Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala.
Umuhimu wa Kusimamisha Swala
Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.a) tuliyoirejea mwanzoni, kusimamisha swala ni nguzo ya pili ya nguzo za Uislamu. Katika kuonyesha umuhimu wa kusimamisha nguzo hii Mtume (s.a.w) a me sem a:
“Sw ala ndio nguzo kubw a ya Dini (Uislamu) mwenye kusimamisha swala amesimamisha dini (Uislamu) na mwenye kuiacha swala amevunja Dini .” (Uislamu)”
Katika Hadithi nyingine, amesimulia Jabir (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Tofauti yetu sisi (Waislamu) na ukafiri ni kuacha swala”. (Muslim) Pia Mtume (s.a.w) amesema:
“Tofauti iliyopo kati yetu (Waislamu) na wengine (wasiokuw a Waislamu) ni swala ”. (Ahmad, Abu Daud, An-Nasai, Tirmidh)
Kutokana na hadithi hizi, tunajifunza kuwa mtu ambaye hasimamishi swala, hatakama anajiita Muislamu si Muislamu bali ni kafiri kama makafiri wengine. Anakuwa kafiri kwa sababu amekanusha amri ya Allah iliyowazi kama inavyobainika katika aya zifuatazo:
“Waambie waja wangu walioamini, wasimamishe swala. ”(14:31)
“... Basi simamisheni swala, kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyow ekewa nyakati makhsusi.” (4:1 03)
“Na waamrishe watu wako kuswali (kusimamisha swala) na uendelee mwenyewe kwa hayo...” (20:132).
Tukumbuke kuwa hawi Muumini yule anayekuwa na hiari katika kutekeleza amri ya Allah na Mtume wake kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo:
“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi”. (33:36)
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kufanya suluhu katika ndoa.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis
Soma Zaidi...Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani.
Soma Zaidi...Atika uislamu swala la kupanga uzazi linaruhusiwa endapo kutakuwa na sababu maalumu za kisheria.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwedna kujifunza jinsi ya kutwaharisha aina mbalimbali za najisi kwa mujibu wa mafundiso ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...