Zifahamu fibroids (uvimbe kwenye via vya uzazi)

Posti hii inahusu zaidi fibroids au uvimbe kwenye via vya uzazi hasa hasa utokea kwenye tumbo la uzazi ambapo kwa kitaalamu huitwa uterusi, uvimbe huu ulitokea watu wengine huwa hawawezi kutambua Dalili zake mapema kwa hiyo leo tunapaswa kujua Dalili zake

Dalili za fibroids.

1. Kwanza kabisa mama anatokwa na damu nyingi kwa ghafla inawezekana zikawa ni tofauti na damu za siku damu hizo zinaweza kuwepo kwa sababu ya kupasuka kwa uvimbe.

 

2. Kutokwa na damu nyingi wakati wa siku za mwezi na damu hizo kwa mara nyingi huwa ni za mda mrefu na uchukua mda kuweza kuisha zinaweza kufika hata siku saba.

 

3. Maumivu ya nyonga.

Kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe kwa hiyo ukandamiza viungo vya nyonga na kusababisha nyonga kuuma 

 

4. Kuwepo kwa haja ndogo ya mara kwa mara.

Kwa kawaida mkojo utoka kama mtu amekunywa chochote ila kama kuna uvimbe mkojo utoka mwingi na wa mara kwa mara.

 

5. Kuwepo kwa maumivu ya mgongo.

Kwa kawaida mgongo uuma  sana na kusababishwa kwa mgandamizo wa uvimbe kwa sababu uvimbe uweza kugandamiza nevu za kwenda kwenye mgongo.

 

6. Maumivu wakati wa kujamiiana.

Kwa kawaida watu wenye matatizo ya kuwepo kwa uvimbe huwa na maumivu wakati wa kujamiiana.

 

7. Kuwepo kwa upungufu wa damu.

Kwa kawaida dalili kubwa ya mtu mwenye uvimbe ni kutokwa kwa damu na damu ikitoka uwepo wa kupungukiwa kwa kiwango cha damu ni kawaida.

 

8. Maumivu ya kichwa uwapata wenye tatizo la uvimbe, kwa sababu ya kupungua kwa damu na pia maumivu ya kichwa uongezeka.

 

9. Maumivu kwenye miguu.

Hali hiyo utokea kwa sababu ya mgandamizo wa nevu zinazoenda miguuni pia na kuwepo kwa upungufu wa damu kwa hiyo Usababisha maumivu kwenye miguu.

 

10. Kuvimba kwenye sehemu za chini ya tumbo hili ni kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe kwenye via vya uzazi.

 

11. Kupata uzazi wa shida.

Kwa kawaida wenye uvimbe kwenye via vya uzazi wanaweza kuwa wagumba kama tatizo halijagunduliwa mapema pamoja na kupata uzazi wa shida.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/03/Friday - 08:01:30 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1037


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-