Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua

Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua

Taratibu za Ndoa ya Kiislamu

Ndoa ya Kiislamu hukamilika kwa kutekelezwa taratibu zake zote kama ifuatavyo;



a) Kuchagua Mchumba

- Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa, Mtume (s.a.w) amesema:

'Mwanamke anaolewa kwa vitu vinne; kwa Utajiri wake, Hadhi yake, Uzuri wake wa sura na kwa dini yake. Mchague yule mwenye msimamo mzuri wa
dini'.'

(Bukhari na Muslim)



- Kwa mujibu wa Hadith hii, Dini ndio sifa ya msingi kuzingatia katika kutafuta mchumba kisha sifa zingine kama elimu, umbo, sura, ukoo, n.k zinafuata. Rejea Qur'an (5:5), (2:221), n.k


- Ni haramu kwa Muislamu kuoa au kuolewa na asiye kuwa muislamu kama kafiri, mshirikina, mkristo, n.k na hata kushiriki katika ndoa na ibada zao pia. Rejea Qur'an (24:26), (9:71), (24:3), n.k



- Si ruhusa kuwaoa Ahlal-Kitaab (Mayahudi na Wakristo) wa zama hizi kwani walikuwa ni wale tu walioamini haki na kuifuata kabla ya kuja Uislamu.
Rejea Qur'an (5:5)



- Wachumba wanaruhusiwa kuonana kabla ya kuoana (ndoa) ila katika mipaka ya Uislamu ili kujuana na kuridhiana.




b) Maharimu

- Ni wanaume na wanawake walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba kama ilivyobainishwa katika Qur'an na Sunnah.


- Wanawake walioharamishwa kuolewa kama walivyobainishwa katika Qur'an

(4:22-24) ni hawa wafuatao;


i. Mwanamke aliyewahi kuolewa na baba yako.

(Babu yako, baba wa baba yako wa kuumeni na kikeni)



ii. Mama (mzazi) aliyekuzaa.

(Bibi aliyezaa waliokuzaa, mama wa bibi aliyezaa aliokuzaa,')



iii. Binti yako uliyemzaa (au binti aliyezaliwa na uliyemzaa,....), binti wa kunyonya na mwanao (na kizazi chake, '.)


iv. Dada yako khaalisa au wa kwa baba au wa kwa mama


v. Shangazi yako; (dada wa baba yako, na dada wa babu yako '.).


vi. Mama mdogo; (ndugu wa mama yako, au ndugu wa bibi yako, '.).


vii. Binti wa ndugu yako mwanamume, khaalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa na yeye).

viii. Binti wa baba yakokhaalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa naye).

ix. Mama wa kukunyonyesha (na mama zake wa kumzaa au wa kumnyonyesha).

x. Dada yako wa kunyonya naye (aliyenyonyeshwa na aliyekunyonyesha).


xi. Mama yake mkeo wa kumzaa (mama mkwe) au wa kunyonyesha (na bibi yake wa kumzaa mama yake au wa kumnyonyesha').
Ama ndugu yake mama yake mkeo yaani, mama mdogo wake au shangazi yake (baba yake mkeo) wa kuzaliwa au kunyonya, unaweza kumuoa akifa mkeo au utakapomuacha na eda ikaisha.


xii. Binti wa mkeo uliyemuingilia (na mjukuu wake,'.).

xiii. Mke aliyewahi kuolewa na mwanao wa kumzaa au wa kunyonyeshwa na mkeo (na kizazi chaki), si mke wa motto wa kupanga au motto wa kulea.


xiv. Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja. Ama akifa mkeo au ukimuacha na eda ikaisha unaweza kumuoa dada yake au shangazi yake au mama yake mdogo.

xv. Mke wa mtu aliye katika ndoa ni haramu.

Wanawake hawa wameharamishwa kuolewa na wanaume wanaofanana na hawa kwa upande wa kiumeni pia.


- Kuna wanawake na wanaodhaniwa ni maharimu lakini si maharimu (si haramu kuwaoa) kisheria. Hawa ni pamoja na mtoto wa baba mdogo, mama mdogo, shangazi, mjomba. Kwa ushahidi wa aya ifuatayo;


'Na (tumekuhalalishia kuwaoa) mabinti wa ami zako na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako na mabinti wa dada za mama zako ' (33:50).



c) Mahari

- Ni kiasi cha mali au kitu anachotoa muoaji kumpa muolewaji kama zawadi

(hidaya) kutoka kwa Allah (s.w).

Rejea Qur'an (4:4), (5:5)

- Mahari haina kiwango maalum na ni uhuru wa mwanamke anayeolewa kutoza kiasi apendacho bali, kisiwe kikubwa au kidogo mno.
Rejea Qur'an (4:20, 24)



Je, Mahari inashusha Hadhi ya Mwanamke?

Jibu Hapana

- Mahari ni hidaya (zawadi) kutoka kwa Allah (s.w) kwa ajili ya kupata radhi zake na kuhalalisha ndoa.


- Mahari humpa sitara mwanamke anayeolewa kwani atakuwa halali tu kwa mwanamume aliyemtolea mahari na kumuoa.

- Mahari huondoa hisia za mwanamume kuona kuwa ndio bei au thamani yake kwa anayemuoa, kwani thamani yake sio sawa na mahari, ni zawadi tu.

- Mahari ni amri ya Allah (s.w) kupewa mwanamke anayeolewa ili kumpa thamani na hadhi zao na kutoonekana ni watu wa kuolewa bure bure.

Jibu Ndiyo

- Kama mahari itafanywa ndiyo bei na thamani ya mwanamke anayeolewa kwa kutozwa na wazazi, huku muolewaji anakosa uhuru wa kutoza mwenyewe.


- Kiasi cha mahari kinachotozwa kinamfanya mwanamke muolewaji atoze

(auzike) kulingana na uzuri, ukoo, hadhi aliyonayo.


- Mahari ikiwa kubwa sana hupelekea ugumu wa kuoa kwa muoaji, hivyo hifadhi ya mwanamke itakosekana katika jamii.


- Mahari ikitozwa kubwa au ndogo sana, hupelekea mzozo, kutohurumiana na kutothaminiana baina ya wanandoa pindi ikitokea wanaachana.



d) Khutuba ya Ndoa

- Ni sunnah kusoma khutuba ya ndoa kabla ya kufunga ndoa kama ukumbusho wa kutii maamrisho ya Allah (s.w) kwa wanaooana na waumini kwa ujumla.



- Khutuba ya ndoa ina sehemu kuu mbili zifuatazo;

i. Kumhimidi Allah (s.w) kwa sifa zake (maamkizi mema). ii. Shahada zote mbili.
Rejea Qur'an (3:102), (4:1), (33:70-71).



e) Kufunga Ndoa

Ndoa ya Kiislamu hufungika kwa kutekelezwa mambo yafuatayo;

- Muoaji atekeleze masharti ya kuoa

- Muolewaji atekeleze masharti ya kuolewa.

- Pawe na walii au idhini yake.

- Pawe na mashahidi wawili au zaidi.

- Pawe na idhini (ridhaa) ya muolewaji.

- Pawe na Ijabu na Kabuli.



Masharti ya Kufunga Ndoa ya Kiislamu

a) Muoaji atekeleze masharti ya kuoa kama ifuatavyo;

- Mke anayemuoa alzima awe muislamu mwema.

- Awe anaoa kwa hiari yake.

- Asiwe maharimu wa mke anayetaka kumuoa.

- Awe amebaleghe na mwenye akili timamu.

- Asiwe katika Ihramu ya Hija.

- Asiwe katika ndoa ya wake wanne anaoishi nao katika ndoa.



b) Muolewaji atekeleze masharti ya kuolewa kama ifuatavyo;

- Mume anayetaka kumuoa ni lazima awe muislamu mwema.

- Asiwe katika ndoa ya mume mwingine.

- Asiwe katika eda ya mume mwingine.

- Asiwe maharimu wa mume anayetaka kumuoa.

- Awe muislamu mwema mwenye akili timamu.

- Asiwe katika Ihramu ya Hija.

- Awe anaolewa kwa hiari yake.



c) Pawe na Walii au Idhini yake;

- Ndoa ya Kiislamu haswihi mpaka awepo Walii wa binti anayeolewa kwani ndiye mfungishaji wa ndoa au kutoa idhini kwa mtu mwingine mjuzi.
- Binti hana idhini ya kujiozesha mwenyewe.



- Mawalii wanaoweza kuozesha katika Uislamu ni hawa wafuatao;

i. Baba mzazi wa mwanamke anayeolewa. ii. Babu mzaa baba yake.
iii. Ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja. iv. Ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja.
v. Mtoto wa kiume wa ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja (mpwa wake).
vi. Mtoto wa kiume wa ndugu (kaka) yake wa kiume wa baba mmoja.

vii. Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja na mama mmoja.
viii. Baba yake mdogo (Ami) aliyezaliwa na baba yake kwa baba mmoja tu. ix. Mtoto wa kiume wa baba mdogo wake wa baba mmoja na mama mmoja. x. Mtoto wa kiume wa baba mdogo wake wa baba mmoja tu.
xi. Serikali ya Kiislamu (Hakimu au Kadhi) katika nchi za Kiislamu.



- Walii wa daraja ya chini hana ruhusa ya kuozesha kama wa juu yake yupo mpaka apewe idhini.



Masharti na Sifa za Walii ili aozeshe

1. Awe muislamu mwanamume.

2. Asiwe mtumwa (sio watumwa).

3. Awe mwema na mwenye akili timamu.

4. Awe anaozesha baada ya kupatikana idhini ya muolewaji.

5. Awe mwadilifu.



d) Pawe na Mashahidi wawili au zaidi wenye sifa zifuatazo;

- Wawe watu wazima waliobaleghe, watoto hawawezi kuwa mashahidi.

- Wawe na akili timamu.

- Wawe waislamu wema wanaume.

- Wawe waadilifu.

- Wawe waungwana, sio watumwa.



e) Pawe na Ridhaa au Idhini ya mwenye kuolewa

- Ndoa ya Kiislamu haiswihi bila idhini ya muolewaji kupatikana. Na idhini yake hupatikana kwa kuwa kimya (kunyamaza kimya).
- Akikataa ndoa haiswihi.



f) Pawe na Ijabu na Kabuli

- Ijabu; ni maneno anayesema Walii (Muozeshaji) kumwambia mume anayeoa.

Mfano: 'Nimekuoza Aisha binti Salimu'.'



- Kabuli; ni maneno ya mume anayeoa kukubali kumuoa binti.

Mfano: 'Nimekubali kumuoa Aisha binti Salimu'



- Hivyo, Ijabu ni kauli rasmi anayotoa Walii (muozeshaji) na Kabuli ni kauli rasmi anayotoa mume anayeoa.



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1101


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

DUA ZA SWALA
DUA ZA SWALA 1. Soma Zaidi...

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
2. Soma Zaidi...

quran na tajwid
TAJWID Utangulizi wa elimu ya Tajwid YALIYOMO SURA YA 01 . Soma Zaidi...

Kujiepusha na kufuata mambo kwa kibubusa
Waislamu wanakatazwa kufanya na kufuata mambo kwa kibubusa (kwa mkumbo) bila ya kuwa na ujuzi unaostahiki. Soma Zaidi...

Epuka kukata tamaa, na yajuwe madhara ya kukata tamaa
37. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah
Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Soma Zaidi...

Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah
7. Soma Zaidi...

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga
Soma Zaidi...

Taqwa (Hofu ya kumuogopa Allah) ni popote ulipo
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '... Soma Zaidi...

NAMNA YA KUSWALI SEHEMU YA KWANZA
Mtume (s. Soma Zaidi...

Kujiepusha na Shirk
Shirki ni kitendo chochote cha kukipa kiumbe nafasi ya Allah (s. Soma Zaidi...