Zijuwe Dalili za minyoo na dalili kuu 9 za minyoo
Utajifunza dalili za minyoo, sababu za minyoo na namna ya kujiepusha na minyoo. Dalili kuu 5 za minyoo mwilini
Dalili za minyoo, sababu zake na kuiepuka minyoo.
Minyoo ni katika wadudu vimelea vinavyowapa shida watu wengi leo hii. Minyoo sio virusi wala bakteria kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakidhania.minyoo ipo katika makundi meengi na huishi katika maeneo mbalimbali kwenye miili yetu ikiwemo tumbo, ini, utumbo, ubongo na kwenye damu na maeneo mengine. Dalili za minyoo hutofautiana sana kulingana na aina ya minyoo na wapi ipo. Lakini zipo dalili zenye kufanana kwa minyoo wote. Katika makala hii nitakwenda kukujuza baadhi ya dalili za minyoo katika mwili wako, pia tutaona sababu za kupata minyoo, wapi minyoo inapatikana na vipi tutaizuia:-
Utaweza kupata minyoo katika hali zifuatazo:-
1.kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama
2.Kunywa maji ambayo si masafi na si salama
3.Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi
4.Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo
5.Kula udongo,
6.Kinyesi cha wanyama na binadamu

DALILI ZA MINYOO
Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-
1.Kichefuchefu
2.Kukosa hamu ya kula
3.Maumivu ya tumbo
4.Kupungua uzito
5.Uchovu wa viungo
6.Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi
7.Kuona minyoo kwenye kinyesi.
8.Kuona damu kwenye kinyesi
9.Tumbo kujaa
Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-
1.minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:
A.Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo
B.Kuwa na alegi
C.Kuwa na homa
D.Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa
2.minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-
A.Kuwashwa
B.Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini
C.Kuwa na uchovu wa hali ya juu.
3.minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-
A.Kupata homa
B.Kuvimba kwa uso
C.Maumivu ya misuli na kuchoka
D.Maumivu ya kichwa
E.Kutokupenda kupigwa na mwanga
F.Matatizo katika macho (conjuctivist)

NJIA ZA KUKABILIANA NA MINYOO
Kwa kuwa tumekwisha kuona namna ambavyo minyoo huenezwa, hivyo basi ni rahisi sasa kutaja namna ya kubambana na minyoo. Njia hizo ni kama :-
1.usile chakula, nyama ana samaki ambaye hajapikwa vyema, ama kula nyama mbichi ama isiyoiva
2.Epuka kugusagusa nyama unapoandaa chakula chako, tenganisha nyama kivyake na vyakula vingine wakati unapoandaa kupika.
3.Safisha vyema vyembo ambavyo vimegusa nyama ambayo haikupikwa
4.Usile mimea ambayo inaishi ndani ya maji yabaridi
5.Usitembee miguu wazi kwenye maeneo machafu ambayo yana kinyesi
6.Safisha vyema kinyesi cha wanyama.
7.Hakikisha unapika vizuri nyama mpaka uhakikishe imewiva vyema,
8.Wanya kungβata kucha ama kunyonya vidole
9.Hakikisha unaosha kila unachokila kwa maji yaliyo safi na salama.
10.Usafi wa mwili, mavazi na mazingira ni muhimu kwa ajili ya kupambana na minyoo.
11.Kuwacha kabisa kula udongo
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 Madrasa kiganjani π3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π4 Kitau cha Fiqh π5 Bongolite - Game zone - Play free game π6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Dalili za kupata uvimbe kwenye kizazi (fibroid)
Post hii inaenda kufundisha kuhusiana na uvimbe wa kizazi kwa wanawake. Uvimbe wa kizazi no uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao unaweza kuwa ndan ya kizazi uvimbe huu ndan ya mwanamke hujulikana kama (uterine myoma au fibroid). Uvi
Soma Zaidi...Mambo yanayopelekea Mjamzito kutokwa na damu
Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali ambayo yanapelekea Mjamzito kutokwa na damu, hizi ni baadhi ya sababu ambazo usababisha Mjamzito kutokwa na damu.
Soma Zaidi...Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Maambukizi kwenye Njia ya Uzazi kwa kifupi hujulikana Kama PID.ni Maambukizi ya mfumo wa Uzazi yanayoathiri wanawake, Maambukizi haya kwa Kawaida huhusisha sehemu Kama shingo ya uzazi,nyuma ya mfuko wa Uzazi na mirija ya uzazi.
Soma Zaidi...Fahamu kuhusu mapacha wanaofanana
Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja.
Soma Zaidi...Namna ya kumpima mtoto uzito
Posti hii inahusu namna ya kumpima mtoto uzito, ni njia ambayo utumika kujua uzito wake na maendeleo ya mtoto.
Soma Zaidi...Dalili za Ujauzito mchanga Siku Saba Baada ya Ovulation
Unaweza kujiuliza ikiwa inawezekana kupata dalili za ujauzito mchanga kama siku 7 baada ya kudondoshwa kwa yai (DPO yaani Days Past Ovulation).
Soma Zaidi...