NINI WANACHOKULA MINYOO

NI NINI CHAKULA CHA MINYOO?
Kama tulivyokwisha kuona aina za minyoo, bila shaka umetambua kidogo kuhusu nini wanakifanya wakiwa mwilini. Hivyo basi katika sehemu hii nitakwenda kukueleza chakula cha minyoo ndani ya mwili:-

1.Wanakula chakula tunachokula, katika aina hizi za minyoo wapo minyoo wanaishi kwenye utumbo mdogo. Hii ndiyo sehemu ambayo chakula kinameng’enywa na kuupa mwili nishati na afya yaani kuupatia mwili virutubisho. Lakini minyoo hawa wakati mwingine wanakula chakula alichokula mtu hata kabla ya kumeng’enywa. Hali hii inaweza kusababishia mtu kukosa virutubisho na hatimaye kukonda ama kupoteza usito.

2.Wanakunywa damu, wapo minyoo wengine wanaishi kwenye mfumo wa damu ama ameneo mengine na kuanza kunyonya damu. Minyoo hawa ni hatari sana kwani wanaweza kusababisha ugonjwa wa anaemia. Ugonjwa huu husababishwa na upungufu wa damu.

3.Wanakula viungo vya mwili, katika minyoo hawa kwa mfano liverfluke hawa wanaishi kwenye ini ama maeneo ya nyongo. Minyoo hawa wanakula ini, na kulisababishia vidonda. Pia ini linaweza kuvimba hatimaye kuleta madhara makubwa.

4.Wanakula tishu nyingine, tofauti na hayo tuliyotaja minyoo hawa wanaweza kula tishu nyingine ndani ya mwili. Kama tulivyoona kuna baadhi ya minyoo wanakaa kwenye ngozi, viungio, ini na sehemu nyingine.