Posti hii inahusu zaidi dalili za Dengue,ni Dalili ambazo huwa kwenye makundi matatu na kuwepo kwa makundi hayautegemea kuongezeka kwa tatizo kwa sababu tatizo likiongezeka bila kutibiwa na dalili uongezeka na kufikia kwenye sehemu isiyo ya kawaida kwa mg
1 Dalili ya kwanza ni homa ya Dengue
Hii ni mojawapo ya homa ambayo huwa tofauti kidogo na homa nyingine kwa sababu kunakuwepo na maumivu ya macho, kichwa kinauma kweli kweli, maupele yanaweza kuambatana na hiyo homa,na maumivu ya kwenye fizi za meno ambayo Usababisha na kuvuja damu kwenye fizi, kutapika damu na kwa wakati mwingine damu inaweza kuwa kwenye kinyesi, kutapika,kuishiwa na hamu ya kula, maumivu ya tumbo hayo yote uambatana na homa.
2. Dalili ya pili ni pale ambapo homa inaongezeka na kusababisha kila sehemu iliyokuwa inavuja kawaida kwenye homa ya kwanza ya dengua kuongeza na maumivu yanaongezeka na sehemu hii kwa kitaalamu huitwa hemorrhagic fever, homa hii inaweza kwenda kuanzia kwenye siku ya kwanza mpaka saba yaan wiki nzima na kwa upande wa watoto kuongezeka kwa homa usababisha kuwepo kwa degedege hali inayosababisha Ugonjwa huu kuleta shida sana kwa watoto.
3. Katika sehemu hii ya pili maumivu ya macho pia uongezeka na kusababisha kuwa mekundu na pia joint kwenye miguuu kuuumia na pia sehemu ile iliyokuwa na upele kidogo kidogo uongezeka na kuwa na mabaka mabaka hali ambayo ufanya Mgonjwa kuweza kuonekana vibaya na pia kiwango cha seli nyeupe za damu kupungua kwa sababu ya kuwepo kwa mashambulizi kati ya seli na Maambukizi kwenye mwili.
4. Katika hatua hiii ya mwisho ni pale Mgonjwa anakuwa amezidiwa sana na katika dalili hizi kupona ni bahati kwa sababu Mzunguko wa damu unapungua, upumuaji upungua , na msukumo wa damu nao upungua hali ambayo husababisha presha kuwa chini na pengine Mgonjwa huwa wa baridi na mgonjwa anashindwa kutulia. Kwa sababu Ugonjwa huu hauna dawa mgonjwa akifikia kwenye dalili hizi anaweza kufariki.
5.Kwa hiyo jamii inapaswa kujua Dalili za Ugonjwa huu na kutoa taarifa kwa wahusika ili kuweza kuokoa maisha ya watu kwa kusaidia kuzuia kuongezeka kwa dalili hali ambayo Usababisha kuwepo kwa vifo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa vipele kwenye midomo na sehemu za siri .Ni ugonjwa ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za uti wa mgongo ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uti wa Mgongo.
Soma Zaidi...Weupe kwenye ulimi unaweza kuwa ni hali ya kawaida. Weupe huu ukichanganyika na utandu huwenda ikaashiria uwepo wa hali fulani za kiafya.
Soma Zaidi...NENO LA AWALI Hapa utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu vidonda vyatumbo.
Soma Zaidi...Post inahusu zaidi athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa wajawazito au ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri.ugonjwa huu uleta madhara kwa wajawazito kama tutakavyoona
Soma Zaidi...Dalili za HIV zina utofauti na dalili za UKIMWI. Kwani HIV huwezakuonyesha dalili wiki ya pili hadi ya sita baada ya kuathirika kisha zinapotea, lakini dalili za UKIMWI huwezakutokea baada ya miaka 5 hadi 10.
Soma Zaidi...Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu kwa kitaalamu anaitwa Anopheles.na anasambazwa na mbu jike pale anapotafuta chakula hasa wakati akiwa na mimba. Mbu hawa hupenda kuishi kwenye mnyasi, madibwi haswa kwenye maji yaliyo simama.
Soma Zaidi...posti hii inazungumziaTetekuwanga . Tetekwanga(varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, kama vile upele. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya mara kwa mara
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ugonjwa wa UTI
Soma Zaidi...