Haki ya Kushiriki Katika Siasa.
Haki ya Kushiriki Katika Siasa.
Siasa ni mambo yote yale yanayohusiana na jamii kwa ujumla. Hivi sasa neno siasa Iimefungamanishwa zaidi na uendeshaji wa Serikali na utawala. Tukumbuke kuwa Uislamu ni mfumo unaotawala uendeshaji wa maisha yote ya binaadamu. Hakuna kipengele chochote cha maisha, Si uchumi, siasa, utamaduni, n.k. ambacho kiko nje ya usimamizi wa Uislamu. Pia Qur'an imedhihirisha wazi kuwa jukumu Ia kuiendesha jamii katika misingi ya Kiislamu liko kwa wote, wanawake na wanaume. Qur'an inawataka Waislamu wote washirkiane katika kutenda na kuamrisha yaliyo mema na washirikiane katika kuyaepuka na kuyakataza yaliyo maovu na yanayovuruga amani. Hatuikuti Qur'an kuwabagua wan awake na wanaume katika jukumu hili bali inasisitiza:
Na Wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake ni marafiki wao kwa wao huyaamrisha yaliyo mema na kuyakataza yaliyo mabaya na husimamisha swala na hutoa zaka na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu na Mwenye hi/dma. (9:71).
Je, wanawake wanaruhusiwa kutoa maoni yao juu ya masuala ya kisiasa?
Katika Uislamu, wanawake wanayo haki sawa na wanaume katika kutoa maoni yao juu ya uongozi wa nchi. Ukirejea na kukiangalia kile kipindi bora katika historia ya Uislam, kipindi ambacho Waislamu walikuwa wakiyaendesha mambo yao kwa misingi ya Uislamu yaani wakati wa Mtume (s.a.w) na wakati wa Makhalifa wanne wa Mtume (s.a.w) tutaona kuwa wanawake walishiriki katika masuala ya jamii zao.
Sura ya 58 katika Qur'an inaitwa "Mujadila" kwani inataja habari za mwanamke aitwaye Khuwaylah binti Tha'Iabah, mke wa Aus bin Samit, ambaye alikwenda kulalamika kwa Mtume (s.a.w) juu ya mila ya kijahili iliyojulikana kwa jina Ia "Zihar'. Mtume (s.a.w) hakuwa na majibu kuhusiana na majadiliano aliyoyafanya na Khuwaylah, ndipo Allah (s.w) akateremsha aya za kisheria za kuharamisha "Zihar'.
Mwenyezi Mungu ameshasikia usemi wa mwanamke yule anayejadiliana nawe sababu ya mum ewe na anashtaki mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. Wale miongoni mwenu wawaitao wake zao mama zao) hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa. Wanasema neno baya na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Msamaha na Mwenye Maghfira..
Na wale wawaitao wake zao mama zao kisha wakarudia katika yale waliyosema basi wampe mtumwa huru kabla ya kugusana. Mnapewa maonyo kwa haya. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyatenda. Na asiyepata (mtumwa) basi afunge saumu ya miezi miwili mfululizo kabla ya kugusana; na asiyeweza basi awalishe maskini sitini. (Mmeamrishwa) haya ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake; na hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu) na kwa makafiri iko adhabu iumizayo. (58: 1-4).
Khuwaylah alikwenda kujadiliana na Mtume (s.a.w) juu ya suala hili Ia kisheria na akatoa masikitiko yake. Qur'an kakika aya hizi, iliondosha tatizo hili katika jamii na wala haikumlaumu mwanamke huyu kwa kutoa malalamiko yake. Wala Mtume (s.a.w) hakumkataza kutoa malalamiko hayo. Wakati wa Ukhalifa wa Uthman, bibi Aisha mke wa Mtume (s.a.w) hakuafikiana na maamuzi mengi ya Uthman. Pamoja na hayo Uthman hakupata kumwambia hana haki ya kutoa maoni yake juu ya masuala ya dola kwa sababu yeye ni mwanamke. Bibi Aisha pia alipinga vikali sana uteuzi wa Au kuwa Khalifa, na baadhi ya masahaba walimuunga mkono. Hakuna aliyesema; Wewe ni mwanamke, huna haki ya kuingilia masuala haya. Hapana shaka yoyote kuwa baadaye Bibi Aisha alijutia sana msimamo wake huo wa kupinga uteuzi wa Au. Hakujutia kwa sababu alijiingiza katika masuala ya kisasa, Ia. Bali alijutia kwa sababu rai yake juu ya Ali haikuwa sahihi.
Aidha siku moja Khalifa Uthman alikuwa amekaa na mshauri wake mkuu aitwaye Mar'wan bin Hassan. Mkewe Uthman alikuwepo wakati Mar'wan akimshauri Uthman. Akaupinga ushauri wa Mar'wan. Mar'wan akakasirika akasema: Nyamaza, tunazungumza mambo ambayo hayakuhusu. Khalifa Uthman akasema: Mwache kwa sababu yeye ni mkweli zaidi katika nasaha zake kwangu kuliko wewe. Tazama, Uthman hakusema, sawa wewe ni mke tu, nyamaza. Hii ni mifano tu.
Hapana shaka kuwa katika Uislamu msisitizo ni kuwa jukumu Ia kwanza ni kuwa mke ni mjenzi na miezi wa nyumba yake, iii nyumbani pawe ni kimbilio, kwa sbabu ya utulivu, furaha na amani. Lakini hii haina maana kuwa kwa sababu hiyo mwanamke hatakiwi kutoa rai yake juu ya masuala ya kisiasa.
Je, Wanawake Wanayo Haki ya Kupiga Kura?
Muundo wa upigaji kura siku hizi ni tofauti na ulivyokuwa zamani.
Siku hizi kuna kujiandikisha, halafu vituo na masanduku maalum na mihuri ya kupigia kura. Katika zama za Mtume (s.a.w) ikiwa watu walitaka kumchagua mtu fulani kuwa kiongozi walitumia utaratibu uliojulikana kama "Bai'at" yaani kiapo cha utiifu (oath of allegiance). Utaratibu huu umetajwa katika Qur'an na Hadith. Allah (s.w) amesema katika Qur'an:
Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake walioamini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaozusha tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawakuasi katikajambojema, basipeana ahadi nao na uwatakie maghufira kwa Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwingi wa rehema. (60: 12). Na katika mkataba wa Aqabah Mtume (s.a.w) alichukua ahadi ya ama hiyo kwa wanaume na wanawake. Haki ya watu wote kupiga kura (universal suffrage) katika nchi za Ulaya magharibi imekuja miaka 1200 baada ya haki hiyo kutangazwa na Uislamu.
"Bai'at" Ilihusu Masuala ya Imani tu? Kutokana na aya hiyo hapo juu (60: 12) wako watu wanaotoa hoja kuwa "bai'at" yaani ahadi ya utii ilihusu masuala ya imani tu, hivyo haiwezi kuhusu viongozi wa serikali au dola. Hoja hii haina nguvu kwa sababu:
1.Mtume (s.a.w) alipewa ahadi ya utii siyo tu kama Mtume bali pia kama kiongozi wa dola (head of state).
2.Katika Uislam hakuna mgawanyo wa vipengele vya kiimani na kidunia, mambo yote yamefungamana pamoja. Imani pia inahusiana na uadilifu, sheria n.k.
3.Aya (60: 12) pia imesema Iwapo "hawakuasi katika jambo jema". Msemo huu unaashiria kuwa ahadi hiyo pia inahusu maamuzi atakayoyafanya kama kiongozi wa dola, kama vile maamuzi ya Kisiasa au kijeshi.
Je, Wanawake wanayo haki ya kushiriki katika Bunge?
Muundo wa mabunge ya leo ni tofauti kabisa na hali ilivyokuwa wakati wa Mtume (s.a.w). Msingi wa kuwepo bunge hata hivyo ni kuwapa fursa wana jamii kujadiliana juu ya mambo yanayoihusu jamii yao. Katika Uislamu msingi mmojawapo wa uendeshaji wa serikali ya Kiislamu ni "Shuura". Waislam lazima washauriane katika uendeshaji wa mambo yao. Khalifa (kiongozi) aliwaita watu wengi au wachache na kutaka ushauri wao juu ya jambo fulani. Hivyo utaratibu huu haukuwa rasmi. Hata hivyo amri ya kushauriana ipo katika Qur'an hivyo muundo wa kupata ushauri huo waweza kubadilika kulingana na kubadilika kwa mazingira, maadam amri ile ya kushauriana inatekelezwa.
Hata hivyo baada ya kutawafu Mtume (s.a.w) ilizuka dhana ya kuwa na "A h/ui haai wal aqi yaani watu wenye vipawa na uwezo maalum kuwa ndio watakaofanya kazi hii ya kumshauri kiongozi wa dola. Wanawake wenye uwezo huo waliendewa majumbani mwao na kutakiwa watoe ushauri wao. Hakuna mwanachuoni au Khaljfa aliyesema: Kwa nini
mnawataka shauri wanawake au wanawake wasihusishwe na siasa. Sharti pekee Ia kuzingatia ni kuwa yote hayo yafanywe kwa kuzingatia misingi ya Uislamu, adabu za Kiislamu na maadili yake. Kisa kimoja kilichotokea wakati wa ukhalifa wa Umar(r.a) chaweza kusaidia kufafanua haki ya wanawake kushiriki katika maamuzi.
Umar (r.a)aliona na hakufurahishwa na tabia iliyozuka ya wanawake kudai mahari kiasi kikubwa sana. Hivyo akaamua kuikomesha tabia hiyo, akasimama katika mimbar msikitini na kusema kuwa kuanzia wakati ule mahari isivuke dirham 400. Na mwanamke atakayedai mahari yatakayozidi dirham 400 basi ziada yote nitaichukua na kuitia katika Baitul MaaI yaani hazina ya serikali ya Kiislam. Papo hapo akasimama mwanamke mmoja amasema: "Yaa Umar! Laisa Laka dhaalika", yaani "Ewe Umar! Huna mamlaka juu ya hilo". Akamkumbusha aya ya Qur'an (4:20) inayowakataza wanaume kudai mahari wanapowaacha wake zao hata kama waliwapa "mrundi wa mali". Neno lililotumika katika Qur'an ni "Qintara" yaani tani. Yaani hata kama mtu atakuwa ametoa tani za dhahabu kama mahari. Yule mwanamke akamwuliza Umar, kwa misingi gani wewe unataka kuwanyang'anya wanawake haki waliyopewa na Allah?
Lau ingekuwa ni makosa kwa mwanamke kusimama katika hadhara ya wanaume na kutoa rai yake basi watu wote wangemkemea na kumtaka akae chini. Hakuna aliyemkataza. Na baada ya kusema hivyo Umar akasema kwa unyenyekevu: "Mwanamke yu sahihi na Umar amekosea". Na akaifuta kauli yake. Umar anajulikana kuwa alikuwa kiongozi madhubuti ambaye hachelei chochote katika kusimamia dini ya Allah. Lau kama ingekuwa ni makosa kwa mwanamke kusimama katika hadhara ya wanaume na kutoa fikra zake basi Umar asingesita hata kidogo kusema: Sawa mimi nimekosea, na wewe pia umekosea kusimama hadharani na kutoa rai yako.
Huu ni mfano wa majadiliano ya wazi (open discussion) ya kujadili muswada wa sheria ambayo Umar alitaka kuipitisha. Lakini ilikwama kwa sababu ya hoja zilizotolewa na mwanamke yule. Kisa hiki kinaweza kulinganishwa na majadiliano ya bungeni katika vipengele vifuatavyo:
(i)Umar, ambaye alikuwa ni kiongozi wa Waislamu alipoona kuwa wanawake walikuwa wakitaja mahari mengi na akaamua kuzuia tabia hiyo kwa kuweka kiwango cha juu kabisa kisizidi dirham 400. Leo,kitendo hicho kinaweza kulinganishwa na uamuzi wa serikali au mswada (bill) wa sheria unaowasilishwa bungeni.
(ii)Mapendekezo hayo ya Umar yalitangazwa msikitini. Na kwa Waislamu msikitini si mahali pa kuendeshea swala tu bali pia katika zama zote msikiti umekuwa ukitumika pia kama mahali pa kujadiliana juu ya masuala mbali mbali ya kijamii, kisiasa na kijeshi. Misikiti pia ilikuwa ndiyo maktaba ya Waislam na mahali pa kuendeshea darsa. Hivyo, misikiti ni majlisi ya halali ya Waislamu kujadiliana mambo yao kama ilivyo bunge. Tofauti iliyopo ni kuwa bunge linaruhusu watu maalum tu lakini misikiti iwazi kwa kila Muislamu.
(iii)Ukweli kuwa Umar aliutangaza uamuzi huo hadharani kabla ya kuutekeleza kunaonesha kuwa watu walikuwa wamepewa fursa ya kutoa rai zao au upinzani wao juu ya uamuzi huo kama ambavyo wabunge hutoa rai zao juu ya mswada wa sheria.
(iv)Yule mwanamke aliupinga uamuzi wa Umar kwa sababu ulikwenda kinyume na Qur'an. Katika sheria za mabunge, katiba ya nchi ndiyo sheria kuu ya nchi (basic law of the land). Sheria yoyote itakayokiuka katiba hutanguka kwani katiba ndio msingi wa sheria zote. Na kwa Waislam Qur'an ndiyo Katiba yao, ndiyo msingi wa sheria zote. Uamuzi wowote unaokiuka Qur'an ni batili na hauwezi kuruhusiwa kupita. Hivyo yule mwanamke alimwonyesha Umar kuwa uamuzi wake ulikuwa unakiuka Qur'an, katiba ya Waislamu. Katiba ambayo haiwezi kufanyiwa marekebisho.
(v)Umar alikiri kuwa yule mwanamke alikuwa sahihi na yeye alikuwa amekosea. Kitendo hicho cha Umar kinaweza kulinganishwa na uamuzi wa serikali kuuondosha mswada wake bungeni.
Hivyo ni dhahiri kuwa kuna kufanana kati ya kisa hiki na majadiliano ya bunge. Zaidi ya kufanana huko yapo pia mambo mengine ya kuzingatia.
Kwanza, ni kuwa msimulizi wa Hadith amesema "Mwanamke alisimama nyuma" bila kulitaja jina Ia mwanamke huyo. Kwa kawaida wasimulizi wa Hadith husema fulani bin au binti fulani alisema kadha kadha. Kutomtaja jina hapa kunaonesha kuwa mwanamke aliyetoa hoja ya kumpinga Umar hakuwa mwanamke mashuhuri anayejulikana kwa watu wengi bali ni mwanamke wa kawaida tu. Na hili laonesha kuwa uhuru na haki ya kumsahihisha kiongozi hata kama ni mkuu wa nchi alikuwanao kila mtu.
Pili, ni kuwa msikiti ulikuwa umefurika watu,ambao waliishi na kumfuata Mtume Muhammad (s.a.w) alipokuwa hai pamoja nao. Walikuwepo maswahaba ambao Mwenyezi Mungu amewasifu katika Qur'an (9: 100) kwa ucha Mungu wao. Lakini hakuna hata mmoja aliyemkemea mwanamke huyo kwa kusimama hadharani na kutoa hoja yake. Na Umar ambaye ujasiri na ukali wake unajulikana sana asingeliruhusu hilo kutokea machoni pake lau angejua kuwa linapingwa na Sheria ya Kiislam.
Na mfano mwingine ni kuwa baada ya kuuliwa kwa Umar, na mashauriano yalipokuwa yakifanyika juu ya nani ashike uongozi wa dola ya Kiislam, Bwana Abdulrahman bin Auf alipewa jukumu Ia kuwauliza watu yupi kati ya Uthman na Ali awe kiongozi. Na imeelezwa katika kitabu kiitwacho AI-Bidaya Wan Nihaya kilichoandikwa na mwanahistoria mashuhuri lbn Kathiir kuwa miongoni mwa watu walioulizwa walikuwa wanawake.
Je, Uislamu unawakataza wanawake kuwa viongozi?
Ili swali hili lijibiwe kwa ufasaha inabidi kwanza upatikane ufafanuzi juu ya nini maana ya uongozi. Katika tafsiri yenye upeo mpana uongozi ni nafasi ya madaraka ya kubeba dhamana (responsibility) na ya kutoa mwongozo au maelekezo.
Tutaona katika kipengele kifuatacho "Haki ya Elimu" kuwa katika jamii bora ya Kiislamu (ideal Muslim society) ni vizuri baadhi ya wanawake wawe madaktari, walimu, wauguzi n.k. Je, hizi si nafasi muhimu zenye dhamana nzito? Je, hizi si nafasi za kutoa mwongozo na maelekezo kwa wengine?
Na hata kama mwanamke hajaajiriwa, nani anaweza kusema kuwa nafasi ya mama nyumbani haibebi majukumu ya uongozi? Nani anaweza kusema kuwa malezi ya watoto si dhamana inayohitaji kutoa maelekezo na mwongozo? Na ni jukumu lipi hasa ambalo ni muhimu zaidi kuliko lile Ia kukiongoza kizazi kipya katika njia iliyonyooka? Kwa hakika ni kukosekana kwa uongozi huu muhimu ndiko kunakochangia kwa kiasi kikubwa sana kuparaganyika na kuanguka kwa jamii zetu leo.
Kutokana na ukweli huu Mtume (s.a.w) amesema katika Hadith:
"Kila mmoja wenu ni mchungaji (yaani kiongozi,), na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya alivyovichunga. Mtawala ataulizwa juu ya raia zake, mume ataulizwa juu ya familia yake, mke ataulizwa juu ya wan awe na nyumba yake, mtumishi ataulizwa juu ya amana alizokabidhiwa ". (Bukhari na Muslim)
Kutokana na Hadhith hii hata kama mwanamke hakuajiriwa bado ni kiongozi.
Hata hivyo kama kilichokusudiwa ni uongozi katika taasisi za umma, hakuna aya ya Qur'an inayokataza moja kwa moja wanawake kuwa viongozi bila kujali kiwango cha nafasi hiyo ya uongozi au umbile Ia nafasi hiyo. Iwapo kutakuwepo na ulazima, na iwapo uongozi wa mwanamke hautakiuka vipengele vingine vya Sheria ya Kiislamu, basi mwanamke anaweza kuwa kiongozi.
Ngazi pekee ya uongozi ambayo Uislam haumruhusu mwanamke kuishika ni ile ya ukuu wa nchi. Hata hivyo kwa kutumia kanuni ya qiyas baadhi ya wanazuoni wanasema mwanamke pia asiwe Kamanda wa Majeshi.
Kwa nini mwanamke haruhusiwi kuwa mkuu wa nchi?
Katika Qur'an hakuna aya inayowakataza wanawake kuwa viongozi. Lakini katika Hadith Sahihi iliyosimuliwa na Bukhari, Muslim, At-Tirmidhy, An-Nasai na wengineo Mtume (s.a.w) alipoambiwa kuwa Waajemi walikuwa wakifanya mabinti za Wafalme wao waliofariki kuwa viongozi wao, alisema: "Watu hawataendelea, hawatafanikiwa katika mambo yao ikiwa watawachagua wanawake kuwa viongozi wao wa nchi."
Hikma ya kuzuiliwa wanawake kuwa viongozi wa nchi ni kuwa katika Uislam mkuu wa nchi si nafasi ya hadhi tu (ceremonial or figure head) bali ni cheo chenye majukumu mengi mazito. Mkuu wa nchi ndiye imamu wa sala za jamaa misikitini. Anatakiwa pia aliongoze jeshi vitani. Kama tulivyoona huko nyuma mwanamke hawezi kuwa imamu wa swala zenye mchanganyiko wa wanaume na wanawake. Na kwa kawaida wanawake wasingependa kuwa makamanda wa majeshi hata wale wanawake wanaodai wafanye kila kazi inayofanywa na wanaume. Na kwa hakika ikifikia katika jamii wanawake wakapenda kuongoza vita, kufanya mipango na kushiriki katika kumwanga damu za watu, basi wakati huo maisha yatapoteza uzuri wake, uzuri unaotokana na moyo wa huruma na mapenzi walionayo wanawake. Uwiano mzuri wa maisha utaondoka iwapo wanawake nao watakuwa na mioyo migumu isiyosita kumwaga damu.
Jambo jingine Ia kuzingatia ni kuwa katika Uislam urahisi Si cheo cha kukigombea bali ni jukumu zito Ia kukimbiwa. Hii ni kwa sababu kiongozi wa nchi anatakiwa asiishi maisha yaliyo bora kuliko ya raia yoyote wa nchi yake. Matokeo yake ni kuwa hata kama mtu alikuwa na maisha mazuri ya anasa kabla ya kuwa kiongozi akipata uongozi anakuwa na maisha duni zaidi. Mtume (s.a.w) kabla ya utume alikuwa na maisha bora zaidi kiuchumi kuliko alipokuwa Mtume. Ingawa angetaka angeweza hata kuwa milionea kutokana na nafasi yake. Katika Hadith zilizokusanywa na An-Nawawi, Bibi Aisha (r.a) amesema mwezi mmoja au miwili ilipita bila kuwasha moto nyumbani mwao kwa sabau hakukuwa na cha kupika. Waliishi kwa tende na maji. Na hii ni pamoja na kuwa Mtume angeweza kuishi katika anasa. Hali ilikuwa ngumu hadi wakeze walianza kulalamika. Wakakemewa na Mwenyezi Mungu (33:2829). Na hali ilikuwa hivyo hivyo kwa Makhalifa waliofuatia. Hivyo uraisi Si cheo ambacho mtu atakigombea kwa hila, rushwa na kampeni za usiku na mchana.
Vyovyote itakavyokuwa katika Uislam mtu hajipendekezi yeye mwenyewe jina lake bali wenzake ndio wampendekeze. Suala Ia wanawake kuzuiliwa kuwa maraisi Si Ia msingi kwa sababu tangu hapo katika idadi ya sasa watu wapatao elfu nne milioni(Bilioni 6) waliopo duniani ni wanaume wangapi ni maraisi au wanaweza kuwa maraisi?
Je, wanawake wanaweza kuwa majaji?
Juu ya sualal hili wanazuoni wa Kiislam wamehitlafiana. Tunachoweza kufanya hapa ni kuzibainisha tu rai zao bila upendeleo.
Rai ya kwanza ni ile inayosema kuwa mwanamke hawezi kuwa jaji.
Hoja zao ni mbili: Ya kwanza ni kuwa mwanamke hawezi kuwa mkuu wa nchi basi hawezi pia kuwa jaji kwa sababu ujaji unaweza kulinganishwa na utawala. Jaji anafanya kazi za kiutawala. Hoja ya pili ni kuwa katika Uislamu, mume ndiye mkuu wa familia. Hivyo kama sheria haijampa mwanamke ukuu wa familia ambayo ni taasisi ndogo basi hawezi kupewa ujaji ambayo ni taasisi kubwa zaidi. Rai hii ndiyo inayofuatwa na wanazuoni walio wengi.
Rai ya pili ni ile inayosema kuwa mwanamke anaweza kuwa jaji.
Hii ndiyo rai ya mwanazuoni mashuhuri aitwayeAt-Tabari. Hoja yake ni kuwa kulinganisha ukuu wa nchi na ujaji si sahihi kwa sababu Hadith imebainisha wazi wazi kuwa walichozuiliwa ni ukuu wa nchi. Kulinganisha ukuu wa nchi na maeneo mengine Si sahihi.
Rai ya tatu ni ile iliyotolewa na Imam Abu Hanifa. Yeye anasema ikiwa mwanamke anaweza kuwa shahidi katika masuala ya fedha basi anaweza pia kuwa jaji katika masuala ya fedha. Hivyo ni dhahiri kuwa ukiondoa ukuu wa nchi, wanazuoni hawajaafikiana wote kwa kauli moja kama katika maeneo mengine wanawake wanaweza kuwa viongozi au Ia.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 554
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Madrasa kiganjani
Funga za Sunnah na umuhimu wake
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa. Soma Zaidi...
Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.
Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi. Soma Zaidi...
Aina ya talaka zisizo rejewa
2. Soma Zaidi...
Sanda ya mwanaume na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Ujuwe utaratibu mzima wa funga na kutekeleza ibada ya Swaumu
Soma Zaidi...
Haya ndio yanayobatilisha Hija
Soma Zaidi...
Funga ya ramadhan na nyinginezo
Nguzo za uislamu (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kwa nini imefaradhishwa kufunga katika Mwezi wa ramadhani?
Soma Zaidi...
Nguzo za kufunga ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
NAMNA YA KUCHINJA KATIKA UISLAMU
عَنْ أَبِي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "إنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِح... Soma Zaidi...
Nadharia ya uchumi wa kiislamu
Dhana ya uchumi wa kiislamu imejegwa jui ya ukati na kati. Dhana hii imetofautiana sana na dhana nyinginezo kama ubepari na ujamaa. Soma Zaidi...