image

Historia ya Dhana ya Kudhibiti Uzazi

Historia ya Dhana ya Kudhibiti Uzazi

4.2 Historia ya Dhana ya Kudhibiti Uzazi

Kampeni za Kikafiri juu ya kudhitibiti Uzazi na Madhara yake

- Ni mpango wa kuzuia mimba uliobuniwa na Margaret Sanger kutoka Marekani mwaka 1913 uliohusika na kuzuia, kutoa mimba, kupunguza na kuzaa kwa hiari.


- Kampeni hizi zilibuniwa kwa majina kama; elimu ya ngono, uzazi wa malezi bora, mpango wa familia, n.k.
Sababu za Kustawi Kampeni za Kudhibiti Uzazi

i. Kuwa huru ili kufanya kazi kwa ufanisi (Mapinduzi ya) Viwanda Ulaya

- Wafanyakazi wengi walishindwa kumudu familia zao kimahitaji kutokana na mabadiliko ya mahitajio viwandani.


ii. Kupunguza idadi ya watu kwa uchoyo wa kutumia rasilimali kwa wachache

(Mishahara midogo ya Wafanyakazi)

- Kutokana na pato dogo, wanawake waliamua kupunguza kuzaa ili kumudu mahitaji ya kulea.


iii. Mapinduzi ya Utamaduni na maadili

- Ili kuishi maisha ya anasa kwa mtu binafsi au familia, wanawake walijiepusha kuzaa sana ili kufikia lengo lao hilo.


iv. Kuepuka jukumu la kulea familia na Kuporomoka kwa Maadili

- Kusambaratika na kuvunjika kwa ndoa, wanandoa na familia, wanawake walikuwa huru kufanya atakalo kama uzinzi, kutoa na kuzuia mimba, n.k


v. Kuwa huru katika kufanya ngono na starehe bila kuwajibishwa kulea

- Wanawake wengi waliona njia pekee ya kustarehe kimwili na kuepuka jukumu la kuzaa na kulea mpaka atakapotaka kuzaa ni kudhibiti uzazi.Hoja za Kikafiri juu ya Kudhibiti Uzazi Hivi Leo na Udhaifu Wake

Kampeni za kudhibiti uzazi leo hii zinaendeshwa kwa hoja ya idadi ya watu kuwianisha na uchumi wao kama ifuatavyo;
i. Hoja kuwa ‘watu wengi hawana elimu, hivyo hawana manufaa kiuzalishaji’Udhaifu wa hoja hii;

- Hakuna uhakika wowote kuwa wachache unaowalea ndio watakuwa bora au vipi kiuzalishaji, kwani ubora wa mtu ni utu wake na sio vitu au anasa.


ii. Hoja ya hali duni kimaisha Afrika ambapo watu wengi hawafii utu uzima kutokana na maradhi na vifo.


Udhaifu wa hoja hii;

- Ukweli ni kuwa uhai, maradhi na vifo viko mikononi mwa Allah (s.w), hivyo maisha duni au kuugua sio sababu ya msingi.


- Vifo vingi hutokana na mafuriko, vimbunga, tetemeko, n.k ambavyo ni nje ya uwezo wa mwanaadamu.

iii. Hoja ya Uhaba wa Rasilimali za KiuchumiUdhaifu wa hoja hii;

- Hoja ya kuwa uchumi utakuwa chini kulingana na idadi ya watu si kweli, kwani watu ndio nyenzo ya kuboresha uchumi wao kama watatumika vizuri.


- Hoja kuwa mahitaji hayatoshi si kweli kwani rasilimali zilikuwepo tangu dunia kuumbwa, kuongezeka watu huongeza na kuboresha maarifa zaidi.


- Hoja kuwa kuna viumbe wasipodhibitiwa idadi wataijaza dunia kwa kuzaana, si kweli kwani tatizo sio kujaza dunia ila ni ugawaji mbaya wa rasilimali.

iv. Hoja ya Ugumu wa MaleziUdhaifu wa hoja hii;

- Hoja kuwa wazazi watashindwa kulea na kuwapa mahitaji watoto wao ni dhaifu kwani kumlea mtoto kianasa ni kumpotezea ushujaa wake baadaye.


v. Hoja ya kuwa, ‘kuzaa kunadhoofisha afya ya mama’Udhaifu wa hoja hii;

- Njia wanazotumia wanawake kuzuia mimba ni hatari na zina madhara zaidi kwa afya ya mama.


Matokeo, Madhara na Athari ya Kudhibiti Uzazi

i. Uhaba wa Wafanyakazi

- Kutokana na udhibiti wa uzazi, rasilimali watu kwa ajili ya uzalishaji ilipungua kwa nchi kama; Ufaransa, n.k


ii. Tishio la Kuporomoka kwa nguvu kazi ya taifa

- Udhibiti wa uzazi ulipelekea kupungua nguvu kazi na uchumi wa taifa pia.iii. Kuporomoka kwa Maadili ya Jamii

- Kukosekana nafasi ya ndoa na malezi katika jamii ndio chanzo cha uzinzi na kila aina ya uovu na uchafu nchi kama Sweden na Amerika.


iv. Kushindikana kutokomeza zinaa na magonjwa yatokanayo na zinaa

- Kustawi kwa starehe na uhuru wa ngono kwa mtu yeyote, kulipelekea kuenea zaidi magonjwa ya zinaa kama vile “UKIMWI” n.k.


v. Kukosekana kizazi kijacho chenye misingi ya maadili na malezi

- Kudhibiti uzazi kulipelekea kukosa kizazi kipya kilichojengenga katika maadili mazuri.

Kumbuka: Ili hoja ya kudhibiti uzazi ikubalike ni sharti yajulikane mambo yafuatayo;

- Idadi ya viumbe vyote wanaoishi na watakaoishi.

- Idadi ya kuongezeka au kupungua kwa chakula duniani.

- Idadi ya viumbe watakaokufa kwa njaa, maradhi, n.k ili kuwianisha na chakula.
- Idadi ya watu wanaoishi na kufa ili kulinganisha na rasilimali zilizopo.Madhara ya Zinaa Katika Jamii

i. Kudhoofika kwa afya na kuweza kueneza magonjwa ya zinaa kama vile; Kisonono, Kaswende, UKIMWI, n.k kwa vizazi vijavyo.


ii. Uzinzi hupelekea kupotea utu wa mtu na kuwa na tabia ya ujambazi, wizi, ulevi, uongo, ulaghai, ubinafsi, kukosa aibu, nidhamu, n.k.

iii. Zinaa husababisha wasichana kujihusisha na ukahaba na kupoteza utu, heshima, thamani na uzuri wao katika jamii.


iv. Zinaa hupelekea kuvunjika na kukosekana nafasi, umuhimu na heshima ya ndoa katika jamii, kila mtu atajimai na yeyote kwa lengo la starehe tu.

v. Zinaa huangamiza umma na kizazi cha mwanaadamu ambapo kila mmoja ataepuka dhamana ya kuzaa na kulea watoto.

vi. Uzinzi pia husababisha kuzaliwa watoto nje ya ndoa ambao hukosa malezi na maadili bora na hivyo kuzama katika dimbwi la ufuska wa zinaa.

vii. Zinaa huharibu maisha ya mwanamke kwa kukosa hifadhi, mapenzi na matunzo ya kweli ya kindoa.

viii. Zinaa husababisha kuporomoka kwa uchumi wa mtu binafsi, familia na nguvu kazi ya taifa kwa ujumla.                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 263


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII SULEIMAN
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU
Soma Zaidi...

NAMNA MTUME(S.A.W) ALIVYOSIMAMISHA DOLA YA KIISLAMU MADINAH
Safari ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)
8. Soma Zaidi...

Miujiza Kama Ushahidi wa Utume wa Nabii Musa(a.s)
Allah(s. Soma Zaidi...

Sababu za makafiri wa kiqureish kuupinga ujumbe wa uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Historia ya Al-Khidhri
Jina Al-Khidhri halikutajwa mahali popote katika Qur’an. Soma Zaidi...

Ijuwe Dua ya Ayyuub(a.s)
Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII ISA
Soma Zaidi...

Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)
(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a. Soma Zaidi...

Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam
Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam. Soma Zaidi...