Mtazamo na Msimamo wa Uislamu Juu ya Kudhibiti Uzaz (uzazi wa mpango) na hukumu yake

Mtazamo na Msimamo wa Uislamu Juu ya Kudhibiti Uzaz (uzazi wa mpango) na hukumu yake

4. Mtazamo na Msimamo wa Uislamu Juu ya Kudhibiti Uzazi

Kupanga Uzazi Katika Uislamu

- Uislamu unawataka watu kuoana na kuzaana kwa utaratibu na mfumo mzuri ili kutunza na kulea maadili ya familia.


- Uislamu umeweka utaratibu wa umri wa kuzaa kati ya mtoto na mtoto kwa muda wa miaka miwili.
Rejea Qur'an (2:233)

- Uislamu umekataza watu kuzaa nje ya ndoa ambao ni wa kiholela na usiokuwa na malezi bora ya kifamilia.


- Uislamu umeruhusu kuzuia mimba tu kama mwanamke ananyonyesha mtoto mchanga au atadhurika kiafya au kuhatarisha maisha yake.

- Uislamu umeweka utaratibu wa kuzaa na kulea kama njia pekee ya kuendeleza na kujenga kizazi cha mwanaadamu katika maadili na uchumi pia.Sababu za Uislamu Kupinga Dhana ya Kudhibiti Uzazi

i. Sera ya kudhibiti uzazi inachochea zinaa ambayo ni njia chafu, mbaya na ina madhara makubwa katika jamii ya binaadamu.
Rejea Qur'an (17:32), (24:2)ii. Sera ya kudhibiti uzazi ni kupinga na kuingilia mpango wa Allah (s.w) katika kupanga uzazi kwa njia ya ndoa.
Rejea Qur'an (2:187), (2:233), (30:21)iii. Dhana kuwa kuongezeka watu hupunguza riziki ni potofu na ni shirki, kwani ni kukana uwezo wa Allah (s.w) wa Kuruzuku na Kumiliki kila kitu.
Rejea Qur'an (29:60)

iv. Kudhibiti uzazi ni kupoteza stara, hifadhi, huruma na mapenzi ya kweli baina ya mwanamke na mwanamume ambapo ni kinyume na utaratibu wa Allah (s.w).

v. Kudhibiti uzazi kwa hofu ya umaskini ni haramu, kwani kila kiumbe Allah

(s.w) amekikadiria riziki yake.

Rejea Qur'an (17:31)

vi. Sera juu ya kudhibiti uzazi inalengo la kuepuka jukumu la kuzaa, kulea na kuendeleza kizazi kwa utaratibu unaofaa.


vii. Sera ya kudhibiti uzazi ni kuchochea ngono huru, ukahaba, kuzaliwa watoto kiholela wasiokuwa na baba na kuondoa nafasi ya ndoa katika jamii.

viii. Kudhibiti uzazi ni dhana ya uchoyo, ubadhirifu na ulafi wa kutaka kumiliki na kutumia rasilimali, uchumi, siasa, n.k kwa watu wachache
Sababu Zinazokulika Kudhibiti Uzazi Katika Uislamu

i. Kuhifadhi au kulinda afya ya mama asishike mimba baada ya kuthibitishwa na daktari anayeaminika kuwa itahatarisha afya au uhai wake.


ii. Iwapo mama ananyonyesha mtoto mchanga kwani mtoto anaweza kuathirika kiafya.

iii. Ikiwa mwanamke hawezi kuzaa ila kwa kufanyiwa operesheni, atalazimika kuzuia mimba baada ya kuzaa kwa operesheni mimba tatu.Baadhi ya Njia Zinazotumika Kudhibiti Uzazi

a) Njia za Kisasa (Morden Method):

i. Kondom, mipira ya kiume na kike (Contraceptives). ii. Kitanzi-loop (Intra uterine device).
iii. Vidonge vya majira (Ant baby pill).

iv. Kufunga kitanzi kwa mwanamke (Tube Legation). v. Kufunga uzazi kwa wanaume (Vasectomy).
vi. Kutoa mimba (abortion).

vii. Uzazi wa maabara (test tube babies).

viii. Kukodisha matumbo ya wanawake wengine, kupandikiza mbegu (surrogate mothers)
b) Njia za Asilia, Maumbile (Natural Method):

i. Kufuata kalenda ya uzazi ya mwanamke (Menstrual Period or Circle).

ii. Kumwaga mbegu za uzazi nje kwa mwanamume (Coitus Interrunts or withdrawal)                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 261


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

ijuwe maawe maan ya kusimamisha swala
Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUUMBWA KWA NABII ADAMU (A.S)NA HADHI YAKE NA HADHI YA WANAADAMU DUNIANI
Adam(a. Soma Zaidi...

maana ya swala kilugha na kisheria
Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee 'Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...

Biashara haramu na njia zake katika uislamu
Soma Zaidi...

Vipengele vya Mikataba ya 'Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina
Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A. Soma Zaidi...

Kumuandaa Maiti kabla ya kufa ama kukata roho
Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA MAMA AMINA MKE WA ABDALLAH MTOTO WA ABDUL-AL MUTALIB
KUZALIWA KWA MTUME (S. Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa Tawala za kifalme baada ya uongozi wa Makhalifa.
Kuanzishwa Ufalme. Soma Zaidi...

Sifa za wuamini zilizotajwa katika surat Al-ma'aarij
Kwa hakika binaadamu ameumbwa, hali ya kuwa mwenye pap atiko. Soma Zaidi...

Kuandaliwa Mtume(s.a.w) maandalizi ya kimafunzo na maandalizi ya ki ilham
Mitume huzaliwa Mitume. Soma Zaidi...

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
1. Soma Zaidi...