Kazi ya chanjo ya Surua

Kazi ya chanjo ya Surua

Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya Surua kwa watoto, ni Aina ya chanjo ambayo utolewa kwa watoto na kufanya kazi mbalimbali mwilini ambazo ni kumkinga mtoto asipatwe na magonjwa.

Kazi ya chanjo ya Surua.

1. Hii ni chanjo ambayo upewa na watoto Ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali kwenye mwili, chanjo hii huwa Iko kwenye mfumo wa poda na uweza kuchanganya Ili iweze kufanya kazi, na wakati wa poda kuchanganya na maji inabidi vyote vinapaswa kutoka kwenye sehemu kiwanda kimoja Ili kuepuka hali ya kuchanganya madawa ambayo yanaweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto kwa sababu mtoto mdogo anahitaji uangalizi wa hali ya juu.

 

2. Kama mtoto hasipopota chanjo hii anaweza kuwa na utapiamlo kwa sababu sura usababisha utapiamlo kwa mtoto na makuzi ya mtoto yanakuwa kwa shida kwa hiyo mtoto anakuwa dhaifu hali inayopelekea mtoto kupata magonjwa nyemelezi kama vile upungufu wa damu, kubanwa kifua, kushindwa kupumua hali hii ujitokeza kwa Sababu ya utapiamlo kwa hiyo watoto wanapaswa kupewa chanjo hii Ili waweze kuwa na afya nzuri na pia kuepuka utapiamlo kwa watoto.

 

3. Ugonjwa wa Surua usababisha ubongo wa Mtoto kuwa na matatizo ambapo mtoto anakuwa na matatizo katika kufikilia na hatimaye mtoto anakuwa na upungufu wa akili na anaweza hasieleweke katika jamii na hatimaye kupoteza taiga la kesho, kwa hiyo tunapaswa kuwapatia watoto wetu chanjo ya kuzuia Surua Ili kupunguza watu wasio na akili timamu kwenye jamii na watoto wajisikie vizuri kwenye jamii. Na wazazi wapewe elimu kuhusu kukosa kwa chanjo hiii kwa watoto

 

4. Pengine mtoto hasipopata chanjo hii ya kuzuia Surua anaweza kuwa  bubu au kiziwi na kusababisha madhara mengine ambayo hayakutarajiwa kwa sababu ya hali ya kutojali au kushindwa kumpatia mtoto chanjo akiwa bado mdogo kwa hiyo basi tunapaswa kutimiza wajibu katika kuwashughulikia watoto.

 

5. Pengine mtoto anaweza hasipate chanjo hii ya Surua kwa hiyo mtoto utamtambua kwa dalili zifuatazo kama vile joto la mwili kupanda Mara kwa mara, mtoto anaweza akawa na upele kwenye mwili mzima au sehemu nyingine za mwili, kikohozi ambacho hakikatiki, Macho ya mtoto kuwa mwekundu kwa mda wote, mtoto hasipopata huduma mapema kifo kinaweza kutokea kwa mtoto.kwa hiyo jamii nzima kwa ujumla wanapaswa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa watoto wanakata chanjo kwa Sababu magonjwa nyemelezi kwa watoto ni mengi mno.

 

6. Hii chanjo ya Surua inabidi mtoto apewa kwenye miezi tisa naa miezi ya Kumi na nane baada ya mtoto kuzaliwa, kwa hiyo dozi hii utolewa mara mbili tu yaani mwezi wa tisa baada ya kuzaliwa na mwezi wa Kumi na nane baada ya mtoto kuzaliwa kwa hiyo kila mzazi anapaswa kujua hilo na kulitendea kazi .kwa hiyo jamii yote inapaswa kutis maanani chanjo hii Ili kuondoa hali ya kuleta madhara kwenye jamii.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 2747

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 web hosting     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 ai web app     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Njia za kujikinga na kisukari

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujikinga na kisukari

Soma Zaidi...
Kazi za chanjo ya polio

Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo za polio na kazi zake,hii ni chanjo ambayo unazuia maambukizi ya Virusi vinavyosababisha polio.

Soma Zaidi...
Mambo yanayosababisha kupona kwa vidonda.

Posti hii inahusu mambo yanayochangia katika kupona kwa kidonda, ni mambo ambayo yapo kwa mgonjwa mwenyewe kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
Zijue faida za maji ya uvuguvugu.

Posti hii inahusu zaidi faida za maji ya uvuguvugu, hasa hasa maji haya ni vizuri kabisa kuyatumia hasa wakati wa asubuhi na pia wakati tumbo likiwa halina kitu, kwa hiyo zifuatazo ni faida za maji ya uvuguvugu.

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotibu Ugonjwa wa homa ya utu wa mgongo

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu homa ya uti wa mgongo, kwa kuwa ugonjwa huu mara nyingi uathiri sehemu za kwenye ubongo kuna madhara ambayo yanaweza kutokea endapo Ugonjwa huu haujatibiwa mapema.

Soma Zaidi...
Msaada kwa wenye tonsils

Posti hii inahusu zaidi msaada kwa wenye tonsils, kwa wale wenye tonsils wanapaswa kufanya yafuatayo ili kuweza kupambana na ugonjwa huu.

Soma Zaidi...