Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao

Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao


Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.s), bali walidhihirisha jeuri yao kwa kumuua ngamia wa muujiza ili waione hiyo adhabu waliyoahidiwa (Rejea Qur-an 7:77). Baada ya kumuua ngamia walipewa siku tatu kama fursa ya mwisho ya kuamini na kutubia makosa yao. Badala ya kutubia kama vile haitoshi kwa kosa walilolifanya, walikula njama za kumuua Nabii Salih na wale walioamini pamoja naye.




Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya matata (kabisa) katika ardhi (hiyo) wala hawakusuluhisha (jambo ila kuharibu tu). Wakasema: β€œApianeni kwa Mwenyezi Mungu (ya kwamba) tutamshambulia usiku yeye (Salih) na watu wake, kisha tutamwambia mrithi wake; Sisi hatukuona maangamio (yake wala) ya watu wake na bila shaka sisi ni wa kweli kwao.(27:48-49)



Basi wakapanga vitimbi (vyao); na sisi tukapanga mipango yetu
(tukapangua vitimbi vyao)na hali ya kuwa hawana habari. (27:50)

Kuangamizwa Makafiri na Kunusuriwa Waumini Mwisho wa siku ya tatu makafiri waliangamizwa na wakanusurika Salih(a.s) na wale walioamini pamoja naye kama tunavyojifunza katika Qur-an:



Basi ilipofika amri yetu, tukamuokoa Salih na wale walioamini pamoja naye kwa rehema Yetu; na (pia tukawaokoa) katika hizaya ya siku hiyo. Hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu (na) Mwenye kushinda.(11:66)



Na wale waliodhulumu (nafsi zao) uliwaangamiza ukelele (uliopigwa na Malaika); wakapambazukiwa wametulia tu (wamekufa) katika majumba yao. Kama kwamba hawakuwamo humo. Sikilizeni. Hakika Thamud walimkufuru Mola wao; basi Thamud wamepotelea mbali. (11:67-68)




Mtetemeko wa ardhi ukawanyakuwa (roho zao) na wakawa wamekufa humo katika miji yao. Basi (Salih) akawaacha (akenda zake), na huku anasema: β€œEnyi kaumu yangu! Nilikufikishieni ujumbe wa Mola wangu na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye nasaha.” (7:78-79)



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa jeshi la Allah(s.w) lililotumika kuwaangamiza makafiri wa Kithamud ni tetemeko la ardhi lililosababishwa na ukelele wa Malaika. Kumbuka:





β€œNa majeshi ya mbingu na ardhini ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, mwenye hikima.” (48:7)



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1483

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰2 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    πŸ‘‰4 Dua za Mitume na Manabii    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Vita vya uhudi

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtume Muhammad s.a. w akutana na Bahira

Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 11

Soma Zaidi...
Mapambano ya waislamu dhidi ya maadui wa kiyahudi madina

Mayahud Mwanzoni Mayahud walipoona kuwa Waislamu wanafunga siku ya Ashura pamoja nao na wanaelekea Qibla cha Baitul- Muqaddas pamoja nao hawakuonyesha chuki ya dhahiri dhidi ya Mtume(s.

Soma Zaidi...
Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Nuhu(a.s)

(i) Tuanze kulingania kwa Tawhiid – kumjua Allah(s.

Soma Zaidi...
Mafunzo kutokana na vita vya badri

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...