Njia za Biashara Haramu Katika Uislamu
Miongoni mwa biashara zilizoharamu hata kama zimetokana na bidhaa halali ni;
i. Muzabanah
- Ni kunufaika kibiashara kutokana na matatizo ya watu (muuzaji na mnunuzi).
ii. Mu’awamah
- Ni uuzaji au ununuzi wa matunda au mazao shambani kabla ya kukomaa kwake na kufaa kuliwa.
iii. Hablul-Habalah
- Ni kuuza au kununua kilichoko tumboni mwa mnyama kabla hakijazaliwa.
iv. Kuuza au kununua bidhaa kabla haijafika sokoni.
Ibn Abbas (r.a) ameeleza:
“Katika mauzo aliyoyaharamisha Mtume (s.a.w) ni mauzo ya chakula mpaka
yawe mikononi mwa mnunuzi…” (Bukhari na Muslim)
v. Kuuza au kununua bidhaa iliyouzwa au kununuliwa tayari na mtu mwingine kwa kuongeza bei au namna nyingineyo.
vi. Kuuza maji au majani asili yasiyogharamiwa kwa chochote.
Jaabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza kuuza maji ya asili.
(Muslim)
vii. Kuuza au kununua samaki walioko baharini, ndege asiyefugwa (anayeruka angani), maziwa yangali hayajakamuliwa, kiumbe kilicho tumboni mwa mnyama, n.k.
viii. Kuuza au kununua damu, uhuru wa mtu, nywele au maziwa ya binaadamu, n.k.
ix. Kuuza au kununua mbwa, nguruwe, pombe, mizoga, masanamu, picha za watu au wanyama, n.k.
x. Ulanguzi (kuhodhi bidhaa) au kuifanya bidhaa iwe adimu sokoni ili baadae uuze kwa bei yak juu unayotaka.
xi. Kuuza au kununua kwa kupunja au kuharibu vipimo.
“Maangamizo yatawathubutikia wapunjao (wenzao vipimo)……….” (83:1-3)
xii. Kuuza kwa kuficha dosari ya bidhaa, n.k.
xiii. Kuuza au kununua bidhaa kwa wizi, hongo, rushwa, riba, n.k.
Rejea Qur’an (2:276-279)
xiv. Aina zote za kamari kama ramli, kupiga bao, utabiri, n.k.
Rejea Qur’an (5:90-91)
xv. Aina zote za miziki, ngoma, n.k.
Bidhaa Haramu Katika Uislamu
Miongoni mwa bidhaa haramu hata kama biashara yake itafanywa kihalali ni;
i. Pombe za aina zote ii. Mizoga, damu, n.k
iii. Mbwa, nguruwe, paka, n.k
iv. Masanamu, picha za watu au wanyama, n.k v. Bidhaa ya wizi, n.k.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala.
Soma Zaidi...Katika uislamu hakuna sheria ya mwanamke kuingizwa eda na kutolewa eda kama ilivyozoeleka. Endelea na post hii ujifunze zaidi
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria. Pia utajifunza umuhimu wake
Soma Zaidi...Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukufundisha kuhusi swala ya tarawehe, faida zake na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...- Je, Ukeweza, (ndoa ya mke zaidi ya mmoja) humdhalilisha mwanamke?
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?
Soma Zaidi...