Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)

Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani.

Hasara za wivu na kutokuwa wazi.

1. Mama Lisa akiwa amepanic vibaya na wasiwasi mkubwa aliingia kwa mama lita akiwa anaita lita ,lita, yaani kwa nguvu sana na kuhamaki, ndipo mama lita akashutuka sana na kumuuliza Mama Lisa kinachoendelea, ndipo Mama Lisa akaangua kilio na kugala gala kwenye sakafu baadae mama lita aka mpoza na kumuuliza kinachoendelea ndipo akaeleza kila kitu akidai kwamba Lita anajua kila kitu kinachoendelea shule na hajatoa taarifa yoyote kwa Mama yake, ndipo lita akaitwa akaulizwa akajibu kwamba hajui kitu chochote na kudai kwamba Lisa huwa anasoma na hajui kinachoendelea.

 

 

 

 

 

2. Hapo mama Lisa akapoa akarudi kwake, kumbe Lisa alikuwa tayari yupo kwao na lita na alisikia kila kitu akamshukuru sana lita, basi mama yake Lisa alipotaka kwenda nyumbani naye Lisa akakimbia akawahi kabla mama yake hajafika nyumbani na akalala kitandani kama vile anaumwa, basi mama Lisa akaenda nyumbani akamkuta mwanae yuko kitandani analalamika kwamba akija kusoma kichwa kinauma ,na akifanikiwa kusoma kuna vitu vinakuwa vinapiga kelele kichwani mwake na akamwambia mama yake kwamba hali hii ilijitokeza mda kwa hiyo nilishindwa kukwambia kwani nilitaka usiumie mama yangu kipenzi.

 

 

 

 

3. Basi mama Lisa akafanana kama vile amechanganyikiwa na akatafuta cha kufanya ili kuweza kumwokoa mtoto wake ili aweze kusoma vizuri kabisa, kwa sababu mama Lisa alimzaa Lisa kwa mwanaume ambaye alikuwa na familia yake tayari kwa hiyo aliamua kumwambia baba yake, na baba yake alikuwa anampenda sana Lisa kwa sababu ndiye aliyekuwa msichana pekee na waliobaki walikuwa ni wavulana, kwa sababu baba yake na Lisa alikuwa hajamtambulisha Lisa kwa mke wake wa ndoa alitamani kumwambia ili aweze kumwokoa mtoto wake, lengo la baba lilikuwa na kuishi na Lisa kwa mda ili aweze kumsaidia.

 

 

 

 

 

4. Basi baba Lisa akatoa siku moja akamwambia mke wake waende mjini na watarudi jion, basi akampeleka mjini akamwambia achukue kila kitu anachokihitaji na yule mama akafurahi sana kusikia vile basi kama kawaida ya wanawake akabeba nguo,wigi na takataka zote kwa sababu baba Lisa alikuwa na hela kweli na aliweza kulipa kila kitu, na baada ya kumaliza shopping waliweka vitu kwenye gari na wakaenda kula na yule mama aliulizwa hoteli anayoipenda akapendekeza hoteli moja iliyoitwa Victoria hotel, wakaenda wakala na kusaza na yule mama alifurahi mno.

 

 

 

 

 

5. Basi walipokuwa wanakula na kunywa na kucheza, baba Lisa aliomba kitanda kusudi wapumzike kidogo ili baadae waende nyumbani basi wakapewa kitanda, na katika kupumzika baba Lisa akamwambia mkewe kwamba ana kitu cha kumwambia na anaomba akipokee na akimsaidia atampenda maisha yake yote na yule mama kwa sababu alikuwa na furaha akamwambia yuko tayari kumsaidia kwa hiyo akamwambia kwamba ana mtoto wa kike na ana matatizo anataka amlete kusudi aweze kumsaidia na baadae atarudi kwa mama yake, yule mama akasita kidogo ila kwa kuwa alikuwa ameahidi kumsaidia alikubali ila aliumia kuona mumewe ana mtoto wa kike na yeye hana na ndiyo iliyokuwa tamaa yake .

 

 

 

 

6. Basi yule mama akaanza kuhoji zaidi kama mme wake huwa anaenda kwa yule mama Lisa kwa sababu sehemu ilikuwa mbali hakuona ushaidi wowote ila baba Lisa alikuwa anaenda na kuhudumia alikuwa anamhudumia mtoto kama kawaida , ila mama yule akamwambia baba amlete yule mtoto ili wamsaidie haraka ila lengo la mama lilikuwa ni kujua mtoto yaani Lisa na mama yake wanaishi wapi, basi wanaume walivyo na akili alikwenda mwenyewe akamleta nyumbani kwake ila mama alikuwa anataka kujua wanaishi wapi, basi Lisa akaletwa pale akawa anapendwa sana na yule mama, akaanzishiwa tution akawa anasoma kama Kawaida na alipopelekwa shuleni kufanya mtihani akawa wa kwanza na baba yake akafurahi akataka kuishi naye ili atoke kwenye mazingira ya kwa mama lisa. ila yule mke wa ndoa kazi yake ni mwanasaikolojia ya watu waliohathariwa na mahusiano kwa hiyo akaanza kuhoji ili kujua tatizo ni lipi basi akapata uhakika kwamba shida ni yule mwalimu na akakaa kimya, lengo lake lilikuwa ni kuharibu kabisa maisha ya mtoto kwa hiyo akamshawishi mme wake wamrudishe mtoto kwa mama yake.

 

 

 

 

 

7. Basi yule mke wa ndoa akajifanya mwema akamsihii mmewe waende wote kwa mama Lisa badi yule mwanaume akakubali wakaenda wote wakamfungia mama Lisa zawadi nyingi pamoja na Lisa,kwa hiyo walipofika kwa mama Lisa na Lita alikuwepo alipomwona Lisa alichukia mno na kusema kwamba amerudi kuchukua nafasi yangu darasani na akasema nitamkomesha na atakuwa anafeli tu, subiri mama Lisa kusikia hivyo alichukia mno na akaanza kumchukia Lita.wale wageni walipoondoka mama yule akaomba number za simu za mama lita na mama Lisa na watu wote hapo akapewa na pia wakaondoka na mumewe na Jumatatu Lisa akarudi shule alifurahi sana kuonana na mpenzi wake na siku nzima hakwenda darasani na lita hakusema kitu nyumbani ila kumtunzia siri tu.

itaendelea baadae.

 

 

 

 

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jamvini Main: Burudani File: Download PDF Views 1052

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)

Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki.

Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)

Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI (sehemu ya sita)

Post inahusu zaidi hadithi ya NIMLAUMU NANI ambayo ni sehemu ya sita, katika kipengele hiki tunaenda kumwona msichana Amina anapambana na hatimaye anafunga ndoa ya kiserikali na Frank

Soma Zaidi...
Hadithi hii inahusu hasara za wivu na kutokuwa wazi

Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu, kwa sababu ya kuwepo kwa marafiki wasio waaminifu wanasababisha kuharibiana maisha bila kujua kwa sababu ya kuonekana wivu na kutokuwa wazi.

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme (sehemu ya nne)

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme sehemu ya nne ni pale bibi anawachanganya kwa maneno yake yaani mke wa kwanza anaambiwa aandae malkia na mke mdogo atafute njia za kufanya kijana wake kuwa mfalme.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)

Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha.

Soma Zaidi...
Usichofahamu kuhusu mazoezi

Posti hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo hufahamu kuhusu mazoezi,ni mambo ambayo utokea au no matokeo mazuri kwa watu wanaofanya sana mazoezi.

Soma Zaidi...
Mahusiano ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mahusiano yaliyotokea kati ya vijana wawili ila yanafika baadae mmoja akamsaliti mwenzake.

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, hapa tunaona Jackie anajibu barua ya Julius kwa kusema yafuatayo.

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara.

Soma Zaidi...