image

Kumuosha maiti hatua kwa hatua nguzo zake, na suna zake

Kumuosha maiti hatua kwa hatua nguzo zake, na suna zake

Kumuosha Maiti



Kumuosha maiti ni Faradh Kifaya. Maiti hawezi kuswaliwa mpaka akoshwe kwanza kama vile ilivyo haramu kuswali bila ya kuwa twahara. Ni maiti ya Muislamu aliyekufa shahidi katika vita vya kupigania Uislamu tu ndiye anayezikwa hivyo hivyo na damu zake bila ya kuoshwa kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
“Ibn Abbas (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alipitisha amri juu ya watu waliokufa katika vita vya Uhud kuwa nguo zao za chuma na ngozi walizovalia zinaweza kuvuliwa bali wazikwe hivyo hivyo na damu pamoja na nguo zao nyingine za kawaida.” (Abu Daud, Ibn Majah).


1. Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake. Watoto wadogo wanaweza kuoshwa na wanaume au wanawake.Pia ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe.
2. Ni mtu mmoja tu anayeosha na mwingine/wengine wa kumpa msaada pale atakapohitajia.
3. Ni muhimu muoshaji ayafahamu masharti ya kuosha maiti ya Muislamu yafutayo:
4. Muoshaji awe Muislamu.
5. Mahali pa kuoshea pawe faragha - panaweza kuwa bafuni, au sehemu ya ua uliojengwa maalumu kwa kazi hiyo au hata chumbani kama wafanyavyo watu wengi.
6. Maiti ioshwe huku imefunikwa gubi-gubi kwa nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenyeza.
7. Muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa gloves.
8. Kuchunga yale masharti yote yanayopaswa yatekelezwe na mwenye kukoga josho la wajibu kama vile kuwa na maji safi ya kutosha, pasiwe na kizuizi cha kuzuia maji kupenyeza mwili wa maiti.


Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na Sunnah za kuosha maiti. Nguzo za kuosha ni mbili:
(i)Nia.
(ii)Kueneza maji mwili mzima wa maiti.



Ni sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi ya hivyo. Lakini katika idadi ya witri kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



Ummu Atiyyah (r.a) amesimulia kuwa: Mtume wa Allah alitujia tulip okuwa tukimuosha (marehemu) binti yake (Zainab r.a). alisema: Muosheni mara tatu au mara tano au zaidi ya hapo kama mtaona hapana budi kufanya hivyo kwa maji ya mkunazi (lot tree) na w ekeni kafuri (karafuu maiti) au kitu kama hicho kwenye maungio (joints). Mtakapo maliza niiteni. Kwa


hiyo baada ya kumaliza tulimwita. Alitupa shuka yake ya kiunoni na kutuambia: Mfunikeni nayo. Katika maelezo mengine, Mtume (s.a.w) alisema: Muosheni katika witri mara tatu, au mara tano, au mara saba na anzeni na upande wake w a kulia na viungo vya kutaw adha. Akasema (Ummu Atiyah): Tulimuosha nywele zake mara tatu na kisha tukamlaza chali (kwa mgongo). (Bukhari na Muslim)



Namna ya Kuosha Maiti hatua kwa hatua
1.Maiti awekwe juu ya kitanda chenye tobo katikati la kupitishia uchafu utokao tumboni kama upo.



2.Lichimbwe shimo (ufuo) usawa wa tobo la kitanda, la kuhifadhi uchafu utakao toka kwa maiti. Iwapo hapana uwezekano wa kutengeneza ufuo, pawekwe kitu cha kukinga uchafu badala yake. Anaweza kuoshewa bafuni. Maiti ifunikwe nguo moja kubwa, iliyo nyepesi kiasi cha kuruhusu maji kupita.



3.Maiti ikalishwe kitako juu ya hicho kitanda na makalio yake yawe sawa sawa na hilo tobo la kitanda na ufuo chini yake na iinamishwe kidogo nyuma. Kama ni maiti ya mtu mzima ni vyema msaidizi wa mwoshaji amuegemeze maiti kwa goti lake.



4.Mwoshaji apitishe mkono wake wa kushoto juu ya tumbo la maiti aliminyeminye kwa taratibu ili utoke uchafu uliomo humo ndani.



5.Amlaze chali na amminyeminye tumbo lake kama hapo awali.



6.Aikalishe tena kisha apitishe mkono wake wa kushoto chini, ukiwa umevalishwa gloves asafishe tupu mbili huku anajimiminia maji kwa mkono wa kulia mpaka atakate.


7.Muoshaji, baada ya hapo, azungurushe kitambaa kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto, akichovye majini, kisha amswakishe maiti vizuri meno ya juu na ya chini, kisha akitupe ufuoni.



8.Azungurushe kitambaa kingine kwenye kidole kidogo cha mkono wa kushoto, akichovye majini, kisha amsafishe kwacho tundu za pua, kisha akitupe ufuoni.



9.Achukue kijiti laini achokonoe kucha zake maiti, iwapo ni ndefu na chafu.



10.Akiwa pia amemkalisha, amtawadhishe maiti kwa kufuata utaratibu wa kawaida wa kutawadha. Lakini wakati wa kumwosha uso, amuinamishe mbele kidogo ili maji yasimwingie ndani.


11.Maiti akiwa katika hali hiyo hiyo ya kukaa, mwoshaji ataanza kumwosha kichwa huku akiwa amemuinamisha kwa mbele. Kama nywele ni nyingi zichanwe panapo uwezekano na zioshwe kwa sabuni. Kisha maji yamiminwe mpaka povu la sabuni liishe. Nywele na ndevu zichanwe vizuri na mwanamke mwenye nywele nyingi asukwe mikia.


12. Nywele zitakazong’oka ziambatanishwe na sanda.



13.Baada ya kuoshwa kichwa, maiti alazwe kwa ubavu wa kushoto, kisha kuanza kumwosha ubavu wa kulia kwa kumiminia maji mbele na nyuma pamoja na kusugua kwa sabuni. Kisha kummiminia maji mengi mpaka povu liishe.



14.Kisha maiti atalazwa kwa ubavu wa kulia na kuoshwa ubavu wa kushoto kama ilivyofanyika kwa ubavu wa kulia.



15.Baada ya makosho haya mawili - la maji na sabuni na la kuondoa sabuni, pawe na kosho la tatu la maji yaliyowekwa karafuu maiti na marashi kidogo. Karafuu maiti inasaidia kulegeza maungio na kufanya mwili wa maiti usitepete.



16.Baada ya makosho haya matatu, mwoshaji anyooshe viungo vya maiti na kumlaza sawasawa kama alivyolazwa mara baada ya kufa, kisha achukue nguo kavu na kumfuta maiti kama mtu anavyojifuta kwa taulo baada ya kukoga. Kisha maiti awekwe juu ya mkeka mkavu na afunikwe nguo kubwa kavu tayari kwa kupambwa na kuvalishwa sanda.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1243


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Wanaostahiki kupewa sadaqat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mda wa mwisho wa kula daku mwezi wa ramadhani
Post hii fupi itakwenda kukujulisha utaratibu wa kula daku. Soma Zaidi...

Aina za swala..
Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mirathi Katika Uislamu, nani anarithi na ni mambo gani ya kuzingatia kabla ya kirisisha
Soma Zaidi...

Dhana ya kumiliki raslimali katika uislamu
Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu. Soma Zaidi...

Aina ya biashara zilizo haramu kwenye uislamu
Hapa utajifunza aina za biashara ambazo ni haramu. Soma Zaidi...

Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzika maiti ya kiislamu, hatua kwa hatua
Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa. Soma Zaidi...

MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k
Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende. Soma Zaidi...

Haki ya kumiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...

Namna ya kuhiji, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...