Navigation Menu



Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza

Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili.

Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza



DALILI ZA MIMBA YA WIKI, NA MIMBA YA MWEZI MMOJA




Baada ya kutambuwa sku sahihi ya kutafuta ujauzito sasa ninakwenda kukufahamisha kama mimba iliingia, kama harakati zako zilifahamika. Dalili nitakazokutajia unaweza kuzishuhudiandani ya wiki ya mwanza mpaka wiki ya nne. Hata hivyo kama utakuwa makini unaweza kugundua ndani ya siku chache tu kama sio siku moja ama mbili.



Kabla ya kuendelea ningependa utambuwe kuwa mimba huleta mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wa mwanamke. Hivyo ni lazima mabadiliko haya yaonyeshe dalili zozote punde tu inapoingia. Hivyo kwa mwanamke akiwa makini na mwii wake anaweza kugundua mabadiliko haya mapema sana. Kuna mwanamke mmoja alinieleza kuwa yeye anaweza kugundua ujauzito kama umetunga ndani ya masaa machache toka akutane kimwili. Nilistaajabu ila nilishindwa kumuuliza anatumia njia gani.



Dalili za mimba changa ni pamoja na:-





DALILI ZA MIMBA KATIKA WIKI YA KWANZA NA PILI (SIKU 7 MPAKA 14)
1.Kuendelea kwa joto la mwili. Kama ulikuwa makini na siku ambayo joto la mwili wako lilikuwa kubwa, kama ulishiriki tendo siku moja ama mbili kabla ama siku ile, basi endapo joto la mwili litakuwa endelevu hii huashiria huwenda ulibeba ujauzito. Kwa nini, ni kwa sababu joto la mwili hutokea baada ya mabadiliko ndani ya mwili hususani homoni mpya huzaliwa kwa ajili ya kuandaa ukuaji wa ujauzito. Mabadiliko haya ya joto yasifananishwe na joto la homa.



2.Katika wiki hii ya kwanza unaweza kuona mabadiliko ya majimaji kwenye uke. Majimaji yaliyokuwa siku za nyuma kidongo yanaweza kuanza kuchukuwa sura ya mfanano wa majimaji meupe ya yai lililovunjwa. Halikadhalika matarajio ni kuwa uke unatakiwa urudi katika hali ya ukavu baada ya kupita siku hatari. Lakini kama ujauzito ulitungwa uke hautarudi katika hali yake ya kawaida ya ukavu hivyo huanza kuzalisha majimaji kwa wingi. Mabadiliko haya si rahisi kuyaona ila endapo utakuwa manini zaidi unaweza kugundua.



3.Kutokwa na damu kidogo (implantation bleeding). damu hii inaweza kutokea mwishoni mwa wiki ya kwanza ama katikati ya wiki ya pili. Damu hii ni kidogo na inaweza kuwa ni matone kadhaa. Haifanani na damu ya hedhi na wala haitoki na maumivu. Damu hii si endelevu inaweza kutoka kwa muda mchache na kukata. Mwanamke anaweza kuona nguo yake ya ndani inamadoa ya damu. Kwa damu hii mwanamke hatahitai kuvaa pedi.



4.Maumivu ya kichwa ama kichwa kuwa chepesi. Hali hii inaweza kuandamana na kizunguzungu. Hali hii si lazima kuipata, hata hivyo wanawake wengine wanaipata ila hawafikirii kuwa ni tatizo kwani hutokea na kuondoka bila ya kuathiri mwili kwa muda mrefu. Hapa anaweza kuona ni hali ya kawaida kama hatatilia maanani mabadiliko haya.



Kumbuka dalili hizo tajwa hapo juu ni ngumu kuziona mpaka uwe makini sana kwani zinaweza kuathiriwa na hali nyingine za kiafya. Kwa mfano joto la mwili linaweza kusababishwa na mambo mengi kama maradhi, uchovu na stress. Majimaji ya ukeni yanaweza kuongezeka kwa sababu ya njia za uzazi wa mpango ama mabadiliko ya homoni.



DALILI ZA MIMBA KATIKA MWEZI WA KWANZA (Ndani ya siku 30)
Dalili hizi huweza kuonekana kwa urahisi kuliko hizo ambazo zimetajwa hapo juu. Ijapokuwa dalili hizi zinatokea ndani ya mwezi mmoja lakini zinaweza pia kutokea nje ya mwezi mmoja, yaani mpaka miezi mitatu. Sasa hebu tuzione dlili hizo:-



1.Kukosa hedthi.
Kama ujauzioto ulishika mwanamke hataweza kupata siku zake. Hii ni dalili ambayowanawake wengi wamekuwa wakiamini kama ndio dalili pekee. Yes hii ni katika dalili kubwa ambazo wanawake wengi wameitaja kuwa ndio dalili yao ya kwanza. Unajuwa ni kwa nini? Ni kwa sababu ndio ya pekee wanayoweza kuigundua. Ukweli ni kuwa kukosa hedhi pekee sio dalili ya ujauzito, hedhi inaweza kukosekana kwa sababu kadhaa kama zifuatazo:-



A.Mabadiliko ya homoni
B.Ujauzito
C.Maradhi
D.PID
E.Vyakula
F.Stress na misongo ya mawazo
G.Matumizi ya madawa
H.Mabadiliko ya hali ya hewa.





Nini mwanamke afanye baada ya kukosa hedhi?.
Yes hili ni swali zuri sana. Mwanamke aliyekosa hedhi kwanza aanze kufikiria kama alishiriki tendo la ndoa katika siku hatari ama laa. Kisha aangalie uwepo wa dalili nyingine kama nitakavyozitaja hapo chini. Kama hana dalili yeyote basui aangalie kama anapata maumivu sehemu yeyote, ama uwepo wa maradhi. Kama vyote hana ni vyema apime ujauzito. Kipimo cha mkojo kinaweza kuchelewa kutoa majibu, hivyo kama atapima wiki ya kwanz na asione kitu basi ni vyema akarudia tena wiki inayofata. Maelezo zaidi juu ya kutumia kipimo nitayataja hapo chini.



2.Maumivu ya matiti na chuchu, kujaa kwa matiti na mabadiliko ya rangi za chuchu.
Dalili hii huwapata wanawake wengi, hata hivyo wapo ambao hawaipati kabisa. Hebu tuanze kuona kwa ufupi dalili hii. Mabadiliko ya rangi ya chuchu na eneo la kuzunguka chuchu. Hii ipoje ni kuwa mwanamke aliyebeba ujauzoto chuchu zake zinaweza kubadilika na kuweka ukiza na weusi. Inaweza kuwa chuchu pekee na na eneo la chini kuzunguka chuchu.



Kwa baadhi ya wanawake wao matiti yanauma na yanakuwa kama yamejawa na kaugumu flani. Wakati mwimgine inaweza kuwa titi moja ama yanaweza kuwa yote ama yakapeana zamu. Ila maumivu haya ni maumivu ambayo yanavumilia si makali kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za kawaida. Kwa wanawake wengine maumivu haya hutokea pale anapoyaminya matiti yake.



Hata hivyo maumivu ya matiti pekee sio dalili ya moja kwa moja kuthibitisha ujauzito. Maumivu ya matiti yanaweza pia kusababishwa na maumivu ya kifua, shida katika homoni ama maradhi mengine. Hivyo bado itahitajika kupuma kupata uhakika.



3.Kukojoa mara kwa mara.
Wiki kadhaa zimepita toka kuingia, homoni mbalimbali zimezalishwa ndani ya mwili,kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mama na mtoto. Homoni hizi zinapelekea mabadiliko mbalimbali ndani ya mwili wa mama, hivyo kusababisha mapigo ya moyo kuongezeka, mchujo wa damu kuwa mkubwa na uzalishwaji wa mkojo kuongezeka. Hapa mama mjamzito ataanza kuhisi mabadiliko katika kukojoa kojoa. Dalili hii kwa baadhi yao inachelewa kuonekana hadi miezi ya mbele.




4.Mapigo ya moyo kuongezeka.
Hapa mwanamke anaweza kujihisi moyo kwenda mbio. Ukweli nikuwa kuna ongezeko la mapigo ya moyo kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya mtoto aliyetumboni hayaathiriki. Dalili hii pia inaweza kuchelewa kuonekana ndani ya mwezi wa kwanza. Kwa baadhi ya wanawake watajihisi lamda ana presha lakini ukweli ni kuwa hii sio presa ni ongezeko tu la mapigo ya moyo.



5.Maumivu ya tumbo.
Dalili hii inaweza kutokea hata katika wiki kadhaa za mwanzo. Ila mara nyingi hutokea ndani ya mwezi wa kwanza na ni endelevu. Yaani dalili hii inaweza kuendeea mpaka mtoto atakapozaliwa. Mwanamke awe makini sana na maumivu haya. Maana yanaweza kusababishwa pia na mambo mengine ikiwemo maradhi. Maumivu haya hayawezi kuwa makali kiasi cja kushindwa kufanya kazi za kawaida. Yanaweza kufanana na ya hedhi ama kuwa na uafadhali kidogo.





DALILI NYINGINE ZA UJAUZITO
1.Uchovu wa mara kwa mara
2.Maumivu ya tumbo mara kwa mara
3.Kichefuchefu
4.Tumbo kukuwa.
5.Mtotockucheza
6.Kuongezeka kwa uzito
7.Kupata kiungulia mara kwa mara
8.Kukosa choo
9.Maumivu ya mgongo
10.Hasira za mara kwa mara
11.Maumivu maeneo ya nyonga
12.Kuharisha



Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 153706


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Faida za uzazi wa mpango kwa watoto.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa watoto, sio akina Mama peke yao wanaofaidika na uzazi wa mpango vile vile na watoto wanafaidika na uzazi wa mpango kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Njia za kumsafisha Mama aliyetoa mimba.
Post hii inahusu njia safi za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki, kliniki nisehemu ambayo mtoto hupelekwa Ili kujua maendeleo ya mtoto akiwa chini ya umri wa miaka mitano Soma Zaidi...

Maambukizi katika mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Maambukizi kwenye Njia ya Uzazi kwa kifupi hujulikana Kama PID.ni Maambukizi ya mfumo wa Uzazi yanayoathiri wanawake, Maambukizi haya kwa Kawaida huhusisha sehemu Kama shingo ya uzazi,nyuma ya mfuko wa Uzazi na mirija ya uzazi. Soma Zaidi...

Sorry kunamchumba wangu katokwa na majimaji meupe na tumbo linamuuma BAADA mda likaacha nidalili za Nini au.nikawaida tu
Majimaji msule sehemu za siriyanaweza kuashiria mambo mengi ka mwanamke. Ikiwemo ujauzitina maradhi. Pia yanaweza kuashiria kuwa mwanamke unaweza kuoatavujauzito amalaa. Soma Zaidi...

Je siku ya kwanza kabisa ya ovulation mimba inakuwa ni uhakika kupata mimba?
Watu wengi wanadhania kuwa kufanya tendo la ndoa katika siku hatari ni lazima kuwa utapata ujauzito. Hili sio sahihi kabisa. Post hii itakwenda kuangalia jambo hili zaidi. Soma Zaidi...

Zijue sababu zinazosababisha kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume
Kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume kunamaanisha kuwa Majimaji (shahawa) unayotoa wakati wa kufika kileleni huwa na mbegu chache kuliko kawaida. Hesabu yako ya manii inachukuliwa kuwa chini kuliko kawaida ikiwa una chini ya mbegu milioni 15. Kuwa na idad Soma Zaidi...

Mimi kwenye korodani yai moja limezungukwa na majimaji ,na haya maji yamekuwepo toka utotoni mwangu lakin bado sijayaona matatizo yake , je kitaaramu hii inaweza kua na athari gani? ,Naombeni ushauri
Korodani ni kiungo muhimu kwa mwanaume, katika afya ya uzazi. Unaweza kusema ni kiwanda cha kutengeneza mbegu za kiume. Kiungo hiki ni sawa na ovari kwa mwanamke. Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo kabla ya kupata hedhi
Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kunyonyesha mtoto
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha mtoto, kunyonyesha ni kitendo cha Mama kutumia titi lake Ili kuweza kumpatia mtoto lishe kwa kipindi chote ambacho Mama upaswa kutumia kwa kunyonyesha mtoto wake kwa hiyo Kuna faida ambazo mama uzipata kutoka Soma Zaidi...