Navigation Menu



image

Mtazamo wa uislamu juu ya ndoa ya mke zaidi ya mmoja

Je jamii inachukuliaje swala la kuoa mke zaidi ya mmoja.

Ndoa ya mke mmoja hadi wanne

 


Suala Ia ndoa ya mke zaidi ya mmoja ni suala Iinalopingwa na baadhi ya watu hasa wale wanaodai kuwa ni watetezi wa haki za wanawake. Mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja imeonekana kwa wapinzani wa ukewenza kuwa ni jambo lililopitwa na wakati na linalomdunisha mwanamke na kumnyima haki zake. Dai hili linatokana na hali halisi iliyodhihiri katika jamii mbali mbali za kikafiri za kale na za sasa ambapo mwanamke ananyanyaswa na kudhalilishwa kweli kweli. Ni katika hali hii ya kudhalilishwa mwanamke, ndipo wakatokea wanaojiita watetezi wa haki za wanawake na wakawashawishi wanawake wajiunge pamoja na kudai kupata haki zao sawa na wanaume.

 


Mpaka sasa mafanikio yaliyopatikana katika harakati hizi za kumkomboa mwanamke ni wanawake kufanya kila kazi zinazofanywa na wanaume, kuvaa sawa na wanaume, kuwa huru kuchanganyika na wanaume, kushindana na wanaume katika nyanja za siasa na uchumi, mume mmoja mke mmoja na kadhalika.

 


Watetezi wa Haki za wanawake wa mtazamo huu, wanapoukuta Uislamu umeruhusu kuoa wake wengi, mmoja hadi wane, hurejea historia na hujisaili, Tumejifunza vya kutosha katika historia kuwa wanaume wamewafanya wanawake mashine zao za kuwafanyia kazi na kuwazalia watoto na kila mwanamume alipooa wake wengi na kuwaweka chini ya himaya yake, ndivyo mwanamke alivyozidi kumnyimwa haki zake na kudhalilishwa, iweje tena leo turuhusu jambo hili liendelee? Hili linapingana kabisa na juhudi zetu katika kumkomboa mwanamke!

 


Fikra hizi zina ukweli mkubwa ndani yake, lakini kasoro yake kubwa ni kule kuulinganisha Uislamu na jamii nyingine. Jamii ya Kiislamu ni jamii iliyoundwa kwa misingi iliyowekwa na Mwenyezi Mungu ambaye ni Muumba, Mjuzi mwenye Hekima aliye Muumba mwanaadamu kwa lengo na kumuwekea utaratibu madhubuti wa maisha utakao muwezesha kufikia lengo na kuishi hapa ulimwenguni kwa furaha na amani. Uislamu kupitia kwa Mitume na vitabu vya Allah (s.w)umekusudiwa usimamishe uadilifu katika ardhi:

 

Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu na dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na uadilfu pamoja nao, iii watu wasimamie uadilfu.(57:25)
Katika sheria ya Kiislamu kuoa wake zaidi ya mmoja hadi wane ni jambo lililoruhusiwa na Allah (s.w). Aya ya Qur-an iliyo ruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja hadi wane ilishuka mara tu baada ya vita vya uhudi - vita vya pili vya Jihadi kwa umma huu wa Mtume (s.a.w) - ambapo Waislamu wengi wapatao sabini walikufa shahidi na kuacha wake wengi wajane na watoto yatima kama tunavyojifunza katika aya:

 

Na kama mkiogopa kutowafanyia uadilfu mayatima, basi oeni mnaowapenda katika wanawake wawili, au watatu au wanne. Na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilfu, basi oeni mmoja tu, au (wawekeni masuria) wale ambao mikono yenu ya kuume imewamiliki. Kufanya hivyo ndiko kutakupelekeni kutofanyajeuri. (4:3).
Aya hii inatupa mafundisho yafuatayo:

 


Kwanza, ukewenza ni ruhusa kutoka kwa Allah (s.w) hivyo wanaume wema na wanawake wema wa Kiislamu hawanabudi kuipokea ruhusa hii kwa lengo Ia kumcha Allah (s.w).

 


Pili, ruhusa hii haikutolewa kwa ajili tu ya kukidhi matamanio ya kimwili bali ruhusa hii imeshuka ili kuwaruhusu wanaume wema wa Kiislamu wawaoe wajane au wanawake wema wanaohitajia nusura na kuepusha wanawake wema kuolewa na wanaume waovu au kukaa bila ya kuolewa jambo ambalo ni mtihani kwa jamii.

 


Tatu, pamoja na kuoa kwa nia hiyo njema ya kuwapatia hifadhi wajane, mayatima na wanawake wema wenye kuhitajia hifadhi ya waume wema wachache waliopo ruhusa hii haikuachwa wazi kwa kuruhusu wanaume kuoa wake wengi wapendavyo kama ilivyokuwa wakati wa Ujahili, bali imetoa ruhusa ya wanawake wane tu.

 


Nne, endapo mwanaume hatakuwa na uwezo wa kukidhi matamanio ya jimai kwa wake zake wote au hatakuwa muadilifu kwa wake zake wote, basi sheria hii inamnyima ruhusa hii ya kuoa mke zaidi ya mmoja.

 


Tano, Aya inaagiza: Fankihu yaani Oeni wala sio Chukueni Hivyo, katika kutumia ruhusa hii ya kuoa mke wa pili hadi wanne, ni lazima kuoa kwa kufuata utaratibu na kuchunga masharti yote ya ndoa ya Kiislamu. Kwa mfano hatalazimishwa mwanamume kuoa mke wa pili na wala hatalazimishwa mwanamke kuolewa na mume aliyekwisha oa.

 


Mume anayekusudia kuoa mke wa pili au zaidi, kiuadilifu na kiucha-Mungu hanabudi kumtaarifu au kuwataarifu wake zake wa kwanza. Mkewe au wakeze, kwa upande wao, hawanabudi kumridhia aoe huku wakimshauri na kumuusia kuwa azingatie sharti Ia uadilifu lililowekwa katika kutolewa kwa ruhusa hii.

 


Ni muhimu kuzingatia kuwa ruhusa ya ukewenza imetolewa na mwenyewe Allah (s.w) ambaye ni Mjuzi mwenye Hikima, hivyo hapana nafasi ya mjadala kuwa inafaa au haifai. Hata hivyo kwa kuzingatia hali halisi ya jamii, bado hekima ya ruhusa hii iko bayana.

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1690


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Namna ya kutambuwa kibla na umuhimu wa kuelekea kibla wakati wa kuswali
4. Soma Zaidi...

Ni mambo gani yanaharibu na kutengua udhu?
Soma Zaidi...

Taratibu za kuchaguwa mchumba katika uislamu
Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

Vipi funga yaani swaumu itapelekea uchamungu na kutekeleza lengo
Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu. Soma Zaidi...

Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hizi ndio suna za swala kwa swala za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Hili ndio lengo la kufunga.
Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga. Soma Zaidi...

Wanaostahiki kupewa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini?
Assalamu Alaykum Warahmatu-llah Wabarakaatuh Naomba kuuliza: Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini? Soma Zaidi...

haki na wajibu kwa wakubwa
Soma Zaidi...

MAFUNZO YA SWALA: NGUZO ZA SWALA, SHARTI ZA SWASL, FADHILA ZA SWALA, HUKUMU YA MWENYE KUACHA SWALA
Soma Zaidi...

sadaka
Soma Zaidi...