5.
5. Haki na Uhuru wa kuchuma katika Uislamu
Kwa kuwa kuchuma kwa njia za halali ni wajibu kwa kila mwenye uwezo wa kufanya kazi, hapana budi kila mtu kupewa uhuru kamili wa kutumia juhudi yake na vipawa vyake katika kuchuma kwa njia za halali. Katika Uislamu ni kosa kubwa kwa serikali au Dola kuweka vikwazo vya kuwazuia watu wasitumie vipaji vyao na uwezo wao wote katika kuchuma kwa njia za halali. Kinyume chake, serikali au dola ya Kiislamu ina wajibu wa kuondoa vikwazo vyote vinavyowazuia watu kutumia vipawa vyao vyote katika kuchuma na inawajibu pia wa kutoa motisha na vishawishi vya kuwavutia watu binafsi au watu waliojiunga katika vikundi wajiingize katika sekta mbali mbali za uchumi kwa juhudi kubwa na maarifa.
Pamoja na uhuru kamili uliotolewa na Uislamu wa kuchuma kwa njia za halali kwa kadri ya uwezo wa kila mtu, pia unampa kila mtu haki ya kumiliki kila alichokichuma kwa njia za halali kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
βWala msitamani vile ambavyo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma, na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma. Na mwombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mjuzi w a kila kitu. (4:32)
Umeionaje Makala hii.. ?
Zoezi hili linamaswali mbalimbali kuhusiana na swala na masharti ya swala.
Soma Zaidi...Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu.
Soma Zaidi...Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha
Soma Zaidi...(a) UgirikiTunajifunza katika historia ya Ulimwengu kuwa jamii ya Wagiriki ilikuwa miongoni mwa jamii zilizoanza kustarabika.
Soma Zaidi...Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba?
Soma Zaidi...