NINI MAANA YA MINYOO: vimelea wa minyoo (parasites)

MINYOO NI NINI?

NINI MAANA YA MINYOO: vimelea wa minyoo (parasites)

NINI MAANA YA MINYOO?

MINYOO NI NINI?
Minyoo ni katika vimelea ama wadudu wanaoishi ndani ya kiumbe aliye hai. Wanaweza kuishi kwenye wanyama kama ngo'ombe, ngurue na mbuzi, pia wanaweza kuishi ndani ya binadamu. Wanajipatia mahitaji humo kama chakula, hewa na kila wanachohitaji. Wakiwa wanaishi ndani ya mwili wa kiumbe hai wanaweza kusababisha madhara makubwa sana katika afya ya mtu. Wadudu hawa kitaalamu wanatambulika kama parasitic worm.

Katika makala hii tutakwenda kujifunza, dalili, sababu, matibabu na njia za kupambana na minyoo katika mazingira yetu. Pia tutaona madhara ya kiafya yanayoletwa na kuishi na minyoo mwilini. Endelea kuwa nasi upate faida hii

Hatari ya kupata minyoo ni kubwa sana maeneo ya vijijini ama katika maeneo ambayo hali ya usafi sionzuri. Nchi zinazoendelea kama nchi za afrika ni katika maeneo ambayo yanakabil;iwa sana na minyoo kuliko nchi zilizo endelea.

Wataalamu wanatueleza kuwa kuna aina zaidi ya 300,000 (laki tatu) za minyoo. Na katika aina hizi kuna aina 300 (mia tatu) za minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu na kumuathiri kwa namna moja ama nyingine.

Minyoo wanazaliana kwa kutaga mayai, na mayai yao yanatofautiana ukubwa, kuna ambayo yanaonekana kwa macho na mengine ni madogo zaidi kwa kuonekana kwa macho. Kuna aina za minyoo hutaga mayai bila ya kuhitaji kuwepo kwa dume, kwani kuna minyoo ambayo ina jinsia zote kwa pamoja (hermaphroditc).

Minyoo huweza kutaga mayai zaidi ya mara sita kwa siku. Na idadi ya mayai yao ni kati ya mayai 3000, mpaka 700000. na mayai yao yanaweza kudumu kwa miezi mingi biala ya kufa, na yanaweza kuvumialia hali mbalimbali za joto.


                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 146


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-