5.
5.1. Misingi na Maadili Katika Uislamu
Maana ya Maadili
Ni mwenendo na tabia inayomfikisha mwanaadamu katika hadhi yake yak ukhalifa na kufikia lengo la kuumbwa kwake.
Mtazamo wa Makafiri juu ya Maadili
Wanafalsafa wa kikafiri wamejaribu kutoa majibu ya maswali ya msingi yafuatayo;
1) Ni lipi lengo kuu la maisha?
2) Ni zipi chem.-chem tunazozitegemea kutambua yapi mema na yapi maovu?
3) Nani msimamizi wa maadili katika jamii?
4) Ni kipi kichocheo kinachowafanya watu katika jamii wawe na maadili?
Udhaifu wa majibu ya maswali haya
1) Lengo kuu la maisha hapa duniani ni;
1. Kuishi maisha yenye furaha – Je, ni furaha ya nini, ya aina gani, ya nani?
2. Kufikia utimilifu – Je, ni upi utimilifu?, wa nini? wa nani?, na kivipi?
3. Kutimiza wajibu kwa lengo la kutimiza wajibu – Je, ni lipi hilo lengo?, nani kaliweka?, lina maana gani?
2) Utambuzi wa mema na maovu ni;
1. Kwa kutumia uzoefu (human experience) – Je, ni uzoefu wa nani? wa nini?
Na kwa muda gani?
2. Kwa kutumia silka zetu (intuition) – Je, tutegemee akili ya nani? kizazi kipi?
3. Kwa kufikiri na kuhoji (rationalism) – Je, ni fikira zipi na za nani?
3) Msimamizi wa maadili ni;
1. Kuwa yatasimamiwa na lengo husika – Je, lengo lipi ndio sahihi? n.k.
2. Kanuni zinazooana na hoja, akili (law of practical reason) – Je, ni akili ya nani itumike? Na kivipi?
3. Serikali kwa kutumia vyombo vyake.
4. Maoni ya watu katika jamii – social pressure
4) Motisha wa Kufuata maadili ni;
1. Kutaka malipo na kuepuka adhabu (reward and punishment) – Je, ni nani anayetoa malipo au adhabu?
2. Maumbile ya binaadamu kutii na kuheshimu sheria.
Hivyo, ni wazi kuwa majibu na hoja zote zinaudhaifu mkubwa sana na kamwe haziwezi kumwongozo mwanadamu kimaadili.
Mtazamo wa Uislamu juu ya Maadili
Udhaifu wa majibu ya makafiri juu ya maadili ni kutojua chanzo, hadhi na lengo halisi la mwanaadamu hapa ulimwenguni.
Hivyo, Uislamu unajenga maadili kwa kujibu maswali yafuatayo kwa usahihi;
1) Nini chanzo cha binaadamu? – Ni Allah (s.w)
Rejea Qur’an (15:28-29)
2) Ni ipi hadhi ya mwanaadamu hapa ulimwenguni? – Ni Khalifa, kiongozi wa
Allah (s.w). Qur’an (2:30-34).
3) Ni lipi lengo kuu la maisha ya mwanaadamu na vyote vinavyomzunguka?
- Mwanaadamu ameumbwa ili kumuabudu Allah (s.w). Qur’an (51:56).
- Viumbe vinavyomzunguka ni kumwezesha binaadamu kufikia lengo lake.
Rejea Qur’an (2:29), (17:70)
4) Ni ipi chem chem ya ujuzi wa mema na maovu?
- Ni Allah (s.w) kupitia Vitabu vyake na Mitume wake. Qur’an (57:25)
- Qur’an na Sunnah (Hadith za Mtume (s.a.w))
5) Ni nani msimamizi wa maadili katika?
- Ni imani thabiti juu ya Allah (s.w), siku ya mwisho na nguzo za imani.
Rejea Qur’an (33:36)
- Mamlaka na Dola ya Kiislamu.
Rejea Qur’an (22:41)
6) Ni kipi kichocheo cha watu Kufuata maadili katika jamii?
- Ni kuhofu adhabu ya Allah (s.w) duniani na akhera
Rejea Qur’an (89:25-26)
- Kutarajia msamaha na malipo ya pepo maisha ya akhera.
Qur’an (9:111), (61:10-13)
- Kuhofu mamlaka ya Dola ya Kiislamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mtume amemfundisha kuwa watoto wafundishwe kuswali wakiwa na miaka saba na waadhibiwe wakiacha wakiwa na miaka 10
Soma Zaidi...Post hiibinakwenda kukufundisha mambo ambayo yanaharibu udhu.
Soma Zaidi...Posti hiibinakwenda kukufundisha kuhusu hadathi ya kati na kati.
Soma Zaidi...Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali.
Soma Zaidi...