Nabii Ibrahim(a.
Nabii Ibrahim(a.s), baada ya kupingwa mawe na kufukuzwa na baba yake mzazi, hakukata tamaa bali aliamua kuikabili jamii na kuifikishia ujumbe wa Uislamu kwa hekima kwa kutumia hoja madhubuti.
(Na kumbukeni) Ibrahimu alipomwambia baba yake Azara “Unawafanya masanamu kuwa waungu? Hakika ninakuona wewe na watu wako mumo katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri.(6:74)
Na namna hivi tulimwonyesha Ibrahimu Ufalme wa mbingu na ardhi (kuwa ni wa Mwenyezi Mungu), na ili awe miongoni mwa wenye yakini.(6:75)
Na usiku ulipomwingilia (Ibrahimu na hali kakaa na makafiri) akaona nyota, alinena “(Nyota) hii ni Mola wangu.” Ilipotua (ikapotea), alisema (kuwaambia wale makafiri kama kwamba yu pamoja nao katika Ibada ile): “Sipendi waola wanaopotea (hawawepo ila wakati makhsusi tu).(6:76)
Na (usiku wa pili) alipouona mwezi unachomoza alisema: “Huu (mwezi) ndio Mola wangu.” Ulipotua alisema: “Asiponiongoza Mola wangu, bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu wapotofu(Na Mola huyu hawezi kuniongoza kwani anakuwa hayupo wakati mwingine).” (6:77).
Na (siku ya tatu) alipoliona jua linachomoza alisema (kuwaambia): “Hili (jua) ndilo Mola wangu. Huyu Mola mkubwa kabisa.” Lilipotua alisema “Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha (na Mungu).(6:78)
(Mimi) nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimewacha dini za upotevu. Mimi (ni Mwislamu) si miongoni mwa washirikina.” (6:79)
Watu wa jamii yake walimshangaa kwa msimamo wake wa kumpwekesha Allah(s.w) na kujadiliana naye kama ifuatavyo:
Na watu wake wakajadiliana naye (kwa kumwambia Unaacha Ibada ya wazee! Utadhurika)! Akasema: “Je, Mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, mnaowashirikisha naye. Isipokuwa Mola wangu akipenda jambo (kuwa, basi litakuwa). Mola wangu anakijua vyema kila kitu. Basi je, hamshiki mauidha (6:80)
“Na nitawaogopaje hao mnaowashirikisha, hali nyinyi hamwogopi kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kile ambacho
hakukiteremshia dalili kwenu (yoyote ya kuonyesha kuwa ni mungu)? Basi kundi gani katika mawili haya (langu au lenu) linastahiki zaidi kupata amani? Kama nyinyi mnajua jambo (lijibuni hili).(6:81)
“(Hapana shaka kuwa) wale walioamini na hawakuchanganya imani yao na ushirikina kuwa hao ndio watakaopata amani, nao ndio walioongoka.(6:82)
Na hizi ndizo (baadhi ya) hoja zetu tulizompa Ibrahimu juu ya watu wake. Tunamyanyua katika vyeo yule tumtakaye (kwa kuwa anakwenda mwendo tunaoutaka). Hakika Mola wako ndiye Mwenye hikima (na) ndiye ajuaye. (6:83)
Umeionaje Makala hii.. ?
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
Soma Zaidi...KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S.
Soma Zaidi...Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri?
Soma Zaidi...Mawaziri waliokuwa washauri wakuu wa Firauni wakataka wakusanywe magwiji waliobobea katika uchawi nchi nzima, kisha wapambanishwe na Nabii Musa(as).
Soma Zaidi...LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam).
Soma Zaidi...Vita vya Ahzab- Maquraish waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu.
Soma Zaidi...