Posti inahusu nzaidi kufunga kwa mishipa ya machozi ya mtoto kwa kawaida mishipa ya mtoto inapaswa kufunguka baada ya mwaka mmoja lakini kwa wengine ubaki imefungwa hata baada ya mwaka mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kwa mtoto.
Sababu za mishipa ya machozi kufunga kwa mtoto.
1.Kama tulivyotangulia kusema kwamba mishipa ya watoto wadogo uanza kufunguka pale anapofikisaha wiki 2 mpaka miezi 3 ama lakini kwa watoto wengine mishipa huu ubaki imefungwa na kusababisha madhara makubwa kwa mtoto katika makuzi yake, kwa hiyo kuna sababu mbalimbali ambazo ufanya mishipa hiyo kufunga na kusababisha madhara makubwa kwa mtoto kama ifuatavyo.
2. Pengine kuna valve ambazo zipo kwenye mwisho wamishipa ya machozi kutofunguka kama inavyotakiwa.
Kwa kawaida kwa mtoto ni lazima valve zote ambazo ziko kwenye macho zinapaswa kufungunguka kwa wakati wake lakini nyingine hubakia zimefungwa hali ambayo Usababisha mishipa ya machozi kwa mtoto kufunga na kusababisha madhara kwa mtoto na kwa jamii inayotunza mtoto huyu kwa hiyo tatizo liligunduliwa linaweza kutibiwa ambapo upasuaji unaweza kufanyika ili kufungua hizo valve.
3. Kuwepo kwa uwazi sehemu ambapo machozi upitia
Kwa sababu ya kuwepo kwa uwazi kwenye sehemu ya machozi yanapopitia kwa kitaalamu huitwa eylid usababisha mishipa ya machozi kufunga, kwa hiyo ili tatizo la kuwepo kwa uwazi usababishwa na maumbile ya mtoto au kuna Maambukizi ya macho ambayo Usababisha kuwepo kwa uwazi huo.Na pia hili tatizo linaweza kusaidiwa kwa kuwepo kwa upasuaji na kuziba sehemu hiyo.
4. Mishipa ya machozi kuwa nyembamba kuzidi kawaida.
Kwa wakati mwingine kuna kipindi mishipa ya machozi inakuwa kweli nyembamba kupita kiasi hali ambayo Usababisha kufunga kwa mishipa ya machozi kwa watoto, kwa hiyo basi ni vizuri kabisa kumpeleka mtoto hospitalini ili kuweza kuona tatizo mliko wapi na kuweza kulifanyia kazi kwa hiyo mishipa nya machozi kwa kawaida inapaswa iwe mipango.
5.Kuwepo kwa Maambukizi kwenye macho.
Kwa wakati mwingine maambukizi ndicho chanzo kikuu cha kuwepo kwa Ugonjwa huu, kwa sababu kama kuna Maambukizi ni vizuri kuyatibu ili kuweza kuruhusu mishipa ya machozi iweze kufunguka na mtoto aweze kuwa kama watoto wengine.
6. Kuuumia kwenye eneo la mishipa ya machozi na mifupa ya pua kuziba.
Kwa wakati mwingine mtoto anaweza kuumia kutokana na vitu mbalimbali kwenye eneo la mishipa ya machozi na kusababisha kufunga kwa mishipa ya machozi na kwa wakati mwingine kama kunakuwepo na kuziba kwenye mishipa ya pua pia usababisha kuziba kwa mishipa ya machozi.
Dalili za mishipa ya machozi kufunga kwa mtoto.
Pengine tunaweza kujiuliza juwa ni Dalili zipi zinazoonyesha kubwa kuna tatizo kwenye mishipa ya machozi kwa sababu tatizo lenyewe liko ndani na hatuwezi kuliona kwa nje, kwa hiyo Dalili ni kama ifuatavyo.
1. Macho kuwa na maji maji.
Kwa kawaida kama mishipa ya machozi imefungwa kitu cha kwanza utaona macho ya mtoto yanatoa maji mara kwa mara na pia mtoto anakaa bila raha kwa wakati mwingine macho yanakuwa yanawasha na mtoto anajikuna kwa hiyo hali hii umfanya mtoto kujihisi vibaya hata kama anacheza na wengine na kwa wakati mwingine wanakuwa wanamnyanyapa kwa sababu ya kutokwa na majimaji machoni.
2. Na pia macho ya mtoto mda wote yanakuwa yanatoka na Matongo tongo.
Kwa kawaida uchafu kwenye macho unakuwa hauna sehemu ya kuchujiwa kwa hiyo Matongo tongo utoka machoni, na kwa wakati mwingine ni kwa sababu ya kuwepo na Maambukizi kwenye jicho ndio yanasababisha hali ya kuwepo kwa Matongo , kwa hiyo mtoto anakosa raha na kujitenga na wengine kwa sababu ya tatizo la kuwepo kwa Matongo tongo kwenye macho
3. Uchafu mwingi kutoka machoni na pengine unakuwa na harufu mbaya.
Kwa wakati mwingine kunakuwepo na uchafu mwingi kwenye macho ambapo mtoto ukaa anapangusa uchafu kwa kitambaa kama ameshakuwa na uwezo huo kwa wakati mwingine mtoto anakuwa na mafua yanayoambatana na uchafu kutoka kwenye macho.
4.Na pia presha ya macho inawezekana kutokea ikiambatana na upofu
Kama tatizo halijafanyiwa ufumbuzi na kuweza kutibiwa upofu wa macho unaweza kutokea kwa mtoto na kusababisha madhara makubwa zaidi. Kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi ni vizuri kufanya mawasiliano na wataalamu wa afya ili kuweza kupata matibabu kwa mda mwafaka.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Post hii inahusu zaidi huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja, aina hiyo ya mimba kwa kitaalamu huitwa complete abortion.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu malengo ya kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano, huduma hii ilianzishwa na WHO na UNICEF mwaka 1990 ili kuweza kuzuia Magonjwa na kuwapatia watoto lishe pamoja na hayo walikuwa na malengo yafuatayo.
Soma Zaidi...Maambukizi kwenye Njia ya Uzazi kwa kifupi hujulikana Kama PID.ni Maambukizi ya mfumo wa Uzazi yanayoathiri wanawake, Maambukizi haya kwa Kawaida huhusisha sehemu Kama shingo ya uzazi,nyuma ya mfuko wa Uzazi na mirija ya uzazi.
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuongezeka uzito kwa wajawazito, Mara nyingi Mama akibeba mimba uongezeka uzito kutoka wiki ya Kwanza mpaka wiki ya mwisho ya kujifungua.
Soma Zaidi...Maambukizi ya fangasi katika sehemu za Siri za mwanamke husababishwa na fangasi wanaoitwa CANDIDA ALBICANS pia maambukizi haya hujulikana kama YEAST INFECTION. Pia hupatikana katika midomo, mpira wa kupitisha chakula,kibofu Cha mkojo ,uume na uke.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vyakula ambavyo usaidia katika uzalishaji wa homoni ya testosterone.
Soma Zaidi...Hizi ni siku hatari kwa mwanamke ambazo ni ahisi kwake kubeba mimba, siku nitakueleza ni zipi na ni zipi sifa zake
Soma Zaidi...