image

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu

Chimbuko la Sheria za Kiislamu

i. Allah (s.w) kupitia Kitabu chake - Qur’an (na Vitabu vingine vilivyotangulia)

- Ndiyo chimbuko kuu la sheria za Kiislamu.

Rejea Qur’an (5:45-47), (59:23), (17:105)



ii. Sunnah (Hadith za Mtume (s.a.w))

- Ni msingi wa pili unaotokana na mwenendo wa Mtume (s.a.w) katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (53:2-4), (3:31-32), (33:21) na (59:7).

- Ndiyo chem chem kuu inayofasiri Qur’an kinadharia na kivitendo na ni

katika wahyi (ufunuo) pia.

Rejea Qur’an (53:3-4)



iii. Ijma’a.

- Maana yake ni Maafikiano ya wanachuoni (wanataaluma) wa Kiislamu katika kutoa hukumu juu ya jambo fulani lisilo na hukumu ndani ya Qur’an au Hadith kwa kupitia misingi ya Qur’an au Sunnah (Hadith).


- Ijmaa inakubalika tu isipopingana au kwenda kinyume na aya ya Qur’an

au Hadith za Mtume (s.a.w)

Rejea Qur’an (3:159), (4:59), (42:38)



iv. Qiyaas.

- Maana yake ni kuyapatia hukumu mambo yasiyo na hukumu ya moja kwa moja katika Qur’an na Sunnah kupitia misingi sahihi ya sheria, hukumu na kanuni zilizopo katika Qur’an na Sunnah.




? Halali na haramu katika Sheria ya Kiislamu

Viwango vya halali na haramu ya mambo mbali mbali katika Uislamu viko vitano;

i. Faradh

- Ni mambo yote halali yaliyolazima na wajibu kutekelezwa na watu.

Mfano; swala, zakat, funga, n.k ii. Mustahabu
- Ni mambo ambayo ni halali yaliyohimizwa kutekelezwa katika jamii.

Mfano; siasa, uchumi, utamaduni, n.k iii. Mubaha (permissible)
- Ni jambo ambalo ni halali na ni ruhusa kulifanya ila si wajibu (si lazima).

Mfano; kujenga nyumba nzuri, kuwa na kipando, n.k iv. Makruhu (Detestable)

- Ni jambo ambalo haliharamishwa moja kwa moja lakini lina madhara. v. Haramu
- Ni mambo yote yanayokiuka maamrisho ya Allah (s.w) na Mtume wake

(s.a.w).



Aina za Makosa na Adhabu Zake Katika Sheria ya Kiislamu

a) Makosa ya Hudud

- Ni yale makosa ambayo hukumu na adhabu zake zimetajwa katika Qur’an

au Hadith za Mtume (s.a.w).



- Mfano wa makosa na adhabu (hukumu) hizo ni;

Kuritadi (ridda) - ,hukumu yake ni kuuliwa. Qur’an (9:5).

Uasi (baghi) – ni kupigana kama wamekataa suluhu. Qur’an (49:9)

Wizi – ni kukatwa mkono wa kulia baada ya kutimizwa sharti kadhaa.

Qur’an (5:38)

Zinaa – hukumu yake ni kupigwa fimbo 100 hadharani. Qur’an (24:2) Ulevi – ni kupigwa viboko 80 kwa mujibu wa Hadith za Mtume (s.a.w). Qur’an (5:90)


b) Makosa ya Qisas

- Ni makosa yanayotokana na kudhulumu haki ya mtu.

- Hukumu yake ni kulipiza kisasi kwa kumfanyia kama alivyokufanyia.

Rejea Qur’an (2:178), (5:45)



c) Makosa ya Ta’azir

- Ni makosa ambayo hukumu au adhabu yake haija tajwa moja kwa moja katika Qur’an au Hadith za Mtume (s.a.w).
- Hukumu na adhabu yake hutolewa na Jaji au hakimu kwa idhini ya kiongozi wa Kiislamu kulingana na kosa na mazingira.



Haki za Wasiokuwa Waislamu Katika Dola ya Kiislamu

Sheria ya Kiislamu inawapa haki wasiokuwa waislamu kama ifuatavyo;

i. Haki ya ulinzi wa mali na maisha yao.

- Ni haramu kumwaga damu ya asiyekuwa muislamu bila sababu ya msingi.



ii. Haki katika sheria ya jinai

- Makosa yote ya jinai (penal laws) adhabu zake ni sawa kwa waislamu na wasiokuwa waislamu pia.


iii. Haki katika sheria ya madai (civil laws)

- Hukumu na adhabu za madai ni sawa sawa kwa waislamu na wasiokuwa waislamu.


iv. Haki ya heshima

- Ni kosa na haifai kumvunjia heshima, kumdhulumu, n.k asiyekuwa muislamu kama ilivyo kwa muislamu.


v. Haki katika sheria ya mtu binafsi

- Sheria ya Kiislamu inahukumu mambo yote ya mtu binafsi kulingana na imani ya dini yake.





                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 936


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu
Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mambo yenye kufunguza swaumu (funga)
Soma Zaidi...

Nguzo za uislamu:Shahada
Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Aina ya talaka zisizo rejewa
2. Soma Zaidi...

Umuhimu wa uchumi katika uislamu
2. Soma Zaidi...

Jinsi uislamu ulivyokomesha biashara ya utumwa wakati na baada ya mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

Watu wanaowajibikiwa kuhiji
Soma Zaidi...

Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

haya ndiyo mambo yanayaribu swala na yanayobatilisha swala
Soma Zaidi...

jamii
Soma Zaidi...

Ni upi umuhimu wa kufunga katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kufunga kiroho, kiafya na kijamii. Soma Zaidi...

Sanda ya mtoto
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...