Mafunzo ya sura zilizochaguliwa

Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Mafunzo ya sura zilizochaguliwa.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Imeangamia mikono ya Abulahab naye amekwisha angamia.
  2. Haitamfaa mali yake wala alivyovichuma (watoto).
  3. (Atakapokufa) Ataingia moto wenye muwako (mkubwa kabisa).
  4. Na mkewe (ni) mchukuzi wa kuni (za fitina).  
  5. (Kana kwamba) Shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa (anayechukulia kuni za fitina).

 

 

      Mafunzo ya sura kwa ufupi.

  1. Binaadamu siku zote huamua kumkanusha Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kibri na jeuri. 
  2. Mali na watoto havina msaada wowote pindi inapokuja adhabu ya Mwenyezi Mungu (s.w).
  3. Watu waovu na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w) wana mwisho mbaya wa kuishia motoni.
  4. Maadui wa Uislamu na waislamu siku zote hawakati tamaa katika kuzuilia watu kuingia na kuufuata Uislamu.
  5. Uchochezi, fitina na uasi ni miongoni mwa makosa makubwa yenye kuangamiza. 


 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Itakapofika Nusura ya Mwenyezi Mungu na Kushinda.
  2. Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi.
  3. Basi (hapo) mtakase Mola wako pamoja na kumsifu na umuombe magh’fira (msamaha) hakika Yeye ndiye apokeaye toba.

   

          Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.

  1. Nusura na mafanikio hutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.
  2. Baada ya nusura na ushindi hatuna budi kumshukuru, kumtukuza na kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu (s.w) bila ya kujivuna.
  3. Katika kufanya juhudi, hatuna budi kuchunga na kutii ipasavyo maarisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
  4. Nusura na mafanikio ya kweli huja baada ya juhudi za dhati za kibinaadamu kufanyika na kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) vilivyo.
  5. Mafanikio ya kweli sio kujilimbikizia mali na anasa za dunia tu, bali ni kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo.  

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Sema: Enyi Makafiri.
  2. Siabudu mnachoabudu.
  3. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. 
  4. Wala sitaabudu mnachoabudu.
  5. Wala nyinyi hamtaabudu ninayemuabudu (mimi).
  6. Nyinyi mna dini yenu na mimi nina dini yangu.

 

                  Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.

  1. Dini ni utaratibu wowote ule wa maisha anaoufuata mtu.
  2. Kuna dini nyingi hapa Ulimwenguni, Ukafiri nao ni dini.
  3. Hakuna uwezekano wa mwanaadamu kufuata dini (utaratibu wa maisha) za ya moja kwa wakati moja, Uislamu na mifumo mingine.
  4. Waislamu wa kweli ni wale wasiochanganya haki na batili kwa kuwahofia makafiri.
  5. Ni wajibu kuitangaza haki kwa wengine bila kuhofia chuki na uadui wao dhidi ujumbe uliowapa.


 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Hakika tumekupa kheri nyingi.
  2. Basi swali kwa ajili ya Mola wako na uchinje (kwa ajili yake pia).
  3. Hakika adui yako ndiye atakayekuwa mkiwa (atakatikiwa na kila kheri).

 

Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.

  1. Mafanikio hayapimwi kwa wingi wa mali na watoto, bali ni kuridhiwa na Mwenyezi Mungu (s.w).
  2. Hakuna neema kubwa kama kujaaliwa kuupokea Uislamu, kuuelewa, kuufuata vilivyo na kuufikisha kwa wengine.
  3. Hatuna budi kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake ipasavyo na kufanya kila jambo kwa ajili yake tu.
  4. Maadui na Wapinzani wa Uislamu ndiyo wenye kupata khasara na kufedheheka duniani na Akhera pia.
  5. Ushindi na mafanikio hupatikana kwa waislamu baada ya kutii na kufuata maamrisho ya Uislamu vilivyo.

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Je, Unajua yule anayekadhibisha dini (asiyeamini malipo ya Akhera)?
  2. Huyu ni yule anayemnyanyasa yatima.
  3. Wala hajihimizi (yeye wala wengine katika) kuwalisha maskini.
  4. Basi adhabu kali itawathubutikia wanaoswali.
  5. Ambao wanapuuza (maamrisho ya) swala zao.
  6. Ambao hufanya riyaa (ya kujionyesha kwa watu).
  7. Nao hunyima misaada (midogomidogo kwa wanaohitajia). 



 

Mafunzo ya Sura kwa Ufupi.

  1. Imani katika Uislamu hudhihirishwa katika matendo ya mtu na sio kauli au maneno tu.
  2. Kuwadhulumu, kuwasimanga au kuwatendea uovu wowote mayatima na wenye shida ni katika makosa makubwa.
  3. Swala ni lazima itekelezwe kwa kuzingatia ipasavyo nguzo, sharti zake pamoja na khushui (unyenyekevu).
  4. Kutenda jambo lolote kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu (s.w) ndio uhai wa ibada ya muumini.
  5. Maisha ni jambo la kijamii ambalo linahitajia watu kuishi pamoja kwa kusaidiana inapobidi.
  6. Muumini wa kweli ni yule aliyemwepesi kutoa misaada kwa wanaadamu wenzie na mwenye kujali matatizo ya wengine yanapowapata.

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Ili kuwafanya Maqureish waendelee.
  2. Waendelee na safari zao za wakati wa kusi (kwenda Yemen) na wakati wa kaskazi (kwenda Sham ndiyo maana tukajaalia jeshi la ndovu kushindwa).
  3. Basi na wa muabudu Bwana wa Nyumba hii (Al-Kaaba).
  4. Ambaye amewalisha (wakati wa) katika njaa na anawapa amani (wakati wa) katika khofu.

 

Mafunzo kwa Ufupi.

  1. Kwa hakika anayelisha na kulinda ni Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake.
  2. Amani, Usalama na Ustawi wa kweli wa jamii hutokana na kushikamana na amri za Mwenyezi Mungu (s.w).
  3. Shukrani za kweli kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni kumuabudu ipasavyo.
  4. Maingiliano ya Mataifa kibiashara ni katika neema za Mwenyezi Mungu (s.w).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 2151

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 Dua za Mitume na Manabii    πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰5 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)

LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam).

Soma Zaidi...
Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo

Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.

Soma Zaidi...
Msonge wa uongozi na siasa katika serikali ya kiislamu mafinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kuzaliwa kwa Mtume S.A.W

Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w, sehemu ya 5. Hapa utajifunza kuhusu kuzaliwa kwa Mtume.

Soma Zaidi...
Historia ya Dhulqarnain

Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: β€œMwenye Pembe Mbili”.

Soma Zaidi...
HISTORIA YA BANI ISRAIL

Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.

Soma Zaidi...