MTAZAMO NA HUKUMU YA KUPANGA UZAZI WA MPANGO KWENYE UISLAMU
Atika uislamu swala la kupanga uzazi linaruhusiwa endapo kutakuwa na sababu maalumu za kisheria.
Kupanga Uzazi katika Uislamu.
Atika uislamu swala la kupanga uzazi linaruhusiwa endapo kutakuwa na sababu maalumu za kisheria. Ugumu wa maisha ama kushindwa kuwalisha watoto si sababu ya kupanga uzazi kwenye uislamu. Na kwa wale ambao wapo katika dharura za kutumia njia ya uzazi wa mpango, si kila njia zinaruhusiwa kwenye uislamu. Uislamu unaruhusu njia zile tu ambazo hazina madhara kiafya. Na pia kuna muda maalumu wa kutumia njia hizi.
Uislamu umeharamisha pia kudhibiti uzazi kwa mtu binafsi kwa khofu ya kushindwa kuwalisha au visingizio vingine. Hata hivyo Uislamu haujawataka watu wazae kiholela.
Kwanza umekataza watu kuzaana nje ya ndoa. Pili, walioona wanatakiwa wazingatie umri baina ya mtoto na mtoto mwingine. Kwa anayetaka kukamilisha muda wa kunyonyesha, basi amnyonyeshe mtoto
wake kwa miaka mwili:
Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwilikamili, kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha…” (2:233)
Kunyonyesha humsababisha mama mzazi kuchukua muda mkubwa kabla ya kuingia tena katika siku zake. Iwapo mwanamke atapata siku zake wakati mtoto yungali mchanga (hajafikia umri wa miaka miwili), anatakiwa ajizuie asipate mimba; kwani katika Hadith iliyosimuliwa na Imamu Muslim, Mtume (s.a.w) amesema kuwa mwanamke akipata mimba wakati yungali na mtoto mchanga, afya ya mtoto hudhurika.
Njia za kuzuia mimba katika kipindi hiki cha kunyonyesha ni zile ambazo hazina madhara ya kiafya kwa baba wala mama. Katika Hadith iliyopokelewa na Bukhari na Muslim, Jabir (r.a) amesema kuwa wakati wa Mtume (s.a.w) wao walikuwa wanatumia njia ya kuzuia mimba inayoitwa ‘azal” (with drawal au coitus interuptus), yaani njia ya kumwaga mbegu za uzazi nje lakini Mtume (s.a.w) hakuikataza.
Hapa ifahamike kwamba suala la kupanga juu ya muda wa kunyonya mtoto linamhusu baba na mama; kwani hali za watu zinatafautiana. Ama kwa mama atakayekuwa na matatizo ya kiafya, ikathibiti kuwa akibeba mimba atadhurika au kuhatarisha maisha yake, anaruhusiwa kufunga kizazi hata kutoa mimba ambayo imeshatunga
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Mda wa mwisho wa kula daku mwezi wa ramadhani
Post hii fupi itakwenda kukujulisha utaratibu wa kula daku.
Soma Zaidi...Miiko au Mambo yanayoharibu/kubatilisha funga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kujitwaharisha kutokana na najisi
Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi.
Soma Zaidi...Ni nini maana ya uchumi katika uislamu
Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi.
Soma Zaidi...