Posti hii inahusu zaidi athari za ugonjwa wa Dondakoo,hali hii utokea iwapo ugonjwa haukutibiwa mapema au umetibiwa lakini bado Kuna matokea hasi ambayo yanaweza kujitokeza kama ifuayavyo.
1. Kupumua vibaya kwa mtoto na pengine mtoto anashindwa kumeza au anameza kwa shida.
Ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtoto zinaweza kuwa za kudumu au kwa mda tunajua kuwa ugonjwa huu ushambulia Koo mara nyingine Koo linapata maambukizi makubwa ambayo usababisha mtoto kushindwa kabisa kumeza au wengine wanafaulu kumeza Ila kwa shida kwa hiyo tunapaswa kutibu ugonjwa huu mapema na Tiba yenyewe ni kumpeleka mtoto kupata chanjo kwa kufanya hivyo tutapunguza shida kwenye jamii na watoto tunawaandalia maisha mazuri na yenye natumaini.
2. Kupooza kuanzia kwenye paji la uso mpaka shingoni, kwa sababu ya kuenea kwa bakteria katika sehemu mbalimbali za mfumo wa hewa maambukizi hayo ufanya sehemu hizo kupooza yaani kuanzia kwenye sehemu ya paji la uso mpaka shiy kwa hiyo tunaona hali hii ni ya kuuumiza hasa kwa mtoto na kumsababishis ulemavu wa kudumu kwa sababu zisizi za msingi kama vile Imani potofu juu ya chanjo au kufanya uzembe katika kumpeleka mtoto kupata chanjo kwa hiyo mtoto anakosa furaha na kupata ulemavu wa kudumu katika maisha yake.
3. Maambukizi yanaenea sana .
Kama ugonjwa huu haujadhibituwa usababisha maambukizi kwa watu wengine na kuleta madhara makubwa ambayo yanawaletea wengine ulemavu wa kudumu ambapo kama na wenyewe hawajatambua dalili mapema wanaweza kuendelea kuishi nao, basi jamii inapaswa kujua wazi dalili za ugonjwa huu wa Donda Koo na kujiadhari mapema kuhusu ugonjwa huu.
4. Kwa Sababu ya kuwepo kwa maumivu makali kwenye shingo, kushindwa kumeza na kupumua kwa mtoto, kuvimba shingo kwa mtoto na kupooza kwa mtoto kifo kinaweza kutokea ikiwa mamb o haya haya kutibiwa mapema, kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua kuwa Dondakoo ni hatari kwa watoto na kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata chanjo na kama Kuna Imani potofu kuhusu chanjo jamii inabidi kuwa macho Ili kuondoa Imani hizi potofu.
5. Chanjo ambayo utolewa ni mchanganyiko wa chanjo ya kuzuia kifaduro, Pepopunda, Homa ya inni, hima ya uti wa mgongo, kwa Jina Moja huitwa pentavalent. Kwa hiyo mama au walezi wanaweza kuuliza wataalamu wa afya Ili kuhakikisha kama watoto wao wamepata chanjo ya Dondakoo Ili kuepusha madhara mbalimbali katika jamii yetu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi ambayo kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili inashuka.
Soma Zaidi...Malaria husababishwa na vijidudu vidogo parasite wanaojulikana kama plasmodium. Vijidudu hivi hubebwa na mbu aina ya anophelesi. Kuna ina nyingi za plasmodium lakini aina 5 tu ndizo husababisha malaria
Soma Zaidi...Tonsillitis kwa kiswahili hujulikana kama mafundomafundo ambayo hutokea pande mbili karibu na Koo na huwa na uvimbe na zikikaa kwa muda bila matibabu hutoa usaha.Dalili na dalili za ugonjwa wa tonsillitis ni pamoja na
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba kemikali, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wa saratani, madhara haya yanayoweza kuwa ni kwa Sababu mbalimbali kama vile kuaribika kwa seli zinazoendelea kufanya kazi kwenye mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Magonjwa vya kurithi ambayo mara nyingi utokea kwenye jamii ni magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwenye familia na wanafamilia walio wengi wakaweza kupata ugonjwa huo Magonjwa yenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia upele, ni njia ambazo utumiwa Ili kupunguza tatizo la upele kwenye jamii, kwa hiyo jamii inapaswa kutumia njia hizi Ili kuweza kupambana na ugonjwa huu ambao unatibika.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu. Yafuatayo Ni madhara ya minyoo;
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya moyo, kwa kawaida watu wakisikia habari za magonjwa ya moyo huwa hawaelewi yanakuwaje kuwaje, Leo nataka niwafahamishe kuhusu magonjwa ya moyo na sehemu mbalimbali zinazoathirika.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa, kwa kawaida tunajua wazi kuwa magonjwa yapo na yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mengine hayasambai yanaweza kumpata mtu mmoja akapona au magonjwa mengine si ya kupona
Soma Zaidi...Pumu ni ugonjwa wa njia ya upumuaji unaojulikana na kizuizi cha muda mrefu cha njia ya upumuaji. Inahusisha mfumo wa upumuaji unaobana njia ya hewa, Inaweza kuwa ya nje (hii hutokea kwa vijana kutokana na mizio) au ya ndani (hutokea kwa wazee)
Soma Zaidi...