7.
7. Mfumo wa benki
Mabenki ni taasisi za fedha ambazo ni muhimu sana katika uchumi. Benki husaidia uchumi kwa kutoa huduma kuu zifuatazo:
Kwanza, Benki hutoa huduma ya kuhifadhi akiba za watu na kuhifadhi mali zenye thamani kubwa kama vile dhahabu, na mfano wake.
Pili, kutokana na akiba inazozikusanya, benki hujikuta kila wakati ina fedha nyingi zisizo na shughuli yoyote. Benki hukopesha fedha hizi kwa watu wanaozihitajia ili ziwe mtaji wa kuendeleza biashara, viwanda, kilimo na sekta nyingine mbali mbali za uchumi na utoaji huduma.
Tatu, benki hutoa huduma ya kurahisisha malipo kwa njia ya hundi (cheque) kuwalipa Wafanyakazi kupitia benki zao au kwa hundi, huwaepusha walipaji na hatari ya ku ib iwa.
Nne, pia benki hutoa huduma ya kutoa malipo ya mbali popote pale penye matawi yake nchini au ulimwenguni. Huduma hii ni muhimu sana kwani huwapunguzia watu mzigo wa kusafiri na fedha nyingi mkononi.
Badala yake benki huidhinisha malipo kwa simu au kwa njia yoyote ya mawasiliano ya haraka katika tawi la Benki hiyo popote lilipo nchini au ulimwenguni kupitia kwenye Account ya huyo anayestahiki kulipwa.
Huduma hizi muhimu na nyinginezo nyingi ambazo hatukuzitaja hapa zinatudhihirishia umuhimu wa kuwepo taasisi hii ya fedha katika jamii. Hivyo ni dhahiri kwamba Uislamu ukiwa ni mfumo kamili wa maisha unaojitegemea kwa kila kitu, hautarajiwi ukapinga au ukaharamisha kuwepo kwa mabenki katika jam ii.Bali Uislamu u n ah aram is ha m ab en ki yanayoendeshwa kwa kipato cha riba.
Mabenki ya Riba
Mabenki ya kitwaghuti (yasiyokuwa ya Kiislamu) sehemu kubwa ya kipato chake hutokana na riba.
Mabenki ya Riba hukopesha watu wenye miradi mbali mbali ya uchumi na kuwatoza riba kubwa katika mfumo wa malimbikizo (compound interest). Sehemu ndogo ya riba inayokusanywa na Benki za Riba, hutumiwa katika kuwalipa wateja walioweka akiba zao ambao ndio hasa matajiri walioifanya Benki iwepo.
Ni kutokana na unyonyaji wa namna hii utakuta, wakati wakulima na Wafanyakazi wa ngazi za chini ambao ndio wanaovuja jasho ili kuchangia riba, hawajimudu katika kujipatia chakula, mavazi, na makazi bora, wenye mabenki wanagawa βbonus β kwa wafanya kazi wao na wao wenyewe wanaponda starehe na anasa zilizopindukia kutokana na riba ambayo hawakuitoleo jasho lolote.
Umeionaje Makala hii.. ?
Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki.
Soma Zaidi...KuzuilianaTumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10.
Soma Zaidi...Hii ni hutuba ya ndoa kwa ufupi, Imekusanya mambo ya msingi yanayohitajika katika hutuba ya ndoa
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha maana ya neno talaka katika uislamu kisheria na kilugha.
Soma Zaidi...Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla.
Soma Zaidi...(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu.
Soma Zaidi...