Posti hii inahusu malengo ya kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano, huduma hii ilianzishwa na WHO na UNICEF mwaka 1990 ili kuweza kuzuia Magonjwa na kuwapatia watoto lishe pamoja na hayo walikuwa na malengo yafuatayo.
Malengo ya kuwahudumia watoto chini ya miaka mitano.
1.lengo la kwanza ni kuzuia vifo kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano.
Hili ni mojawapo ya lengo ambalo limeweza kuwepo kwa sababu hapo mwanzoni palikuwepo na vifo vingi vya watoto wadogo chini ya miaka mitano kwa sababu ya kutokuwepo kwa chanjo na baada ya kuwepo kwa chuo Magonjwa mengi yamepungua kama vile kifua kikuu, kifadulo, Surua na magonjwa mengine mengi.
2.Lengo la pili ni kupunguza magonjwa.
Kuanzia malengo yalipoanza na mpaka sasa hivi magonjwa mengi yamepungua ambapo watoto Upata chanjo mapema na pia akina mama uweza kupata chanjo na dawa ili kuwakinga watoto wadogo na pia mahudhurio ya kliniki kila mwezi ambayo uangalia maendeleo ya mtoto.
3. Kuondoa aina yoyote ya ulemavu kwa watoto.
Hapo mwanzoni palikuwepo na ulemavu mbalimbali kwa watoto na sasa hivi ulemavu huo umetoweka kwa sababu ya kuwepo kwa dawa na maelekezo mbalimbali ya wataalamu wa afya kwa kufanya hivyo ulemavu kwa watoto wadogo umepungua kwa kiasi kikubwa.
4. Lengo lingine ni kuona maendeleo mazuri na ukuaji wa watoto kwa wakati, kufuatana na lengo hili watoto wengi wameweza kuangaliwa kuanzia miaka sifuri mpaka miaka mitano na pia mahudhurio ya kliniki yanafanyika ili kuweza kuangalia maendeleo ya mtoto kwa kutumia vigezo mbalimbali ambavyo ni uzito na kuangalia maendeleo ya kwa ujumla.
5. Kwa hiyo tunaona malengo haya ni mazuri na yameleta faida kubwa kwa watoto kwa hiyo tunapaswa kuwapeleka watoto kupata chanjo na mahudhurio ya kliniki ili kuweza kutokomeza maradhi yanayowapata watoto na kuzuia vifo kwa watoto wadogo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya HCG katika kupima mimba, HCG maana yake ni human chorionic gonadotropin ni homoni ambayo uonekanekana kwenye mkojo na damu kama mtu ana mimba.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mwanzo za ujauzito katika wiki ya kwanza
Soma Zaidi...DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO) Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Utasa wa Mwanaume hutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu za kiume, utendakazi usio wa kawaida wa manii au kuziba kwa manii ambayo huzuia utoaji wa mbegu za kiume. Magonjwa, majeraha, matatizo ya kiafya sugu, u
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nadharia ya kupata mtoto wa kiume.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Magonjwa yanayoshambulia sana ovari na Dalili zake, haya ni magonjwa ambayo yanashambulia sana ovari ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma muhimu anazopaswa kupewa mama mjamzito wakati akiwa na mimba, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua yaani ndani ya masaa ishirini na manne, tunajua wazi kuwa Mama akiwa mjamzito anaweza kupata matatizo mbalimbali kwa h
Soma Zaidi...