Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida za Uzazi wa mpango. Uzazi wa mpango ni huduma ambazo hutoa chaguo kwa familia kuwa na idadi ya watoto wanaotaka katika muda maalum, wanahisi na mbinu iliyoamuliwa.
Faida za Uzazi wa Mpango
Faida za Uzazi wa mpango zimegawanyika katika makundi manne ambayo Ni kwa watoto, kwa mama, kwa wanandoa na kwa jumuiya
Faida za Uzazi wa mpango Kwa Watoto
1. Watoto Kupata upendo kutoka kwa wazazi.
2. Hupata muda wa kutosha wa kunyonya
3. Watoto wanaweza kupata nafasi ya kuelimishwa na wazazi.
4. Kiwango cha vifo vya watoto wachanga/watoto hupunguzwa kwa Muda kati ya ujauzito.
Faida za Uzazi wa mpango Kwa Mama Ni pamoja na;
1. Mama atakuwa na afya kwa sababu anapata muda mwingin wa kupumzika baada ya ujauzito uliopita.
2. Kupunguza idadi ya mimba zisizotarajiwa.
3. Kupunguza idadi ya magonjwa ya uzazi, kiwango cha vifo.
4. Mama anapata muda mwingin na nafasi kwaajili ya kufanya shughuli nyingine.
Faida za Uzazi wa mpango Kwa Jumuiya Ni pamoja na;.
1. Familia ndogo inaongoza kwa uhifadhi wa maliasili na huduma.
2. Familia ndogo husaidia taifa kuwa na shule za kutosha, hospitali na huduma zingine za kimsingi.
3. Familia ndogo huzuia ukosefu wa ajira usio wa lazima.
4. Shughuli ndogo zilizopangwa polepole huleta furaha, maelewano ya amani na ustawi
Umeionaje Makala hii.. ?
Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa mtoto pindi anapozaliwa,tunajua wazi kuwa mtoto anapoanza kutokeza kichwa tu ndio mwanzo wa kuanza kumtunza mtoto na kuhakikisha anafanyiwa huduma zote za muhimu na zinazohitajika.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuhusu njia za uzazi wa mpango, uzazi wa mpango ni njia za kupanga uzazi Ili kupata idadi ya watoto unaohitaji
Soma Zaidi...Hali ya ujauzito huanza kutabirika Mara tu ya kujamiana, pia chemikali (hormon) za mwili huanza mchakato wa kuongeza na kupunguza utendaji kazi wa kemikali hizo mfano.follical stimulating hormon (FSH) na lutenazing hormon kuivisha yai tayari kwa kutengen
Soma Zaidi...Unaweza kupitiliza siku zako za hedhi kwa sababu nyingi. Post hii itakueleza ni kwa nini umechelewa kupata siku zako.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube, ni sababu ambazo ufanya mirija ya follapian tube kuziba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, ni faida wanazozipata waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji, ni madhara madogo madogo ambayo utokea kwa watumiaji wa matatizo ya kupumua.
Soma Zaidi...