Mtazamo na Msimamo wa Uislamu Juu ya Kudhibiti Uzaz (uzazi wa mpango) na hukumu yake
4. Mtazamo na Msimamo wa Uislamu Juu ya Kudhibiti Uzazi
Kupanga Uzazi Katika Uislamu
- Uislamu unawataka watu kuoana na kuzaana kwa utaratibu na mfumo mzuri ili kutunza na kulea maadili ya familia.
- Uislamu umeweka utaratibu wa umri wa kuzaa kati ya mtoto na mtoto kwa muda wa miaka miwili.
Rejea Qur’an (2:233)
- Uislamu umekataza watu kuzaa nje ya ndoa ambao ni wa kiholela na usiokuwa na malezi bora ya kifamilia.
- Uislamu umeruhusu kuzuia mimba tu kama mwanamke ananyonyesha mtoto mchanga au atadhurika kiafya au kuhatarisha maisha yake.
- Uislamu umeweka utaratibu wa kuzaa na kulea kama njia pekee ya kuendeleza na kujenga kizazi cha mwanaadamu katika maadili na uchumi pia.
Sababu za Uislamu Kupinga Dhana ya Kudhibiti Uzazi
i. Sera ya kudhibiti uzazi inachochea zinaa ambayo ni njia chafu, mbaya na ina madhara makubwa katika jamii ya binaadamu.
Rejea Qur’an (17:32), (24:2)
ii. Sera ya kudhibiti uzazi ni kupinga na kuingilia mpango wa Allah (s.w) katika kupanga uzazi kwa njia ya ndoa.
Rejea Qur’an (2:187), (2:233), (30:21)
iii. Dhana kuwa kuongezeka watu hupunguza riziki ni potofu na ni shirki, kwani ni kukana uwezo wa Allah (s.w) wa Kuruzuku na Kumiliki kila kitu.
Rejea Qur’an (29:60)
iv. Kudhibiti uzazi ni kupoteza stara, hifadhi, huruma na mapenzi ya kweli baina ya mwanamke na mwanamume ambapo ni kinyume na utaratibu wa Allah (s.w).
v. Kudhibiti uzazi kwa hofu ya umaskini ni haramu, kwani kila kiumbe Allah
(s.w) amekikadiria riziki yake.
Rejea Qur’an (17:31)
vi. Sera juu ya kudhibiti uzazi inalengo la kuepuka jukumu la kuzaa, kulea na kuendeleza kizazi kwa utaratibu unaofaa.
vii. Sera ya kudhibiti uzazi ni kuchochea ngono huru, ukahaba, kuzaliwa watoto kiholela wasiokuwa na baba na kuondoa nafasi ya ndoa katika jamii.
viii. Kudhibiti uzazi ni dhana ya uchoyo, ubadhirifu na ulafi wa kutaka kumiliki na kutumia rasilimali, uchumi, siasa, n.k kwa watu wachache
Sababu Zinazokulika Kudhibiti Uzazi Katika Uislamu
i. Kuhifadhi au kulinda afya ya mama asishike mimba baada ya kuthibitishwa na daktari anayeaminika kuwa itahatarisha afya au uhai wake.
ii. Iwapo mama ananyonyesha mtoto mchanga kwani mtoto anaweza kuathirika kiafya.
iii. Ikiwa mwanamke hawezi kuzaa ila kwa kufanyiwa operesheni, atalazimika kuzuia mimba baada ya kuzaa kwa operesheni mimba tatu.
Baadhi ya Njia Zinazotumika Kudhibiti Uzazi
a) Njia za Kisasa (Morden Method):
i. Kondom, mipira ya kiume na kike (Contraceptives). ii. Kitanzi-loop (Intra uterine device).
iii. Vidonge vya majira (Ant baby pill).
iv. Kufunga kitanzi kwa mwanamke (Tube Legation). v. Kufunga uzazi kwa wanaume (Vasectomy).
vi. Kutoa mimba (abortion).
vii. Uzazi wa maabara (test tube babies).
viii. Kukodisha matumbo ya wanawake wengine, kupandikiza mbegu (surrogate mothers)
b) Njia za Asilia, Maumbile (Natural Method):
i. Kufuata kalenda ya uzazi ya mwanamke (Menstrual Period or Circle).
ii. Kumwaga mbegu za uzazi nje kwa mwanamume (Coitus Interrunts or withdrawal)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah.
Soma Zaidi...Jinsi ya kumuosha maiti wa kiislami mwanaume au mwanamke
Post hii inakwenda kukufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya kumuosha maiti wa kiislamu
Soma Zaidi...Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...Nini kifanyike baada ya mazishi ya kiislamu
Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika.
Soma Zaidi...Hadhi na Haki za Mwanamke katika jamii mbalimbali hapo zamani
Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.
Soma Zaidi...