Aina za minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya aina za minyoo
AINA ZA MINYOO
Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa. Aina hizi ni Minyoo wanaotambulika kama flatworm, roundworm na thory-headed worm. Majina ya minyoo hawa yanafanana na maumbile yako kama tutakavyoona hapo chini. Wengi katika hawa minyoo wanaweza kuonekana kwa macho
Minyoo inayotambulika kama Tapeworm
Hawa ni katika aina za flatworm, minyoo hawa wanaumbo lililo bataa yaani flati. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kunywa maji ambayo yana mayai ya minyoo hawa au lava. Pia unaweza kuwapata. Minyoo hawa kwenye chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuiva vizuri.kama nyama hasa ya ngurue. Karibia nyama za wanyama wote zina wadudu hawa.
Minyoo hawa wanaonekana kama pingili zilizoungana na kutengeneza cheni ndefu. Minyoo hawa wanaweza kuwa warefu mpaka kufikia futi 80 na wanaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu mpaka miaka 30.
minyoo inayotambulika kama flukes
Hawa pia ni katika aina za minyoo waitwao flatworm. Mwanadamu anaweza kuwapata minyoo hawa kupitia maji yasiyo salama,kupitia mboga ambazo hukuwa ndani ya maji.pia kwa kula samaki ambaye ana minyoo hawa. Pia inatokea ukaosha mboga, tunda kwa kutumia maji ambayo yana minyoo hawa.
Minyoo hawa wanapoingia mwilini wanaelekea kwanye utumbo mdogo na huko ndipo huishi, pia maeneo mengine wanapoishi ni kwenye damu, na tishu za mwili kama ini. Kuna aina nyingi za aina hii ya minyoo, lakini ukubwa wao hawazidi nchi kadhaa.
minyoo wanaotambulika kama Hookworm
Hawa ni minyoo aina ya roundworm. Minyoo hawa wanaweza kusambazwa kwa kupitia kinyesina udongo. Hasa kwa wale wanaokula udongo ni rahisi sana kupata aina hii ya minyoo. Njia nyingine nyepesi kwa kupata minyoo hawa ni kwa kutembea miguu peku kwenye udongo ambao una mayai au lava wa aina hii ya minyoo. Malava haya yanaweza kuingia kwenye ngozi yako.
Minyoo hawa wanaishi kwenye utumbo mwembamba, na kwa kuwa kichwani kwao kuna kama miimba ilofanana na ndiwano, wanaitumia kujitundika kwenye utumbo mdogo. Ukubwa wao hauzidi nusu nchi.
minyoo wanaotambulika kama pinworms (threadworms)
Hawa ni katika minyoo wadogo sana na maranyingi hawana madhara. Minyoo hawa ni maarufu sana kwa watoto, walezi wa watoto wadogo na maeneo yeye watoto wadogo wengi unweza kuwapata sana hawa. Wana rangi nyeupe na ukubwa wao hauzindi nusu nchi.
Minyoo hawa unawapata kwa kuyala mayai yao kutoka kwa mtu mwenye minyoo hii. Mayai ya minyoo hawa hayawezi kuonekana kwa macho. Pindi unapokula mayai haya yanakwenda kukaa kwenye utumbo mdogo mpaka kutotolewa. Wakati wa usiku minyoo wanawake wanakwenye chini kwenye puru na kutaga mayai kwenye mikunjo ya puru. Kama mtu atajikuna sehemu ya puru mayai yale yanabakia mkononi zaidi ya masaa kadhaa.
Ikitokea mtu huyu ameshika kitu bila ya kunawa mayai yele yanabaki pale. Kama mtu mwingine akapashika pale na akala kitu bila ya kunawa anaweza akayala mayai yale na kupata minyoo. Pia minyoo hii unaweza kuipata kwa kuvuta hewa yenye mayai ya minyoo hii.
Minyoo hii haina athari zaidi kwa afya lakini mwenye minyoo hii atahisi kuwashwa kwenye puru, ama kuzungukia sehemu ya haja kuwa, wakati mwingine maumivu yatumbo. Wakati mwingine ngozi inawasha sana. Minyoo hawa pia kwa wanawake wanaweza kuhama kutoka kwenye puru na kuelekea kwenye uke wa mwanamke na kuingia ndani. Huenda hali hii ikapelekea kupata UTI na matatizo mengine ya kiaya.
Kupambana na minyoo hawa hakikisha unaosha mikono unapoamka, unapotaka kula chochote, kuingia kwenye choo safi na usipende kushikshika vitu hasa maeneo ya vyoo vya watu wengi. Minyoo hawa ni rahisi kutibika tofauti na minyoo wengine.
minyoo wanaotambulika kama trichinosis worm
Minyoo hawa ni katika minyoo ambao wanapatikana kutoka kwa wanyama. Mtu anaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula nyama ambayo haukuiva vyema, ama kwa kula nyama mbichi. Malava ya minyoo hawa yanakwenda kwenye utumbo mdogo, na huko huweza kuingia kwenye mirija ya damu na kuenda maeneo mengine ya mwili, kwenye misuli na tishu za mwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitau cha Fiqh π2 web hosting π3 kitabu cha Simulizi π4 ai web app π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Dalilili za homa ya manjano
posti hii inahusu dalili za Homa ya Manjano ni maambukizi ya virusi yanayoenezwa na aina fulani ya mbu. Maambukizi hayo ni ya kawaida zaidi na kuathiri wasafiri na wakazi wa maeneo hayo.
Soma Zaidi...Dalili za Upungufu wa Damu kwa Watoto
Upungufu wa damu kwa watoto (Anemia) ni hali inayotokea wakati mwili wa mtoto unapokuwa na kiwango kidogo cha chembechembe nyekundu za damu au protini ya hemoglobin kuliko kawaida. Hali hii ikiachwa bila kutibiwa inaweza kuathiri ukuaji wa kimwili, kiakili, na mfumo wa kinga wa mtoto. Makala hii inaelezea dalili kuu za upungufu wa damu kwa watoto na hatua za kuchukua ili kuwasaidia.
Soma Zaidi...Magonjwa ya kuambukiza.
Posti hii inahusu zaidi Magonjwa ya kuambukiza, ni magonjwa ambayo yanaweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na kuweza kusababisha madhara yale yale kwa mtu aliyeambukizwa au anayeambukiza kwa hiyo Maambukizi yanaweza kuwa ya moja kwa moja au yasi
Soma Zaidi...Upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo.
Post hii inahusu zaidi upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo dalili zake na namna ya kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo hilo.
Soma Zaidi...βDalili za UKIMWI Huchukua Muda Gani Kuonekana?
Watu wengi hujiuliza ni muda gani huchukua kwa mtu aliyeambukizwa virusi vya HIV kuanza kuonyesha dalili za UKIMWI. Makala hii inafafanua hatua tatu za maambukizi ya HIV, muda unaochukua kwa dalili kujitokeza, na kwa nini kupima ndiyo njia pekee ya uhakika ya kujua afya yako.
Soma Zaidi...Visababishi vya maambukizi kwenye milija na ovari
Posti hii inahusu zaidi visababishi vya maambukizi kwenye milija na, ni mambo yanayosababisha maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...