picha

Haki ya Serikali kuzuia Dhulma

Haki ya Serikali kuzuia Dhulma

Haki ya Serikali kuzuia Dhulma



Kwanza,
serikali ya Kiislamu inao wajibu wa kuandaa mazingira mazuri ya kihuduma na kimawasiliano kuwawezesha raia kujiletea maendeleo na inao wajibu wa kuingilia kati ili kusimamia haki na kuzuia dhulma. Ni wakati gani kwa mfano ambapo serikali inaweza kuingilia kati. Allah ndiye aliyeziumba rasilimali zilizopo duniani na hivyo ni wajibu wa binaadamu kuzitumia rasilimali hizo kwa manufaa ya watu na kwa ufanisi. Hivyo serikali yaweza kuingilia kati iwapo rasilimali hizo zitatumiwa kuwadhulumu watu au hazitatumika kwa ufanisi.



Pili, baadhi ya kazi ni haramu katika Uislamu kwa sababu zimefungamana na mambo ya haramu, kama vile kamari, umalaya, uchawi, ulevi n.k. Ni wajibu wa serikali kuona kuwa mambo hayo hayapewi nafasi katika jamii.



Tatu, ni wajibu wa serikali pia kutoa fursa sawa kwa watu wote ya kuendeleza na kuvikuza vipaji vyao kwa kuwapa fursa sawa za elimu na mafunzo. Ni wajibu wa serikali kugharamia elimu kwa ajili ya manufaa ya watu wote. Elimu ni haki ya msingi kwa wanadamu wote.



Nne, ni wajibu pia wa serikali kuhakikisha kuwa hata katika zile kazi za halali kisheria zinafanywa kwa uadilifu pasi na dhulma yoyote. Yaani Serikali ihakikishe mathalani kuwa bidhaa zinazotolewa zimefikia ubora kwa wanaoizalisha, kuona kuwa uadilifu wa kitaalamu unadumishwa, kuona kuwa Wafanyakazi wanalipwa mishahara kwa haki.
Hata hivyo, Uislamu hauelemei upande mmoja tu wa kumtetea mfanyakazi peke yake wala kumtetea mwajiri peke yake. Wafanyakazi pia wakileta madai yasiyo ya haki ni juu ya serikali kuingilia kati.



Tano, ni wajibu wa serikali pia kuzuia mambo yanayoweza kudhuru watu, kwa mfano kama mtu akijenga kiwanda cha hatari katika makazi wanamoishi watu. Au hata mambo yanayoweza kuwatesa wanyama, kama kuwabebesha mizigo mizito sana hadi wanaanguka na kuvunjika miguu au kufa, au kuwafanyisha kazi kwa mateso makubwa na kutowapa chakula cha kutosha. Hali kadhalika serikali inaweza kwa mfano kuzuia magari au meli iliyopakia abiria au mizigo kuliko uwezo wake.



Sita, katika suala la usambazaji wa bidhaa, serikali inaweza kuingilia kati iwapo watu watahodhi vyakula na bidhaa nyingine muhimu kwa lengo la kupandisha bei.
Saba, ni wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu (in-frastructures) na kuidhibiti, kwa mfano kujenga barabara, madaraja, reli, kusambaza maji ya bomba, kujenga mitambo ya umeme, simu n.k.



Wakati wa Ukhalifa wake, Ali (r.a) alimwambia Nahri, ambaye alikuwa mkuu wa jimbo la Misri; โ€œUsifanye ukusanyaji wa kodi ya ardhi kuwa ndiyo kazi yako kubwa; kazi yako kubwa ni kuindeleza ardhi hiyo.โ€




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 1154

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game     ๐Ÿ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰5 ai web app     ๐Ÿ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa

Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.

Soma Zaidi...
TOFAUTI KATI YA MAKATOZO NA MAAMRISHO KATIKA SUNNAH

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ู‡ูุฑูŽูŠู’ุฑูŽุฉูŽ ุนูŽุจู’ุฏู ุงู„ุฑูŽู‘ุญู’ู…ูŽู†ู ุจู’ู†ู ุตูŽุฎู’ุฑู ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ู‚ูŽุงู„ูŽ: ุณูŽู…ูุนู’ุช ุฑูŽุณููˆู„ูŽ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ูŠูŽู‚ููˆู„ู: "ู…...

Soma Zaidi...
Hizi ndio nyakati za swala tano na jinsi ya kuchunga nyakati za swala.

Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkuchunga nyakatibza swala tano.

Soma Zaidi...
Mambo yanayoharibu Udhu (yanayobatilisha udhu)

Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu.

Soma Zaidi...