Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria. Pia utajifunza umuhimu wake
TWAHARA NA UMUHIMU WAKE
Maana Ya Twahara Katika Lugha Ya Kawaida:
Ni usafi na kuondosha uchafu au takataka za kihisia (kugusika) kama najsi ya mkojo au kinginecho, na za kidhahania kama kasoro (mapungufu) na maasi.
Kutwaharisha ni kusafisha, nako ni kupaweka mahala maalumu katika hali ya usafi. [Al-Libaab Sharhul Kitaab (1/10) na Ad-Durru Al-Mukhtaar (1/79)].
Ama kisharia (kitaaluma):
Ni kuondosha kinachozuia kuswali kama hadathi au najsi kwa kutumia maji (au kinginecho), au kuondosha hukmu yake kwa mchanga. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (1/12)].
Hukmu ya twahara:
Kutwaharisha najsi na kuiondosha ni jambo la wajibu ikiwa mtu atakumbuka na ataweza. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:
((ÙˆÙŽØ«Ùيَابَكَ ÙÙŽØ·ÙŽÙ‡Ù‘ÙØ±))
((Na nguo zako zitwaharishe)) [Al-Muddath-thir (74:4)]
Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala):
((Ø£ÙŽÙ† Ø·ÙŽÙ‡Ù‘ÙØ±ÙŽØ§ بَيْتÙÙŠÙŽ Ù„ÙلطَّائÙÙÙينَ وَالْعَاكÙÙÙينَ وَالرّÙÙƒÙ‘ÙŽØ¹Ù Ø§Ù„Ø³Ù‘ÙØ¬ÙودÙ))
((Ya kwamba itakaseni Nyumba Yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu na wanaojitenga humo kwa ‘ibaadah, na wanaoinama na kusujudu)). [Al Baqarah (2:125)]
Ama kujitwaharisha na hadathi, hilo ni lazima ili ruhusa ya kuswali ipatikane kwa neno lake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
(( لَا تÙقْبَل٠صَلَاة٠بغير طهور))
((Swalaah haikubaliwi bila ya wudhuu). [Swahiyh Muslim 224]
Umuhimu Wake:
1- Twahara ni sharti ya kusihi kwa sala ya mja. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((لَا تÙقْبَل٠صَلَاة٠مَنْ Ø£ÙŽØÙ’دَثَ ØÙŽØªÙ‘ÙŽÙ‰ يَتَوَضَّأَ ))
((Haikubaliwi Swalaah ya mtu mwenye hadathi mpaka atawadhe)). [Imepasishwa na Al Bukhaariy (135), Muslim (225].
Kuswali na twahara ni kumtukuza Allaah. Na hadathi na janaba – ingawa si najsi zenye kuonekana – lakini hata hivyo ni najsi za kidhahania zenye kukifanya kilichoingiwa navyo kuonekana kichafu. Hivyo basi, kuwepo kwake huteteresha utukuzo kwa Allaah, na huenda kinyume na msingi wa usafi.
2- Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Amewasifu wenye kujitwaharisha. Anasema:
((Ø¥Ùنَّ اللّهَ ÙŠÙØÙØ¨Ù‘٠التَّوَّابÙينَ ÙˆÙŽÙŠÙØÙØ¨Ù‘Ù Ø§Ù„Ù’Ù…ÙØªÙŽØ·ÙŽÙ‡Ù‘ÙØ±Ùينَ))
((Hakika Allaah Anawapenda wenye kutubia mara kwa mara na Anawapenda wenye kujitwaharisha)). [Al Baqarah 2:222]
Akawasifu watu wa Masjid Qubaa kwa Neno Lake:
((ÙÙÙŠÙ‡Ù Ø±ÙØ¬ÙŽØ§Ù„ÙŒ ÙŠÙØÙØ¨Ù‘Ùونَ Ø£ÙŽÙ† يَتَطَهَّرÙواْ ÙˆÙŽØ§Ù„Ù„Ù‘Ù‡Ù ÙŠÙØÙØ¨Ù‘Ù Ø§Ù„Ù’Ù…ÙØ·Ù‘ÙŽÙ‡Ù‘ÙØ±Ùينَ))
((Ndani yake kuna watu wanaopenda kujitwaharisha, na Allaah Anawapenda wenye kujitwaharisha)). [At Tawbah 9:108]
3- Kutojali au kutotilia maanani kujitakasa na najsi, ni moja kati ya sababu za kuadhibiwa watu makaburini. Imepokelewa na Ibn 'Abbaas akisema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita kwenye makaburi mawili akasema:
(( Ø¥ÙنَّهÙمَا Ù„ÙŽÙŠÙØ¹ÙŽØ°Ù‘َبَان٠وَمَا ÙŠÙØ¹ÙŽØ°Ù‘َبَان٠ÙÙÙŠ كَبÙÙŠØ±ÙØŒ أَمَّا هذا Ùَكَانَ لَا يَسْتَنزه Ù…Ùنْ بَوْلÙÙ‡ÙØŒ ))
((Kwa hakika wawili (hawa) wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. (la kuwashinda kutekeleza au kujiepusha nalo). Ama huyu, alikuwa hajitakasi na mkojo wake)). [Abu Daawuud (20), An Nasaaiy (31-69), na Ibn Maajah (347) kwa Sanad Swahiyh].
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakufundisha mambo ambayo yatasababisha swqla yako isikubaliwe.
Soma Zaidi...Kuchunga au kutekeleza ahadi ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli.
Soma Zaidi...Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala.
Soma Zaidi...