Post hii inahusu njia safi za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni.
Njia za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni.
1. Kama tulivyoona hapo mwanzoni kwamba njia hii utumika kumsafisha Mama kwa kutumia vyuma kawaida mimba ikiwa chini ya miezi minne au wiki kumi na mbili njia hii I aweza kutumika na pia wanaopaswa kuitumia ni wataalamu wa afya sio wake wanaotoa mimba ki magendo ni dhambi kwa Mungu na taifa pia .
2. Kwanza kabisa unapaswa kuandaa vifaa muhimu ambavyo vitaweza kutumika na pia viwe vimepitishwa kwenye usafishwaji wajoto la hali ya juu Ili kuweza kuondoa wadudu ambao wanaweza kuleta madhara baada ya kumsafisha vifaa hivi vinapaswa kutumiwa na wataalamu wa afya tu na sio wale wanaotoa mimba kinyume na utaratibu wa sheria za serikali na ki maadili.
3. Pia mwelezee mama kitu kinachopaswa kufanyika kama ni kumsafisha kwa sababu ya mimba inayotaka kutoka au ni kwa sababu ya kutoa mtoto aliyefia tumboni, pia mama naye anapaswa kukupatia ruhusa ya kufanya hivyo na pia familia inapaswa kuelezea kila kitu kinachoendelea na kuweza kushirikiana nawe kwenye kazi hiyo.na pia pakitokea shida yoyote unapaswa kuwaeleza familia na ndugu wa mama na mama mwenyewe.
4. Kabla ya kuanza kazi unapaswa kufunua sehemu muhimu ambazo unapaswa kufanyia kazi sio kumfunua mama mzima hapo unakuwa umekosea maadili ya kazi, pia mama anapaswa kufunikwa vizuri na vitambaa maalum ambavyo kwa kitaalamu huitwa drape, hivi vitambaa Vimo kila kituo cha afya na pia kwenye hospitali kubwa vipo kabisa.pia wakati wa kazi ikitokea vikachafuka ni vizuri kabisa kuviweka sehemu maalumu na kuweza kumwekea mama vitambaa vingine na kazi inaendelea.
5. Hakikisha kwamba vifaa vyako ambayo unataka kuviweka kwenye uke ili kuweza kutoa kichanga unaviweka vizuri ili kuweza kuepukana na uharibifu kwenye sehemu mbalimbali za via vya uzazi, hakikisha unaviweka sawa pia wakati wa kutoa mimba iliyoharibika ni vizuri kumpiga mama sindano ya ganzi kwa sababu maumivu ni makubwa mno, kwa hiyo namna ya kuweka vifaa inapaswa kuwa sawa ili kuweza kuepukana na uharibifu wowote wa via vya uzazi.
6. Pia unapaswa kusafisha sehemu zote za via vya uzazi kuanzia kwenye sehemu za uke zote kwa kuua bakteria ambao wakiingia ndani wanaweza kuingiza maambukizi, pia na msafishaji anapaswa kuwa makini kwa kuvaa sterile gloves ambazo zinazuia kuingiza uchafu kwenye mwili wa mama na kuzuia magonjwa ambayo yanaweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoa huduma, magonjwa sugu ambayo yanaweza kusambaa ni homa ya nini pamoja na maambukizi ya Ukimwi.
7. Baada ya kusafisha na kuweka vyuma kwenye sehemu husika unapaswa kuvuta uchafu wote kutoka kwa Mama na hakikisha uchafu wote unaisha kabisa na kuhakikisha na damu yote inaisha na pia kama mama ana maumivu unapaswa kumpatia dawa ya maumivu ili aweze kutulia.
8. Baada ya hapo unapaswa kumshauri Mama na kumwambia mda mzuri wa kubeba mimba ili kuweza kuepukana na matatizo ya mimba kutoka mara kwa mara na kama mimba imetoka zaidi ya mara moja ni vizuri kabisa kutafuta sababu ya kutoka kwa mimba.
9. Pia ndugu jamaa na marafiki wote wanapaswa kuwa pamoja na mama ili kuweza kumtunza mama katika kipindi chote mpaka atakapofikia wakati wa kubeba mimba nyingine, na pia jamii inapaswa kuacha mila mbaya na desturi za kuona kwamba kutoa mimba ni mkosi kwa jamii.
10. Kwa hiyo mama baada ya kutoka kwa mimba anapaswa kwenda hospitali ikiwa amepata shida yoyote ya kiafya hata kama hana mtoto kwa sababu changamoto anazozipata Mama baada ya kujifungua na aliyetoa mimba anaweza kupata hizo hizo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua.
Soma Zaidi...Download Kitabu cha elimu ya Ujauzito na malezi ya mimba.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo mtoa huduma anaweza kuzitumia kuangalia kama mtoto amevunjika baada ya kuzaliwa.
Soma Zaidi...PEP Ni dawa ambazo utumiwa na watu wanaojamiiana na watu wenye virus vya ukimwi ila wenyewe hawawezi kupata kwa sababu ya kutumia dawa hizo.
Soma Zaidi...Ukiwa mjamzito unaweza kushuhudia kutokwa na damu. Je damu hii ni ya hedhi?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mwanzo za ujauzito katika wiki ya kwanza
Soma Zaidi...Je unaweza kunielezaKwa mjamzito kuumia wakati wa tendo la ndoa tatizo linaweza kuwa ni nini?
Soma Zaidi...Kama unadhani una tatizo la kuwahi kufika kileleni basi post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa Mwanaume, ni sababu ambazo umfanye mwanaume ashindwe kumpatia mwanamke mimba.
Soma Zaidi...