Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Na. |
Zakat |
Sadaqat |
1. |
Inahusiana na utoaji wa mali tu. |
Inahusiana na utoaji wa mali na huduma. |
2. |
Ni faradhi (amri) tu kwa tajiri muislamu aliyefikia kiwango cha Nisaab. |
Ni wajibu kwa kila mtu kadri ya uwezo wake pindi inapohitajika. |
3. |
Zakat hutolewa kwa kiwango maalumu (2.5% au 1/40) cha mali inayojuzu kutolewa zaka. |
Sadaqat haina kiwango maalumu. Kila muislamu atatoa kulingana na uwezo wake. |
4. |
Zakat hutolewa baada ya mwaka au mavuno. |
Sadaqat haina muda maalumu wa kutoa. |
5. |
Zakat hustahiki kupewa Waislamu tu. |
Hupewa mtu yeyote bila kujali dini au uwezo wake, bali kila anayehitajia. |
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...