Uchumi Katika Uislamu
Maana ya Uchumi
- Ni uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa mali, rasilimali na huduma mbalimbali katika jamii ili kujenga mahusiano kati ya binaadamu na Allah (s.w).
Sifa za Uchumi wa Kiislamu
1. Dhana ya mafanikio
Huzingatia hatima yake ambayo ni kupata radhi za Allah (s.w) pekee.
2. Dhana ya umilikaji mali
Mmiliki hakika wa pekee wa mali na rasilimali zote ni Allah (s.w).
3. Dhana ya bidhaa
Ni kitu kilicho safi, kizuri, twahara, halali, n.k.
4. Dhana ya matumizi
Haifai kufuja au kutumia mali au rasilimali kwa njia za haramu.
5. Mizani ya wakati katika kutumia
Ni kujiuliza, nini matokeo ya mali au rasilimali hiyo baada ya muda fulani?
Njia na Misingi ya Uchumi Halali Katika Uislamu
i. Pasiwe na udanganyifu wowote katika uuzaji na ununuzi wa bidhaa au mali.
Rejea Qurβan (17:35), (26:181-183), (83:1-4)
ii. Pasiwe na viapo katika kuuza au kununua bidha, kwani ni miongoni mwa kuuza kwa ujanja-ujanja.
Abu Qatada ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
βKuwa mwangalifu na viapo vingi katika uuzaji, kwa sababu japo
kunarahisisha uuzaji, kuna punguza barakaβ (Muslim).
iii. Pawe na uhuru kamili kwa mnunuzi kuikataa au kuikubali bidhaa baada ya kuiangalia.
iv. Bidhaa yenyewe iwe halali na iwe imechumwa kwa misingi ya halali pia.
v. Kuwepo na maelewano kati ya muuzaji na mnunuzi bila masharti. Dosari yeyote ya bidhaa ijulikane kabla ya manunuzi kufanyika.
vi. Muuzaji awe na uhuru wa kuuza bidhaa yake kwa bei yenye maslahi kwake na isiwe ya kumnyonya mnunuzi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hiibinakwenda kukufundisha mambo ambayo yanaharibu udhu.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi
Soma Zaidi...- Riba ni kipato chochote kile cha ziada kutokana na mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara.
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...