kinapaswa kuwa kawaida ila kikizidi kiasi usababisha kuwepo kwa kuharibu sehemu mbalimbali hasa kwa mtoto hatimaye kusababisha mimba kutoka, kwa hiyo akina Mama wanapaswa kufahamu kwamba homa yoyote isiyo ya kawaida wakati wa ujauzito ni hatari kwa makuzi ya mtoto tumboni.
3. Mishutuko mbalimbali.
Mishutuko mbalimbali inayoweza kuwa ya moja kwa Moja au isiyokuwa ya Moja kwa Moja usababisha mimba kutoka, kwa mfano mama kupigwa sehemu za tumbo usababisha mishutuko kwenye sehemu zilizoshikilia mtoto na kusababisha mimba kutoka au kwa wakati mwingine mishutuko inayosababishwa na msongo wa mawazo pamoja na mambo ya kusikitisha yanaweza kusababisha mimba kutoka. Kwa hiyo jamii inapaswa kumtunza Mama na kuhakikisha anapata mazingira mazuri Ili kuweza kuruhusu mimba kukua vizuri.
4. Magonjwa mbalimbali nayo usababisha mimba kutoka.
Kuna baadhi ya magonjwa ambayo usababisha mimba kutoka hasa kama ni ya mda mrefu kwa mama mjamzito hayo ni kama kisukari cha kupanda na kushuka, shinikizo la damu na ukosefu wa baadhi ya homoni au vichocheo vinavyosababisha makuzi ya mtoto mfano kichocheo cha progesterone kikipungua ni hatari kwa makuzi ya mtoto tumboni, sio kwamba walio na magonjwa haya wote mimba utoka hapana ila wakiamua kuchukua matibabu na kufuata mashariti Wana uwezo wa kujifungua salama. Kwa hiyo kama mjamzito yeyote anajua ana tatizo hilo ni vizuri kabisa kupata ushauri kwa wataalamu wa afya na kupata matibabu Ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.
5. Baadhi ya madawa na mazingira magumu usababisha mimba kutoka.
Kuna watu ambao katika maisha yao wamezoea kutumia madawa ambayo ni hatari wakiendelea kutumia hasa wakiwa na wajawazito madawa hayo ni kama madawa ya kulevya,watumiaji wa quinine wakiwa na malaria, matumizi ya vinywaji vikali kama vile konyagi matumizi ya sigara, haya yote usababisha kutoka kwa mimba kabla ya wakati, kwa hiyo ni vizuri kabisa kama mama akubeba mimba anapaswa kuachana nayo kabisa Ili aweze kupata mtoto mwenye afya.
6. Kukosa mlo kamili wa kutosha na wenye virutubisho mbalimbali.
Kwa kawaida mama akibeba mimba damu upungua kwa hiyo anapaswa kula vyakula vya kuongeza damu Ili kuweza kupata mtoto mwenye afya na afya ya mama mwenyewe, ila Kuna akina Mama ambao wakibeba mimba hawali kabisa au wanakula chakula kidogo hali inayosababishwa kutoka kwa mimba au wakati mwingine wanakula aina Moja ya chakula na kusababisha kukosa kwa madini kwa mtoto hatimaye mimba kutoka, kwa hiyo akina Mama wanashauliwa kula mboga za majani, matunda na vyakula vya madini ya chuma.
7. Kuwepo kwa maambukizi kwenye mfuko wa kizazi.
Kuna wakati mwingine kwenye mfuko wa kizazi kunakuwepo na maambukizi, hali ambayo usababisha mimba kutoka kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi. Kwa hiyo akina Mama wanapaswa kutumia dawa mbalimbali Ili kuweza kuepuka mimba kutoka kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi.
8. Kutoa mimba mara kwa mara.
Hii ni tabia inayohusu zaidi akina dada wakiwa bado hawajahitaji watoto ila wanakuwa na wapenzi wao hali inayosababisha kubeba mimba na kutoka kwa hiyo kwenye mfumo wa uzazi ujitengenezea mazingira ya kutoa mimba kabla ya kukomaa hali inayosababisha mimba kutoka kwa sababu ya mazoea ya mara kwa mara. Kwa hiyo akina dada wanapaswa kuacha tabia ya kutoa mimba ila watumie uzazi wa mpango au wasubiri wakati.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Utajifunza dalili za mwanzoni za mimba changa kuanzia wiki moja baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kujaa tmgesi tumbon
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
Soma Zaidi...Hivi unadhani kuharisha ni katika dalili za mimba, vipi kuhusu kutopata choo pia inaweza kuwa ni ujauzito?
Soma Zaidi...Kipimo cha mimba kwa mkojo kimekuwa kikitumika sana kuangalia ujauzito. Kipimo hiki kinapotumika vibaya kinaweza kukupa majibu ya uongo. Kuwa makini na ujue muda sahihi.
Soma Zaidi...Kupata ujauzito hufungamana na mambo mengi ikiwepo afya vya wawili yaani me na mume na mengineyo. Unaweza kushiriki sikuvhatari na usiupate mimba. Postivhii ibakwendavkukufahamisha undani wa jambo hili.
Soma Zaidi...Korodani ni kiungo muhimu kwa mwanaume, katika afya ya uzazi. Unaweza kusema ni kiwanda cha kutengeneza mbegu za kiume. Kiungo hiki ni sawa na ovari kwa mwanamke.
Soma Zaidi...Je na wewe ni moja kati ya wake ambao wanahitajivkujuwa siku za kupata mimba. Ama siku za competes mwanamke mimba. Post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kazi za homoni katika Mzunguko wa hedhi, katika kipindi hiki kuna homoni mbalimbali ambazo ufanya kazi kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...